Jumatatu, 20 Jumada al-awwal 1447 | 2025/11/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  12 Jumada I 1447 Na: 1447 / 04
M.  Jumatatu, 03 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan Kuhusu Kukamatwa kwa Abdul Aziz Abdul Jalilov
(Imetafsiriwa)

Mnamo 30 Oktoba 2025, Abdul Aziz Abdul Jalilov, mwanachama wa Hizb ut Tahrir kutoka Uzbekistan, alikamatwa katika Shirika la Uhamiaji la Uswidi huko Stockholm.

Kwa ufahamu wetu, Shirika hilo la Uhamiaji limeamua kumrudisha Ndugu Abdul Aziz Uzbekistan.

Katika suala hili, tungependa kulitanabahisha Shirika la Uhamiaji la Uswidi yafuatayo:

Kwanza: Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislamu ambacho amali zake zimefungika na kazi ya kifikra na kisiasa pekee, na kinajiepusha na aina zote za vurugu.

Pili: Kupigwa marufuku kwa Hizb ut Tahrir na mateso ya wanachama wake nchini Uzbekistan ni mambo ya kisiasa tu, kama ilivyotangazwa na wataalamu wengi na watetezi wa haki za binadamu.

Tatu: Kwa miaka mingi nchini Uzbekistan, maelfu ya Mashababu (wanachama) wetu wamekamatwa, na mamia wamekufa chini ya mateso. Wengi wangali wamefungwa hadi leo. Mwaka huu, kesi nyingi za Mashababu wetu zimefanywa, na kwa mara nyengine tena wamehukumiwa kifungo cha muda mrefu.

Nne: Kumrudisha Ndugu Abdul Aziz Uzbekistan kunamaanisha kwamba atakabiliwa, kwa uchache, na kifungo na mateso!

Kwa hivyo, tunakutakeni mubatilishe uhamisho wa Abdul Aziz na mumwachilie huru mara moja.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu