Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  23 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 14
M.  Ijumaa, 31 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Shahidi Mwengine katika Magereza ya Uzbekistan
(Imetafsiriwa)

Ni kwa huzuni na uchungu mkubwa kwamba tunaomboleza kwa Waislamu wa nchi yetu, na kwa Ummah wote wa Kiislamu, mtu mwengine mstahiki ambaye amejiunga na msafara wa mashahidi wa Hizb na akasafiri kwenda kwa masahaba wa juu kabisa. Jana, Mei 30, saa 10 am saa za Tashkent, swala ya janaza iliswaliwa kwa Valiyev Hamidullah. Mmoja wa wanasayansi wetu wa kisiasa waliokomaa (anayejulikana kama Dwamla Qalanfur) kutoka Tashkent, aliuawa shahidi baada ya miaka 25 ya dhulma. Utawala wa Uzbekistan haujaacha kuwauwa wasomi wanyoofu kutoka nchi yetu kwa miaka 25 jela. Wakati huu, ili kuficha uhalifu wake, serikali ya Uzbekistan ilikabidhi mwili wa profesa huyu, ambaye alikuwa kielelezo cha ajabu cha uimara na ujasiri, kwa familia yake kwa njia ya kutisha. Asubuhi ya Mei 28, jamaa zake walipokea simu kutoka gerezani na kuwajulisha kwamba walipaswa kuja mara moja, na kwamba profesa alikuwa mgonjwa. Walipokwenda, madaktari wa hospitali hiyo walisema walikuwa wakiandika taratibu za kuuachilia mwili huo. Kilichokuweko, ni kuwa ingawa profesa alikufa siku nne zilizopita, walimhamisha katika hospitali ya jiji na kumueka mgonjwa huyu kwenye mashini za kutoa msaada kwa uhai. Ni muhimu kutaja kuwa wiki moja kabla ya kifo chake, habari zilienea juu ya kuongezeka kwa ukandamizaji katika gereza ambalo ndugu yetu alikuwa akitumikia kifungo chake...

Tunatoa rambirambi za dhati kwa wanafamilia, jamaa na ndugu wote wa mheshimiwa huyo, na tunasema tena kwamba Profesa Hamidullah alikuwa ni miongoni mwa wasomi ambao kwa hakika walistahiki cheo cha warithi wa manabii watukufu bila ya kutia chumvi. Baada ya yote, katika wakati ambapo maelfu ya wanazuoni wanazitumikia tawala dhalimu zilizoundwa na makafiri wakoloni katika nchi za Kiislamu na kuhalalisha sera zao zisizo za Kiislamu, thamani ya wanazuoni wetu wa kiungu kama Hamidullah inazidi kutambulika. Tazama hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ustaadh Hamidullah imekuwa moja ya hoja za mwisho za Mwenyezi Mungu dhidi ya watu wa idara ya kidini katika nchi yetu. Mufti na maimamu wa misikiti. Je, hawa maimamu wakiongozwa na Mufti watatoa hoja ipi ya kuusaliti Uislamu na Waislamu?! Watakuwaje watakaporegea kwa Mwenyezi Mungu, na wanachuoni wa Mwenyezi Mungu kama Hamidullah kusimama mbele yao? Nyuso zao zitaelekezwa chini. Je, watazingatia kabla ya roho zao kuondoka siku moja?! Pamoja na kwamba Ustadh wetu Hamidullah alipata fursa ya kuishi kwa raha, kwa neema mbalimbali, vyakula, na mavazi, hakukubali kuuza maisha yake ya dunia kwa dini yake. Pamoja na hayo yote, profesa, mithili ya watu wengine wanaodhulumiwa, aliishi robo karne ya maisha yake katika hali za kinyama za jela na shinikizo la kimwili na kisaikolojia, na bado hakusahau ahadi yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amueke ndugu yetu Hamidullah kesho Akhera pamoja na bwana wa mashahidi, Hamza bin Abdul Muttalib, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na amtie katika mabustani makubwa ya peponi aliyowaahidi wale waliouawa kishahidi katika njia yake! Ifahamike kwamba kujitolea mhanga kwa wanavyuoni hawa wa Mwenyezi Mungu kamwe hakutapotea bure, sio katika dunia hii wala kesho Akhera. Hapana shaka kwamba njia yao ya maisha ambayo imekuwa kigezo cha uthabiti, inatimiza tu lengo kubwa, ambalo ni ushindi wa Uislamu na Waislamu, kwa sababu hii ndiyo Sunnah thabiti ya Mwenyezi Mungu katika mapambano baina ya Haki na Batili. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

[ذَلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللهُ لَانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ * سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ * وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ]

“Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao. Atawaongoza na awatengezee hali yao. Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha.” [Muhammad 47:4-6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu