Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  12 Safar 1442 Na: 1442/01
M.  Jumanne, 29 Septemba 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Katika kumbukumbu ya Miaka Sita ya Mapinduzi Yao
Mahouthi Wanabinafsisha Umeme Baada ya Kupandisha Bei za Bidhaa Tanzu za Mafuta na Gesi!

(Imetafsiriwa)

Mahouthi walisherehekea kumbukumbu ya miaka sita ya kuingia kwao Sanaa mnamo Septemba 21, 2014 M, na kama kawaida yake, kwa hotuba ya kurudiwa rudiwa ya kuchosha ya bwana wao duni na butu zaidi Abdul-Malik al-Houthi, ambayo ndani yake aliwaahidi watu wa Yemen kuendelea kwa hali kama ilivyo! Haikushughulikia mafanikio ya kiuchumi ambayo mapinduzi ya Septemba 21, 2014, yaliahidi kwa watu katika kurahisisha mzigo wa kiuchumi kwenye mabega yao baada ya serikali wa Basindawa kukubali kuchukua hatua juu ya mapendekezo ya kirasilimali yaliyooza ya Benki ya Dunia.

Shirika la Umeme la Umma linajiandaa kutoa umeme tena kwa watu wa nchi hii ambao wanataka kuwafikishia kwao kwa bei ya riyal (150-180) kwa badali ya ada ya uingizaji huduma ya riyal 5,000 pamoja na riyal 1,000 kama ada ya usajili wa kila mwezi ili kulipia uokozi wa miaka sita ambapo hawakuona umeme, kwa kuongeza bei maradufu ya kilowatt mara 30 zaidi ya ilivyokuwa kabla ya Septemba 21, 2014 !! Ili Mahouthi wakadirie haya kama mafanikio, waliyaleta baada ya miaka sita ya kukatwa kwa umeme, wakati ambao waliruhusu vituo vya umeme vya kibinafsi vilivyouza kilowatt moja kwa riyal (200-300).

Hili ndilo tunda la pili la mapinduzi ya Septemba 21, 2014, ambayo yalikuja baada ya tunda la kwanza la mapinduzi ambayo kwayo watu wa Yemen walipitia na wangali wanapitia shida, ambayo ni kupanda maradufu kwa bei za bidhaa tanzu za mafuta (2-5) na gesi (3-5) ambapo ilisababisha kupanda kwa bei ya vitu vyote vinavyohusiana nazo. Na kushindwa kwa mapinduzi ya Septemba 21, 2014 kuzirudisha (bei) katika zama zake za awali, riyal 4000 kwa debe (lita 20)  la petroli na dizeli, na riyali 1200 kwa mtungi wa gesi.

Mafanikio ya mapinduzi ya Houthi hayatakoma wakati huu, bali yatakuja kwa mfululizo na kwa kufuatana, na yatakula kila kitu kibichi na kikavu kuanzia kupandisha bei ya juu ya bidhaa tanzu za mafuta, kukata mishahara ya wafanyikazi wa sekta ya umma, na ubinafsishaji wa umeme hadi katika elimu ambayo imekuwa kwa kucha zake - kwa kuwafanya wajinga watu kupitia kuwaweka mbali na elimu - kwa kuwalazimisha wanafunzi walipe riyal elfu moja kwa mwezi na kupangilia kwake elimu ya kibinafsi na kulipisha ada ya masomo, matibabu, barabara, nk ... kama mojawapo ya mafanikio ya "Maandamano ya Qur'an"!! Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambazo zimeilazimisha serikali ya Basindawa, kuondoa ruzuku kutoka kwa bidhaa tanzu za mafuta, ambao wamewanyooshea Mahouthi mikono huku wakishuhudia hili. Mahouthi hawajui kwamba hukmu ya umeme katika Uislamu ni katika mali ya umma ambayo imetokana na msingi wake juu ya umilikaji wa umma – bidhaa tanzu za mafuta na gesi - hivyo hawatofautishi kati ya mali ya kibinafsi na ya umma na mali ya dola!!

Jicho la Aden liko juu ya ubinafsishaji wa viwanda vya kusafisha mafuta vya Buriqa, na Sanaa juu ya ubinafsishaji wa Shirika la Umma la Umeme, moja yao ni mvuke na mwingine ni moto, hivyo mwenye akili hatafuti himaya katika moja ya hizi mbili. Katika siku za zamani, Aswad Ansi mmoja alitokea nchini Yemen - Abahala bin Qais - ambaye alionyesha kujali nchi na watu wake, lakini akaifisidi, na kishawishi chake kikaisha kwa kuondolewa kwake, lakini leo kuna Abahala wengi zaidi!!

Uislamu uko mbali na kila kaulimbiu na vitendo vya Mahouthi ambavyo kwavyo wanatatua mambo ya kiuchumi na mambo mengine ya maisha. Hakika utabikishaji wa Uislamu hautakuwepo ila katika dola ya Khilafah Rashida ya pili, ambayo ndani yake mbingu itanyesheza mvua yake na ardhi itatoa baraka zake zitakazoviridhisha kwazo viumbe vinavyoishi ardhini na viumbe vinavyoishi mbinguni, ambayo Hizb ut-Tahrir inawalingani watu wenye iman na hekima kushirikiana nayo katika kuisimamisha.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Yemen

                      

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu