Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 594
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika siku ya tatu ya Idd al-Fitr Iliyobarikiwa, sawia na Jumamosi, 12 Machi 2026 M, mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walikusanyika katika afisi ya hizb katikati mwa jiji la Khartoum ili kupeana salamu za Idd. Mkutano huo ulijumuisha mashababu kutoka kote Khartoum, Omdurman, Jabal Awliya, Kalakila, Nile Mashariki, na maeneo mengine. Walitoa pongezi zao kwa Idd iliyobarikiwa na kuelezea furaha yao ya kuonana baada ya miaka mingi ya vita.
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki, kupitia matembezi mikubwa na taarifa kwa vyombo vya habari zilizoandaliwa kote Uturuki chini ya kauli mbiu “Iokoeni Al-Aqsa! Simameni dhidi ya Amerika!”, ililaani ukandamizaji wa umbile nyakuzi la Kizayuni, kiburi cha mkoloni Amerika, na kimya cha watawala wa nchi za Kiislamu kuhusu udhalilishaji huu.
Je, ni nini maana ya kauli za Trump zenye kusitasita—kutoa Iran masaa 48, kisha siku 5, kisha siku 10—na pendekezo lake la mpango wenye nukta 15? Namna gani ujanja wa kauli, nyingi kutoka kwa Trump na chache kutoka kwa Iran, na tangazo la televisheni ya Iran kukataa pendekezo la Trump? Matokeo ya hayo yote ni nini?
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki iliwasilisha taarifa kwa vyombo vya habari yenye hoja kumi kwa Umma wa Kiislamu wakati wa mkutano na waandishi wa habari, yenye kichwa cha habari: “Vita dhidi ya Iran: Ukafiri ni Mila Moja, Na Waislamu ni Umma Mmoja”
Pongezi za Kitengo cha Wanawake kwa Mnasaba wa Ujio wa Idd ul-Fitr Iliyobarikiwa 1447 H
Al-Waqiyah TV: Pongezi za Kundi la Wabebaji Da’wah kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Iliyobarikiwa 1447 H
Baada ya kuchunguza mwezi mwandamo wa Shawwal katika usiku huu mtukufu, usiku wa Alhamisi, kuonekana kwa mwezi mwandamo kumethibitishwa kwa kuonekana halali kisharia katika baadhi ya nchi za Waislamu. Kwa hivyo, kesho Alhamisi itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na siku ya kwanza ya Idd al-Fitr iliyobarikiwa.