Afisi ya Habari
Uzbekistan
H. 7 Rabi' I 1447 | Na: 1447 / 02 |
M. Jumamosi, 30 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Huku Amerika Ikiunga Mkono Mauaji ya Halaiki mjini Gaza, Inaingia Uzbekistan Kama Mshirika wa Usalama!
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 28/8/2025, Rais Shavkat Mirziyoyev alimpokea Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani wa Ushirikiano wa Kimataifa, Paolo Zampoli. Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Huduma ya Habari ya Rais, “Mkutano huo ulijadili ushirikiano wa kimkakati kati ya Uzbekistan na Marekani na upanuzi wa ushirikiano wa pande nyingi.”
Wakati wa mkutano huo, masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na usalama yalikuwa vipaumbele vya juu. Ilibainika kuwa tukio muhimu zaidi ni mkutano wa ushirikiano wa kimkakati uliopanuliwa, ambao utafanyika msimu huu.
Kwa kuzingatia kasi ya ukuaji wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili, mtiririko wa bidhaa uliongezeka kwa 15% mwaka 2024. Hivi sasa, mkusanyiko wa miradi wa pamoja inazidi $11 bilioni. Kwa mujibu wa huduma ya habari ya Rais, “Ilisisitizwa kuwa ushirikiano thabiti kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za usalama, ugaidi, itikadi kali na uhamiaji haramu utaanzishwa.”
Amerika inatekeleza muundo wa ushirikiano wa kiuchumi kupitia taasisi zake shirikishi: Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, na makampuni ya kifedha. Uwekezaji kupitia taasisi hizi huamsha utaratibu wa shinikizo la kisiasa kupitia shinikizo la deni la mustakabali. Kwa hivyo, uchumi wa nchi na maamuzi ya kisiasa yatakuwa chini ya udhibiti wa Washington. Mfano wazi wa hili ni kwamba deni la umma la Uzbekistan limezidi dolari bilioni 70, na mzigo wa madeni na kodi kwa watu unaongezeka.
Amerika pia inatoa “ushirikiano” katika sekta ya usalama. Swali ni: Marekani imepata usalama wapi? Nchini Iraq, Afghanistan, au Libya? Chini ya kivuli cha kutetea demokrasia, damu ya watu wengi wasio na hatia imemwagika katika nchi hizi kwa miongo kadhaa, na miji na vijiji vimeharibiwa. Mjini Gaza, Amerika inaongoza mauaji haya ya halaiki ya kihistoria kwa uungaji mkono wake mkubwa kwa umbile nyakuzi la Kiyahudi, ambalo linaua makumi ya watoto na wanawake kila siku. Kwa hivyo, ni yakini kwamba kauli mbiu za Amerika, kama vile kupambana na ugaidi na ushirikiano wa usalama, zinaficha kupenya kwa huduma zake za kijasusi nchini, udhibiti wa operesheni za ndani, na mkakati unaolenga kuhakikisha usalama wake yenyewe, sio ule wa Uzbekistan.
Kwa hivyo, njia iliyopendekezwa na Amerika kwa jina la “ushirikiano” kwa kweli ni njia ya hatari na mitego. “Misaada” yake ya kiuchumi ni deni na utegemezi, na ushirikiano wake wa usalama ni tishio la udhibiti wa nje na ukosefu wa utulivu.
Tunaiambia serikali ya Mirziyoyev kwamba kazi yako ya kwanza na ya dharura zaidi ni kutanguliza maslahi ya Uislamu na Waislamu wakati wa kuanzisha uhusiano wowote na mkoloni Amerika, ambayo, pamoja na chuki na matamanio yake ya kikoloni, inatekeleza mauaji na njaa dhidi ya Waislamu kote ulimwenguni, haswa mjini Gaza. Tunaonya kuwa sera yake ya kinafiki inaweza kuiburuza Uzbekistan na eneo zima kwenye michezo hatari ya siasa za kijiografia na kusababisha ukosefu wa utulivu.
Enyi Waislamu wa Uzbekistan: Ushirikiano unaotolewa na serikali kwa jina la “maendeleo ya kiuchumi na usalama” huongeza tu mateso yaliyowekwa juu yenu na dola za kikoloni kama vile Amerika, Urusi, China na nchi za Magharibi. Je, hadi lini mutakaa kimya kuhusu mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi ya serikali hii na ukiukaji wake wa imani yenu, huku ikibeba unyanyapaa wa “watumwa” na “wafanya kazi weusi”? Hata hivyo, je, haya yote si kwa sababu ya “ushirikiano” huu hasa? Suluhisho ni moja: isipokuwa muishi kama Ummah mmoja na Waislamu wote chini ya Khilafah Rashida inayotabikisha Shariah ya Mwenyezi Mungu juu yenu, kamwe hamtakuwa huru kutokana na udhalilifu na utumwa munaoupata leo! Hata hivyo, tunakukumbusheni tena kwamba kumhisabu mtawala wenu, kuchunguza matendo yake kwa kuzingatia hukmu za Shariah, na kumrekebisha mara moja anapokengeuka kutoka kwenye haki—yaani kuamrisha mema na kukataza maovu—ni jukumu lenu. Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[كُنتُمۡ خَیۡرَ أُمَّةٍ أُخۡرِجَتۡ لِلنَّاسِ تَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَتَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ]
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aal-i-Imran: 110].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uzbekistan |
Address & Website Tel: |