Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 27 Rabi' II 1447 | Na: HTY- 1447 / 07 |
M. Jumapili, 19 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa wafikia Kukaba Uchumi wa Yemen ili Kukamata Rasilimali Zetu za Kiuchumi
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 15/10/2025, Gavana wa Benki Kuu ya Aden, Ahmed Al-Maabqi, alikutana jijini Washington D.C., na mkuu wa ujumbe wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) nchini Yemen, Esther Pérez Ruiz, na mwakilishi wa IMF, Mohamed Maait, akiandamana na Naibu Waziri wa Fedha Hani Wahab na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Waziri Msaidizi wa Fedha Abdul Qader Amin. Hii ilifuatiwa na mkutano kati ya Waziri wa Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa na Gavana wa Yemen kwa Benki ya Dunia, Waed Badhib, na Riccardo Puliti, Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa wa Kanda ya Mashariki ya Kati, pamoja na ushiriki wa Naibu Waziri wa Mipango Nizar Basuhaib, Naibu Waziri wa Fedha Hani Wahab, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Abdul Qader Amin, kwa uwepo wa Stefan G. G. Reimbert, Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia katika Mashariki ya Kati, na Dina Abu Ghaida, Meneja wa Benki ya Dunia nchini Yemen.
Mikutano hii miwili ilitanguliwa na mashauriano ya maandalizi yaliyofanyika Amman mnamo tarehe 8 na 9 Oktoba 2025 kati ya ujumbe wa IMF na serikali ya Aden, ikiwakilishwa na Waziri Mkuu Salem Saleh bin Breki na Gavana wa Benki Kuu Ahmed Al-Maabqi, chini ya jina la “Mashauriano ya Kifungu cha 4” kati ya Yemen na IMF, ikifuatiwa na utoaji wa taarifa ya kuhitimisha.
Mkutano wa kwanza ulijadili njia za kuendeleza mipango na programu za IMF nchini Yemen, ambazo zimesitishwa tangu 2014, na dori yake tya kiufundi na ushauri, kama vile kusaidia uhuishaji wa sarafu ya nchi hii kwa kuleta utulivu wa kiwango cha ubadilishaji, kuboresha viwango vya akiba za kigeni, na kuimarisha utulivu wa kifedha nchini kupitia mpango mkuu wa mageuzi ya kimali na kifedha, na kuendelea mageuzi ili kuhakikisha mtiririko wa mikopo ya kigeni, ambayo Esther Ruiz ameitaja kama “kujitolea kikubwa kwa ajili ya mageuzi ya kifedha na kiutawala.”
Ama kuhusu mkutano wa pili – ambao ni hatari zaidi – ulilenga kuwezesha kupenya kwa Shirika la Fedha la Kimataifa nchini Yemen chini ya pazia la sekta ya kibinafsi ya kigeni kupitia dirisha la uwekezaji, ambalo kwa sasa linafanya kazi kwa kiasi kidogo cha dolari milioni 15.9 katika sekta za chakula na afya, huku wale walio nyuma yake wakiweka macho yao kwenye uvuvi, mawasiliano ya simu na nyaya za chini ya bahari, miradi ya mauzo ya umeme, na mwisho viwanja vya mafuta.
Kabla ya ujumbe wa serikali kuruka kuelekea Washington, mabalozi wa dola mbili za kikoloni – Abda Sharif wa Uingereza na Katherine Corm Kammoun wa Ufaransa – walifanya mikutano tofauti jijini Amman pamoja na ujumbe wa Yemen, wakitoa “usaidizi” wa nchi zao na kutangaza “kuunga mkono” kwao juhudi za utulivu na maendeleo za Yemen, huku ujumbe wa serikali ukipokea maagizo ya kutii. Hii haishangazi kwa watawala vibaraka kama hao.
Je, watu sasa wanaelewa kuwa kuzorota kwa janga la kiuchumi lililoendelea tangu mwanzoni mwa 2025 hadi 31/07/2025 kunahusishwa moja kwa moja na programu za IMF? Kwamba usipoiendea na kuiomba, itaharibu uchumi wako kwa sababu umefungamana na mipango yake na uchumi wa kibepari? Ili kuelewa uhalisia huu, soma “Confessions of an Economic Hit Man” ya John Perkins, ambayo inafafanua jinsi mipango kama hiyo inavyopangwa na ala zinazotumiwa kuitekeleza.
Vituo vitatu hatari – 1975, wakati Benki ya Dunia ilipofanikiwa kufungua afisi ya siri ndani ya Benki Kuu ya Sana'a; 1995, wakati Benki ya Dunia iliweka mageuzi ya kifedha na kiutawala; na 2011, wakati IMF ilipoingia – kupitia hatua hizi, uchumi wa Yemen ulihusishwa sana na uchumi wa kibepari. Hili limeleta madhara makubwa kwa Yemen, na watu wake lazima wajikomboe kutoka kwenye mshiko wake, ambao umekusudiwa kuiweka Yemen kufungwa milele. Maadamu mfumo wa kibepari unaendelea kutekelezwa nchini Yemen na maeneo mengine ya ardhi za Kiislamu, hatutatoka katika hali hii ya janga; badala yake, tutazama katika mgogoro mpya kila siku.
Furaha ya kiuchumi na ustawi wa watu wa imani itaambatana na nyanja zote za maisha – kisiasa, kijamii, mahusiano ya kimataifa, na mengineyo – chini ya hukmu ya Uislamu ndani ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Hili ndilo suluhisho pekee msingi. Inasikitisha kwamba suluhisho hili si jambo kuu la Ummah katika makundi yake yote. Hizb ut Tahrir inalifanyia kazi, na hatutachoka wala hatutakata tamaa bali tutaendelea kulibainisha kwa watu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[هَذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ]
“Hii ni bayana kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamngu.” [Aal-i Imran: 138].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |