Jumanne, 15 Jumada al-thani 1443 | 2022/01/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  29 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: HTY- 1442 / 45
M.  Jumamosi, 10 Julai 2021

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Kwa Mujibu wa Mahouthi Kazi ya Kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume ni Uhalifu!

 (Imetafsiriwa)

Kama kawaida, Mahouthi bado wangali wanawazuia Mashababu watatu wa Hizb ut Tahrir - wabebaji ulinganizi wa kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ambao ni, Shaif Al-Shradi, Muhsin Al-Jaadaby na Ayub Al-Shradi, katika kituo chao cha kizuizi jijini Sana'a tangu mwezi uliopita wa Rajab, sio kwa kosa lolote walilofanya isipokuwa kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mkono wa udhalimu umewafikia Mashababu hawa wa Hizb ut Tahrir, baada ya kushiriki kwao katika karne moja ya kuvunjwa kwa Khilafah, 1342 - 1442 H, ambayo iliandaliwa chini ya uongozi wa Mwanachoni, Amiri wa Hizb ut Tahrir, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, katika miji 100 kote ulimwenguni. Na majina yao hayakujumuishwa kwenye orodha ya wafungwa walioachiliwa huru wakati wa vipindi vilivyopita vya mwezi wa Ramadhan na kundi la Houthi chini ya propaganda ya kuwaachilia huru wafungwa wote.

Kumuomba Mwenyezi Mungu asimamishe utawala wa Uislamu ardhini - baada ya kukatizwa kwa miaka mia moja - ni kosa machoni mwa wale wanaodai mwenendo wa Quran na hata kuwaadhibu wale wanaofanya kazi ya kuhukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu!!! Na waliridhika na kuendelea kutengwa kwa Uislamu kutoka kwa usuluhishi katika maswala anuwai ya maisha, na kutawaliwa kwa nchi za Magharibi ambazo zinataka kuiangamiza dola ya Kiislamu - Khilafah, juu ya Waislamu na kuibadilisha na mifumo ya serikali kutoka kwao iliyozaliwa na akili za wanadamu kama vile itikadi batili ya kutenganisha dini na maisha, kuzibadilisha hukmu za Sharia zinazotokana na itikadi ya "Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu", ni tofauti kubwa ilioje! Hukmu za Uislamu ni zenye kuendelea hadi mwisho wa zama, na hukmu za wanadamu huteteleka baada ya miaka mia mbili kupita tangu kuwekwa kwake.

Ongeza kwa hicho kifungu kidogo, kwamba Mahouthi wanazidanganya familia za wafungwa hawa, kwa kutowabainisha watu waliowakamata wana wao kwa nia ya kuwafuatilia na kuficha watu halisi waliowakamata, hivyo watu wawaiteje zaidi ya kuwa ni genge lililochukua udhibiti wa mambo ya serikali? Kwa kuongezea, hawajali afya ya wafungwa wao wagonjwa. Je! Haitoshi kwa Mahouthi udhalilifu wa ulimwengu huu kabla ya kujuta Siku ya Kiyama kwa Mwenye Nguvu, Mlazimishaji, Bwana? Tunatoa changamoto kwa Mahouthi na wengineo kuthibitisha uhalifu wowote dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir.

Wakati huo huo, Mahouthi siku hizi, kwa kuja kwa Idd ul-Adha, wameanzisha kampeni ambayo kwayo wanafanya kazi ya kuwaachilia huru wafungwa wao kutoka katika magereza ya wale wanaowapiga vita na kumwaga damu yao.

 [مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ]

“Mna nini? Mnahukumu vipi?” [Al-Qalam: 36]. Wafungwa wenu wana haki zaidi ya kuachiliwa huru, na wamefanya kile walichofanya na kupigana, na wafungwa kutoka Hizb ut Tahrir hawana kuachiliwa huru, kwa kuwa wamefanya jambo la kinyama?!

Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa kinachofanya kazi katika nchi zaidi ya 40 ulimwenguni, hivyo basi siasa, kuchunga mambo, ni kazi yake na Uislamu ndio mfumo wake, na njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ndio njia yake ya kusimamisha utawala wa Uislamu, kama vile Mtume (saw) alivyosimamisha dola iliyohukumu kwa Uislamu mjini Madina Munawarah, baada ya kuanzisha kikundi chake na wanaume ambao walilelewa kwa msingi wa Aqeedah ya Tawhiyd (Upweke wa Mwenyezi Mungu), na fikra na hukmu za Uislamu, ili Uislamu uwe ndani yao, kwa hivyo waliingia katika mvutano wa kifikra na fikra yasizokuwa za Kiislamu, kwa hivyo wakazishinda baada ya kuelezea ufisadi wake, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alishinda Nusrah kuchukua utawala baada ya kuitafuta. Kwa hivyo, dola ikaanzishwa kwa ajili Waislamu iliyomsumbua Shetani, kwa hivyo amekuja kuiangamiza, kama vile kusimamishwa kwa dola ya Khilafah Rashida ya pili inavyoutingisha uovu wa ulimwengu leo ​​kuzuia kusimamishwa kwake. Wanawezaje kufanya hivyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameahidi kuwanusuru waumini wanaofanya kazi kuisimamisha katika maisha haya na yajayo? Mwenyezi Mungu (swt) asema:

إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ﴿

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Ghafir: 51].

Na Muhammad (saw) ametupa bishara njema ya kusimama kwake:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” (Imesimuliwa na Ahmad kutoka kwa al-Nu'man ibn Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu