Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 6 Shawwal 1445 | Na: HTY- 1445 / 29 |
M. Jumatatu, 15 Aprili 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Huku kukiwa na Maandamano, Makongamano, na Kauli Mbiu Tupu, Palestina ingali Inakaliwa Kimabavu hadi Itakapokombolewa!
(Imetafsiriwa)
Sana'a na idadi kubwa ya miji nchini Yemen ilishuhudia maandamano makubwa mnamo Ijumaa, 26 ya Ramadhan, 1445 H, sawia na Aprili 6, 2024, kwa mnasaba wa ya Siku ya Kimataifa ya Al-Quds.
Siku ya Al-Quds sio tu kuhusu kuzikomboa Al-Aqsa na Al-Quds kutokana na najisi ya Mayahudi, kama wengine wanaweza kufikiria. Karibu miaka hamsini imepita tangu kuanzishwa kwake, na maadhimisho yake ya kila mwaka, lakini ulimwengu umeona maandamano tu!
Siku ya kimataifa ya al-Quds (Jerusalem) (Kifursi: روز جهانی قدس) ilizinduliwa na Khomeini mnamo 1979 “ ili kuhamasisha na kuonyesha na kunyanyua utambuzi miongoni mwa Ummah,” kama walivyoiweka, mnamo Ijumaa mwisho ya Ramadhan. Ilianzishwa hapo awali na Majusi wa Kisasani Jumatano ya mwisho ya mwaka kabla ya Mwaka Mpya wa Kifursi kusherehekea Nowruz kwa kuwasha moto na kuruka juu yake ili kujiondolea magonjwa kabla ya kuandaa sahani kuu saba zikianzia na herufi “S”!
Wasiokuwa Waislamu pia wanashiriki katika Siku ya Kimataifa ya Jerusalem, hata umbile la Kiyahudi linasherehekea Siku ya Jerusalem kama sikukuu ya kitaifa, kukumbuka kuunganishwa kwa Jerusalem Mashariki kufuatia "Usanii" wa 1967. Sio sikukuu rasmi nchini Iran kama Nowruz, ambayo inaashiria mwanzo wa mwaka katika kalenda ya Kifursi. Siku ya Kimataifa ya Al-Quds imeanzishwa kwa sherehe sawa na Siku ya Walimu, Siku ya Wanawake, Siku ya Arbor, na sikukuu zingine zinazosherekewa na Umoja wa Mataifa, ikialika ulimwengu kuziadhimisha kwa tarehe maalum kila mwaka. Umoja wa Mataifa umetabanni Nowruz kwani inaashiria usawa wa mchana na usiku kwa mwaka mzima, ukiizingatia kuwa sikukuu rasmi, ukidai inaambatana sana na chata za UNESCO katika kukuza tamaduni tofauti tofauti na urafiki miongoni mwa watu na jamii mbali mbali!
Kwa kuongezea, Sana'a alishuhudia mnamo Jumatano, 24 Ramadhan 1445 H, kongamano lililopewa jina la “Palestina: Kadhia Kuu ya Ummah,” la pili la aina yake lililofanyika jijini Sana'a, Yemen, sawa na Kongamano la Kimataifa la kuunga mkono Mapinduzi ya Palestina linalofanyika jijini Tehran kila miaka michache.
Maandamano haya yote ya “Watu Mamilioni” na makongamano hufanyika ili kukusanya huruma ya watu na kuwahadaa wafuasi – huku vita nchini Yemen vikikaribia mwisho wake – kuamini kwamba wako kwenye njia ya kuikomboa Al-Quds. Walakini, hizi ni kauli mbiu tupu. Uko wapi Uislamu wapi katika utawala wao nchini Yemen?! Yeyote anayenyanyua bendera ya Uislamu na kudai kuunga mkono njia yake, iwe Palestina au kwengineko, lazima kwanza atabikishe Uislamu kwa maneno na vitendo.
Haiwezekani, katika miradi miovu ya Kimagharibi dhidi ya Uislamu, kupeana dori kwa Ibn al-Alqami, sawa na dori yake katika uvamizi wa Tartar wa ardhi za Waislamu, kupanga kwa ajili ya mhimili wa upinzani unaoongozwa na Iran nyuma ya sherehe ya kimataifa ya Siku ya al-Quds na kuitisha makongamano ya Quds. Hii inaweza kusababisha vita vya kikanda kati yake na Operesheni Mlinzi wa Ustawi, na kuipatia udhibiti kamili juu ya Hormuz na Mlango wa Bab al-Mandab, Bahari ya Arabia, na Bahari Nyekundu. Kafiri Magharibi hutumia njia zake bora za kuzuia Uislamu kufikia madarakani na kuweka nchi za Kiislamu chini ya utawala wa watawala vibaraka ambao huvuruga watu kwa fikra ya madhehebu na maswala mengine, wakiwakengeusha kutoka kwa Dini yao na njia zao za kweli. Palestina inasalia kuwa chanzo tu cha kauli mbiu kwa kile kinachoitwa Mhimili wa Upinzani. Kama Ali Khamenei alivyosema kwamba Iran leo iko katika harakati za kujijenga na haiko tayari kwenda vitani na ‘Israel’ kwa niaba ya Hamas.
Haipaswi kusemwa kwamba wale wanaofichua kile kinachojulikana kama Mhimili wa Upinzani wameunganishwa na serikali zingine, kwa watawala wengine, iwe nchini Uturuki, Ghuba, Misri, au nchi zingine za Kiislamu, wameingia ndani ya utumwa kuanzia kichwani hadi miguuni. Tuko hapa kumfichua kila anayefanya biashara na kadhia za Waislamu na washirika na Kafiri Magharibi. Tunalingania wazi kusimamishwa kwa dola ya Waislamu ambayo inatabikisha Uislamu ndani na kubeba Uislamu kama ujumbe wa mwongozo na nuru kwa ulimwengu, na kuondoa mipaka na vizuizi kati yao na kuwafagia watawala vibaraka na maovu yao yote katika kaburi la sahau.
Leo, watu wa Yemen hawana chaguo ila kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kwani ndiyo itakayo nyanyua bendera ya Uqab na kukabiliana na zile njama ovu, ikikomboa ardhi za Waislamu zilizokaliwa kimabavu.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfal:24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |