Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nidhamu ya Kuadhibu ya Kiislamu 

Ni baraka za Mwenyezi Mungu (swt) kumtuma Mtume wake na Dini ya Haki (Uislamu) na kutubariki sisi na Khilafah ambayo kupitia kwake Ummah wa Waislamu wanabeba jukumu la kulingania ujumbe wa Uislamu kwa wanadamu. Uislamu sio tu dini bali ni nidhamu kamili inayosimamia kila nyanja ya maisha yetu – ima ni akhlaqi au vitendo vya ibada au ni siasa, uchumi au masuala ya kijamii au ni masuala yanayohusiana na sera ya kigeni au nidhamu ya elimu – Uislamu una ahkaam (maamrisho na makatazo) ambayo yanatupa muongozo kamilifu juu ya masuala yote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ عَمَّا جَاءكَ مِنَ الْحَقِّ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا)

“Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake.” (5:48) Hivyo basi, Shari'ah ambazo zilizomshukia Mtume wetu (saw) kwa njia ya Qur'an na Sunnah zimejumuisha ndani yake ahkaam kuhusiana na mahakama, uhalifu, viapo, ushahidi na adhabu ambazo zinatekelezwa na Dola ya Kiislamu.

Kwa miaka 1300, Khilafah ilikuwa ikiwatekelezea haki raia wake kwa kuwatekelezea sheria hizo mfano katika eneo la India lilikuwa likisimamiwa na sheria za Kiislamu mpaka Waingereza walipowasili na kuzifutilia mbali. Tokea wakati huo mizozo baina ya watu ina hukumiwa kwa Ukafiri (sheria ambazo sio za Kiislamu). Baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni Waingereza, Waislamu walitakiwa watekeleze sheria za Kiislamu kuhusiana na adhabu. Lakini, uongozi wa kisiasa wa Pakistan ulijisalimisha kwa utawala wa kifikra wa Kimagharibi na kuchukua sheria za Uingereza zikiwa na tofauti ndogo, hivyo kuyatelekeza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt).

 (وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ) “Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu." [TMQ 5:47] Kuzidi kwa viwango vya uhalifu leo nchini Pakistan ni kutokana na kutotekelezwa kwa hukumu za nidhamu ya adhabu ya Kiislamu.

Ili kulemaza hisia za Waislamu, adhabu chache za Kiislamu zimetekelezwa na pia zikiwa hazina ikhlass ndani yake kama inavyoshuhudiwa katika utekelezwaji wake ambapo muundo wa mahakama, sheria za viapo, ushahidi na utambulishwaji wa uhalifu zimekitwa kwa mujibu wa fikra za Ukafiri. Hivyo basi, rai ya eti "Hukumu za Kiislamu" hazikuacha athari yoyote muhimu katika maisha ya Waislamu.

Miongo ya muendelezo wa utekelezaji wa sheria za Ukafiri zimeziba sura ya mahakama na nidhamu ya adhabu ya Uislamu katika akili za Waislamu leo. Zaidi ya hayo, athari ya thaqafa ya Kimagharibi kutokana na kupigiwa debe na wakoloni imeteka akili za Waislamu kiasi kwamba imefikia kuuliza baadhi ya masuali kwa sheria za Kiislamu. Lengo la Makala hii ni kuonyesha namna nidhamu ya adhabu ya Uislamu ilivyo. Mwenyezi Mungu (swt) awaongoze Waislamu kuweza kutekeleza Shari'ah ya Muhammad (saw) kwa ukamilifu kupitia kusimamisha tena Khilafah na Yeye (swt) atubariki tuwe na mujtama wa Kiislamu ambapo uhalifu utakuwa mchache kiasi kwamba ni vigumu kuusikia. 

Aina za Adhabu (Uqoobah)

Kuna aina nne za adhabu za kiShari'ah:

1. Hudood (adhabu ambazo zimekatika)

2. Jinayaat (adhabu za uhalifu)

3. Ta'zeer (adhabu ambazo hazijakatika)

4. Mukhalafaat (adhabu za kwenda kinyume)

Maana ya uhalifu kiShari'ah

Kabla kuingia kina katika kila aina ya adhabu, ni muhimu kuelewa maana ya uhalifu kwa mujibu wa Shari'ah. Hukumu za kiShari'ah zinazohusiana na vitendo vya mwanadamu ni tano: faradhi (lazima), mandub (imependekezwa), mubah (imeruhusiwa), haramu (imekatazwa) na makruh (haipendezi). Faradhi ni amrisho la lazima kufanywa na ukiliacha wapata dhambi, mandub ni amrisho ambalo ukilifanya wapata thawabu na usipolifanya hupati dhambi, mubah ni amrisho ambalo ukilifanya hupati thawabu na usipolifanya hupati dhambi, haramu ni amrisho ambalo ukilifanya wapata dhambi na makruh ni amrisho ambalo ukilifanya hupati dhambi na ukiliwacha wapata thawabu.

Vitendo ambavyo adhabu zimewekwa juu yake ni vile vya kutelekeza faradhi, kutenda haramu na kwenda kinyume na maagizo ya Serikali ya Kiislamu. Kosa (uhalifu) ni kitendo baya (qabeeh) ambacho Shari'ah imekifanya ni kosa; ima kitendo hicho kiwe kinaingia chini ya haramu (kimekatazwa) au Shari'ah imeweka adhabu maalum kwa kitendo hicho. Hivyo basi, vitendo haviwi uhalifu ikiwa Shari'ah haijasema hivyo.  Hivyo basi, kiujumla hakuna adhabu juu ya vitendo vya makruh na mubah. Lakini, Shari'ah imempa Khalifah haki ya kutoa maagizo ya adhabu kwa ukiukaji baadhi unaoingia katika Mukhalafaat mfano ukiukaji kuhusiana idara ya Serikali ya Kiislamu, ujenzi wa majengo na sheria za barabarani n.k. Zaidi ya hayo, hakuna adhabu kutokana na kutelekeza mandub au kufanya kitendo cha makruh kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) ana adhibu tu kwa kutotenda faradhi na kutenda haramu.

Hivyo basi, vitendo vyote ambavyo vimejumuishwa katika uhalifu ima vinatokamana na maarisho na makatazo au vinatokamana na tabbani ya Khalifah kwa mujibu wa ijtihad na ndio vilivyo na adhabu chini ya nidhamu ya adhabu ya Kiislamu.

Kwa nini kuweko na sheria za kuadhibu?

Kutenda uhalifu hakupo ndani ya maumbile ya mwanadamu. Na pia sio maradhi ambayo yamemuathiri mwanadamu. Bali ni kukiuka nidhamu ambayo imempangia mwanadamu vitendo vyake.

Mwenyezi Mungu (swt) alimuumba mwanadamu na akaumba ghariza na mahitaji ya kiviungo ndani ya mwanadamu. Ghariza na mahitaji ya kiviungo ni nishati muhimu ndani ya mwanadamu ambayo humpelekea kushibisha. Kwa hivyo mwanadmu hutenda vitendo vyake ili kuweza kushibisha. Kuacha kushibisha ghariza na mahitaji ya kiviungo pasina nidhamu husababisha vurugu. Hivyo basi, ili kupangilia vitendo vya mwanadamu, Mwenyezi Mungu (swt) akateremsha ahkaam al-Shari'ah (sheria za Kiislamu) ambazo zinatupa muongozo kamilifu juu ya vitendo vyetu. Mwenyezi Mungu (swt) aliweka hukumu katika halali (zimeruhusiwa) na haramu (zimekatazwa). Mwenyezi Mungu (swt) alimhutubia mwanadamu kufanya vitendo ambavyo ni faradhi au kujiepusha na vitendo vya haramu. Hivyo basi, yule anaye telekeza faradhi au anaye tenda haramu amefanya kitendo kibaya (qabeeh) na hivyo kustahiki kuadhibiwa.

Kwa kukosekana adhabu, mujtama hauwezi kuhifadhika na maovu kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt) (وَلَكُمْ فِي ٱلْقِصَاصِ حَيَوٰةٌ) “Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi.” (TMQ 2:179). Mwenyezi Mungu (swt) ameelezea kuhusu kulipiza kisasi kwamba ni kitu kinacho okoa maisha katika mujtama. Hili sio kwa kuokoa maisha ya yule aliyeadhibiwa kwa kuwa kulipiza kisasi adhabu yake ni kifo na sio uhai wake, bali kwa yule anayeshuhudia kufanyika kwa kisasi katika mujtama. Mtu mwenye akili anajua kuwa atauliwa ikiwa ataua mwengine. Hivyo basi, ina mkanya asifanye kosa la kuua na hivyo kuulinda mujtama.

Zaidi ya hayo, adhabu itakayo tekelezwa na Dola, hapa duniani kwa mujibu wa dhambi maalum basi itaondosha adhabu akhera, kwani yule ambaye alipewa adhabu ataomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu (swt). Mtume (saw) alisema,        

«وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا، فَعُوقِبَ فِي الدُّنْيَا، فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَهُ. وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا، ثُمَّ سَتَرَهُ اللَّهُ، فَهُوَ إِلَى اللَّهِ، إِنْ شَاءَ عَفَا عَنْهُ، وَإِنْ شَاءَ عَاقَبَهُ»

“Yeyote anayetenda kitendo cha dhambi na akapewa adhabu ya kiShari'ah kuhusiana na hilo, itahesabiwa ni kafara ya dhambi hilo, na yeyote anayetenda dhambi lakini Mwenyezi Mungu akalificha, basi itakuwa ni kwa Mwenyezi Mungu ima amsamehe au amuadhibu." Na Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ)

“Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye Kusamehe, Mwenye Kurehemu." [39:53]

Katika historia ya Kiislamu hususan wakati wa Dola ya Kiislamu ya Madina, tunaona kwamba wale waliofanya zinaa walijiwasilisha kwa hiyari yao wenyewe mbele ya Mtume (saw) na baada ya mchakato maalum, yeye (saw) akatangaza hadd (adhabu) juu yao. Hivyo basi, ili kumridhisha Mola wao (swt) na kupata huruma Yake, watu aina hiyo walijisalimisha wenyewe ili waweze kuokolewa na Moto kwa gharama ya adhabu ya duniani.

Hivyo basi, tunapata mazingatio au manufaa kutoka kwa adhabu kwa ujumla. Kwanza, adhabu ni kinga kwani zinawakinga watu kutokana na kufanya uhalifu. Hivyo basi, uhai, mali na heshima zinalindwa kwa kuwa mujtama umekingwa na uhalifu kwa kujifunga kikamilifu kwa kutekeleza adhabu kwa njia ambayo hakuna hata mmoja atakaye fikiria kufanya kosa lolote. Pili, adhabu zinaondosha adhabu za akhera kwa kuwa mtu atamuomba Mwenyezi Mungu (swt) msamaha kama ilivyo elezewa hapo juu.

Nani aliye na mamlaka ya kutekeleza Uqoobaat (adhabu)?

Mamlaka ya kutekeleza adhabu za kiShari'ah yako kwa Khalifah (au Imamu) ambaye anatekeleza adhabu hizo kupitia maagizo ya Dola. Hakuna mtu au shirika ambalo lina haki au jukumu la kutekeleza adhabu kwa watu. Kwa sababu Khalifah anapata mamlaka yake kutoka kwa Ummah kupitia bay'ah (ahadi ya utiifu) na Ummah nao unampa bay'ah kwa sharti kwamba atatekeleza sheria za Kiislamu ndani ya Dola. Kinyume na makundi au mashirika kwani hayana bay'ah kutoka kwa Ummah ili ziwahukumu wala hayatambuliwi kama “Ulil Amr” (wale walio na mamlaka).

Hivyo basi, Khalifah anasimamia mambo ya watu, ana tabbani hukumu za kiShari'ah katika utekelezwaji ndani ya Dola ya Kiislamu na kuwaadhibu wale wanao kiuka sheria hizo.

Mtume (saw) alisema, «الإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْؤولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imamu (Khaleefah) ni mchungaji (ana majukumu) kwa watu aliopewa mamlaka juu yao.”

Aina za adhabu za Kiislamu na maelezo yao kwa kifupi

Adhabu za kiShari'ah zimegawanyika aina nne, kama ifuatavyo:

1. Hudood
Shari'ah imeelezea kuwa Hudood ni adhabu zilizopo kwa mujibu wa vitendo vya kihalifu (haramu). Kuadhibiwa kwake ni haki ya Mwenyezi Mungu (swt) na sio wanadamu au Dola. Hivyo basi, adhabu hizo zimetajwa waziwazi katika kitabu, na mtawala au anaye tawaliwa hana haki ya kupunguza au kuondosha adhabu hiyo kwa niaba ya Mwenyezi Mungu (swt). Zinaitwa Hudood, kwa sababu kwa ujumla zinamkinga mwenye kutenda dhambi asirudie kulitenda dhambi hilo ambalo ameadhibiwa kwa hadd (adhabu). Kwa mfano, Mwenyezi Mungu (swt) ameagiza,

(الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ وَلاَ تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ)

“Mzinifu mwanamke (ambaye hajaolewa) au mwanamume (ambaye hajaoa) mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu” (24:2) na

(وَٱلسَّارِقُ وَٱلسَّارِقَةُ فَٱقْطَعُوٓا أَيْدِيَهُمَا جَزَآءًۢ بِمَا كَسَبَا نَكَٰلًا مِّنَ ٱللَّهِ)

“Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu.” (5:38).

Hivyo basi, hudood ni adhabu zilizo katika kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ambazo zinatekelezwa na mamlaka ya Dola ya Kiislamu.

Kwa mtizamo huu, kuna hadith maarufu ya Rasulullah (saw)

«وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ كَانَتْ فَاطِمَة بِنْت مُحَمَّدٍ، لَقَطَعْت يَدَهَا»

“Naapa kwa Yule ambaye Mkono Wake imo roho yangu! Lau Fatima (binti ya Mtume (saw)) angelifanya hili (angeiba), ningelimkata mkono wake." (Sahih Bukhari 6787).

Hivyo basi, kwa mujibu wa riwaya sahihi haina shaka kuwa hakuna aliye na mamlaka ya kumsamehe mtu ambaye amehukumiwa hadd kwa kosa la kiuhalifu. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) hakutaja kuhusu kafara ya uhalifu. Lakini, lau mtu aliyefanya dhambi akatubia kwa ikhlass na akaadhibiwa kwa hadd basi hapo ndipo atakapo samehewa akhera.

Mwenyezi Mungu (swt) ametufahamisha sisi,

 (قُلْ يَاعِبَادِي الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لاَ تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ)

“Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye Kusamehe, Mwenye Kurehemu." [39:53]

Hivyo basi, uhalifu kama sariqa (uwizi), zinaa, liwat (ngono ya jinsia moja), kunywa khimr (pombe), irtidaad (kuritadi), qadhf (shutuma za zinaa), qutaa’ al-turooq (uwizi wa barabara kuu) na uasi unaingia katika hudood ambazo lazima zitekelezwe na Dola ya Kiislamu na ambazo hazina kafara duniani.

2. Jinayaat                                                                                                                                                      Ama kuhusu jinayaat (makosa ya kihalifu) Shari'ah imejumuisha adhabu baadhi katika kikundi hichi. Adhabu hizi zinapewa wale waliotekeleza uhalifu (vitendo vya haramu) ambavyo kuadhibiwa kwake ni haki ya binadamu. Kwa hivyo, mtu ambaye haki yake imekosewa kwa sasabu ya uhalifu ana wezeshwa na Shari'ah ima kulipiza kwa kutaka adhabu au kumsamehe muhalifu kwa mujibu wa hukumu za Kiislamu. Kuua mwanadamu pasina na hatia au kumdhuru kimwili ni makosa ya jinai yanayoadhibiwa kwa mujibu wa Shari'ah. Mwenyezi Mungu (swt) ameagiza:

(كُتِبَ عَلَيْكُمُ ٱلْقِصَاصُ فِى ٱلْقَتْلَى ٱلْحُرُّ بِٱلْحُرِّ وَٱلْعَبْدُ بِٱلْعَبْدِ وَٱلْأُنثَىٰ بِٱلْأُنثَىٰ)

“Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa- muungwana kwa muungwana, mtumwa kwa mtumwa, mwanamke kwa mwanamke." (2:178).

Lakini, lau warithi wa kiShari'ah wa mtu aliyedhuriwa wanataka kumsamehe mkosaji, basi wanaruhusiwa kufanya hivyo kwa kutaka diyyah (pesa za damu) kutoka kwa mtu aliyetenda uhalifu kama alivyotufahamisha Mwenyezi Mungu (swt),

(فَمَنْ عُفِىَ لَهُۥ مِنْ أَخِيهِ شَىْءٌ فَٱتِّبَاعٌۢ بِٱلْمَعْرُوفِ وَأَدَآءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَٰنٍ)

“Na anaye samehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani."  (2:178).

Rasulullah (saw) alisema,

«مَنْ قُتِلَ لَهُ قَتِيلٌ فَهُوَ بِخَيْرِ النَّظَرَيْنِ إِمَّا أَنْ يَقْتُلَ وَإِمَّا أَنْ يُفْدَى»‏

“Lau mtu ndugu yake ameuliwa, anaweza kuchagua mambo mawili: Anaweza kuchagua muuaji auliwe, au anaweza kutaka pesa za damu." (Sunan Ibn Majah 2624).

Mfano wa uhalifu unaostahiki adhabu au pesa za damu zinajumuisha kuua kimakusudi, kuua bila kukusudia, kudhuru mwili n.k.

3. Ta’zeer

Ta'zeer ni adhabu ambazo hazijakatika na hupewa mtu kutokana na dhambi ambalo halina hadd (adhabu za kukatika) ndani ya Qur'an na Sunnah. Lau muhalifu atapewa adhabu inayostahiki hadd au jinayaat, basi huadhibiwa kwa adhabu maalum na hahukumiwi na aina yoyote ya ta'zeer. Lakini, ikiwa Qur'an na Sunnah haikubainisha waziwazi kwa kutaja adhabu kwa kitendo cha uhalifu, basi makosa hayo huadhibiwa kwa ta'zeer. Hivyo basi, ta'zeer ni adhabu kwa madhambi ambayo hakuna hadd au kafara yoyote. Kwa mfano, Shari'ah imeweka adhabu maalum kwa madhara ya kimwili; kwa hivyo uhalifu aina hiyo hautapelekea katika hukumu ya ta'zeer.  Zaidi ya hayo, Qadhi (hakimu) atatekeleza hukumu ya ta'zeer kwa mujibu wa hali ya uhalifu uliotekelezwa kwa msingi wa ijtihad (kuelewa waqiah na kuvua hukumu ya kiShari'ah kutokana na ushahidi wa vyanzo vya kiShari'ah). Lakini, Qadhi au Khalifah hawezi kutabbani adhabu yoyote kwa matamanio yake kwa kuwa Shari'ah imekataza baadhi ya adhabu kama kuadhibu kwa kuchoma moto n.k. Lakini baadhi ya hudood au jinayaat zinaweza kutekelezwa kama ta'zeer. 

Ta'zeer ni tofauti na adhabu nyingine kwa sababu mtu anayehukumiwa na ta'zeer anaweza kusamehewa na Serikali au kifungo chake kikapunguza ilhali katika hudood au jinayaat hakuna msamaha kutoka kwa Serikali. Kwa sababu hudood au jinayaat zinapewa yule ambaye amekiuka haki ya Mwenyezi Mungu (swt) na wanadamu pia. Hivyo basi, uhalifu unaostahiki hudood au jinayaat unaadhibiwa bila mbadala. Lakini, uhalifu unaostahiki ta'zeer kama kumshutumu Khalifah amefanya makosa n.k Serikali inaweza kumpunguzia au hata kumsamehe muhalifu.

Hukumu ya ta'zeer inapatikana kupitia Qiyaas (mchakato wa kuvua hukumu ya kiShari'ah kwa kulinganisha) kwa mujibu wa hali ya uhalifu wenyewe. Khutuba kutoka kwa Mtungaji (swt) ameweka qareena (kielekezi) kuhusu ukubwa wa kitendo kibaya kwa mujibu wa adhabu inayotakiwa kuvuliwa.

Zaidi ya hayo, kutabbani na kutekeleza adhabu kama hizo zinatakiwa iwe kupitia kufahamu waqiah na kwa mujibu wa 'illah (sababu ya kiShari'ah) zinazohusiana na "kukinga (kutokana na haramu) kama alivyofunua Mwenyezi Mungu (swt), (وَلَكُمْ فِى ٱلْقِصَاصِ حَيَوٰةٌ) “Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi.” (TMQ 2:179). Mifano michache ya ta’zeer ni kama:

1. Lau mtu atajaribu kubaka lakini kwa sababu ya kuweko na kizuizi asifikie kiwango cha kufanya ngono inayostahiki hadd, ataadhibiwa kwa ta'zeer ya kutiwa jela miaka mitatu pamoja na kupunguziwa idadi ya bakora na kuhamishwa. Hii ni kwa sababu itakuwa amefanya kitendo cha haramu kinachostahiki hadd lau kusingekuwepo na kizuizi na kwa kuwa kitendo kibaya hakikufikia kiwango cha hadd, muhalifu huadhibiwa kwa ta'zeer.

2. Kuuza fasihi chafu, video, audio na huduma zote zinazohusiana na hizo zinaadhibiwa kwa kutiwa jela miezi sita.

3. Lau mtu atakunywa kilevya kisichokuwa pombe, mfano hash au madawa, basi ataadhibiwa kwa bakora na kutiwa jela miaka mitano pamoja na faini.

4. Lau mtu ambaye anajua kuwa mali ni ya uwizi na akainunua vivyo hivyo, basi ataadhibiwa kwa kufungwa jela kifungo kati ya miezi miwili au miaka miwili pamoja na jukumu la kumlipa aliyeibiwa.

5. Lau mtu atakuwa na nia ya kushiriki katika kuuendea kinyume umoja wa Serikali ya Kiislamu, kwa kupigia debe asbiy’yah (ukabila), basi ataadhibiwa kwa kutiwa jela kwa mujibu wa ukubwa wa uhalifu alioutenda kwa muda wa kati ya miaka mitano na miaka hamsini.

4. Mukhalafaat

Shari'ah umeweka adhabu za Mukhalafah ambazo huadhibiwa wale waliokiuka hukumu (maagizo) ya Imamu (Khalifah). Kwa sababu Shari'ah imemruhusu Khalifah kutabbani sheria katika masuala ya mubah, mfano sheria za barabarani ambazo zinaingia katika idara ya Serikali kwa mujibu wa mashauriano na wajuzi au baraza la Ummah, ni muhimu kuwa ukiukwaji wa sheria hizo uwekewe adhabu. Kama kukiuka sheria za kiidara ni uasi kwa Imamu. Mfano kuwaasi mu'awineen (wasaidizi wa Khalifah) ni kumuasi Khalifah kwa kuwa Khalifah ndiye aliyewaagiza watekeleze maagizo ya sheria za Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amefaradhisha kumtwii Khalifah, kama Yeye (swt) alivyoagiza:

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا أَطِيعُوا ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا ٱلرَّسُولَ وَأُولِى ٱلْأَمْرِ)

“Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi." (4:59), meaning listen and obey those who are granted authority by the Ummah.

Zaidi ya hayo, kumtwii Ameer ambaye amechaguliwa na Khalifah ni faradhi kwa Waislamu, kama alivyotufahamisha Rasulullah (saw),

»من أطاعني فقد أطاع الله، ومن يعصني فقد عصى الله، ومن يطع الأمير فقد أطاعني، ومن يعص الأمير فقد عصاني«

“Yeyote atakaye nifuata mimi, amemfuata Mwenyezi Mungu; na ambaye hatonifuata mimi, hamfuati Mwenyezi Mungu; na anaye mfuata Ameer (kiongozi), basi amenifuata mimi; na ambaye hamfuati Ameer, basi hanifuati mimi." (Bukhari / Muslim).

Lakini, kumfuata huko ni katika mema (ma'roof) pekee na sio katika maovu (munkar) kama alivyosema yeye (saw) «إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ» “Kufuata ni katika yaliyo mema pekee.” (Sahih al-Bukhari 7145).

Ni ushahidi tosha kuwa kujifunga na maagizo ya Imamu ni sharti kwa yeye kutekeleza sheria za Kiislamu na sio sheria za Kikafiri. Hivyo basi, kutofuata maagizo ya Khalifah ni kosa (kukiuka) linastahiki adhabu kwa mujibu wa hukumu ya Qadhi wa Serikali ya Kiislamu. Baadhi ya mafuqahaa' (wanasheria wa Kiislamu) wamejumuisha mfano wa adhabu hizo ni ta'zeer na sio kama kifungu tofauti. Lakini, katika kupangilia wakatofautisha ta'zeer na mukhalfaat kuwa ta'zeer ni adhabu zinazopewa wanao kiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) moja kwa moja na ilhali mukhalafaat ni adhabu zinazopewa wanao kiuka maagizo ya Khalifah.

Ni muhimu kufahamu kuwa maagizo yanayotolewa na Khalifah yanahusiana pekee na tabbani za ahkaam na sio utungaji wa ahkaam hizo kibinafsi kwa sababu ni haramu kwa Khalifah kutabbani chochote isipokuwa Shari'ah.

Ama kuhusu masuala ya mubah, mifano ya hatua za kiusalama wa bait ul-maal (Hazina ya Serikali), ujenzi wa miji na mipango ya jeshi n.k, haya huachiwa Khalifah kuamua kwa mujibu mashauriano. Hili limevuliwa kutokana na ufahamu wa hadith «أَنْتُمْ أَعْلَمُ بِأَمْرِ دُنْيَاكُمْ» “Munayo elimu bora zaidi (katika masuala ya kiufundi) katika dunia yenu.” (Sahih Muslim 6128).

Ina maanisha masuala ya mubah yanahitaji elimu na ujuzi wa mambo ya kidunia na hivyo kuweza kutegemea akili na tajriba ya mwanadamu kuhusiana na waqiah unavyosonga. Kwa mfano huo, Khalifah atatabbani sheria zitakazo tatua masuala yanayo ingia katika idara na aweza kufunga adhabu katika ukiukaji wa maagizo yake ya kiidara.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Sadiq Amin

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 11:03

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu