Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hofu ya Wamagharibi kwa Khilafah Inawasukuma Kutumia Nguvu zao ili Kuizuia

(Imetafsiriwa)

Waislamu wanajua kuwa Wamagharibi hawataki Uislamu uishi katika umbo lenye mamlaka ya utendaji. Wanajua pia kuwa dola zao za kikoloni na vyombo vyao vya habari, vya kijasusi na kisiasa vinafanya kazi muda wote kuzuia kurejea kwa Dola ya Khilafah. Wamagharibi wanafahamu sana maana ya kurejea kwake kuwa umbo lenye mamlaka ya kisiasa na uongozi wa kifikra wa kiulimwengu. Wanashughulika na fikra ya kurejea kwake kuwa ni uhalisia uliopo.

Mchunguzi yeyote hahitajii kupata shida ya kufuatilia kile kilichokwisha kutolewa na vyombo vya habari vya maadui juu ya kurejea kwa Dola ya Khilafah duniani kuchezea akili na kueneza uongo na hila danganyifu, kama makala, makongamano na semina za wanafikra wa Kimagharibi kuathiri nafasi za Waislamu kuelekea Dola ya Khilafah na kuwaweka mbali nayo kifikra na kisiasa, na kuwepesisha kila kitu kitakacholeta rai jumla dhidi ya fikra ya kurejea kwa Dola ya Khilafah kiulimwengu. Haya hayakufungika kwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na nchi za Magharibi tu, bali idara zao za kisiasa na kijasusi na zile zinazoitwa idara za usalama za taifa zinafanya kazi muda wote nje ya vyombo vya habari na katika hali ya usiri, kufuatilia na kuongea kila kitu kitakachozuia upatikanaji au ukaribiaji wa kurudi kwa Dola ya Khilafah. Harakati hizi zinajulikana kwa matokeo yake, ambayo yanaacha alama ya wazi na dalili, zinazoonyesha kwa uwazi muelekeo huu kwa wachunguzi makini na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa.

Kwa kuhakikisha hili, tutaonyesha baadhi ya mifano ya matendo ya kisiasa na vyombo vya habari kwa maslahi makuu ya Wamagharibi ya kikoloni na kikafiri katika vita vyao dhidi ya fikra ya Dola ya Khilafah, majaribio yao ya kuivua fikra hii kutoka katika uungaji mkono wa kiasili wa ummah, upandikizaji wake wa fikra ya kutowezekana kurejea Khilafah na uwezekano wa Waislamu kurejesha nafasi zao katika kuongoza mataifa kupitia dola ya Khilafah kama uongozi wa kifikra wa kisiasa wa dunia, ukosoaji wake wa thaqafa ya Hizb ut Tahrir, ilio mstari wa mbele na kiongozi katika mapambano ya kisiasa, chama imara kinachofanya kazi ya kuisimamisha Khilafah, katika ufahamu wake wa uelewa wa fikra yake, utambuzi wa taasisi zake, uoni ambao unafuata siasa za kimataifa, na kielelezo chake cha katiba na utayari wake wa kuongoza Dola ya Khilafah ijayo mwanzo tu wa kuja kwake, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu (swt), katika masuala yote yahusuyo sera za dola za ndani na nje.

Kwanza: Wakati Patrick Buchanan, mshauri wa awali wa Rais Nixon, Ford na Reagan, alipochapisha makala yake yenye anuani “Fikra Ambayo Muda Wake Umefika” mnamo 23/6/2006, hii haikuwa kuithibitisha fikra ya kurejea kwa Khilafah kutokea Morocco hadi Pakistan kuwa ilikuwa ni suala la wazi, bali ni kuonya dhidi ya kurejea kwake, kwa kusema: “Kama utawala wa Kiislamu ni fikra ilioenea miongoni mwa umma wa Kiislam, basi kwa vipi jeshi bora zaidi duniani litaizuia? Je hatuhitaji sera mpya?”

Akizungumza kwa kuzingatia umakini juu ya ukweli ulioshuhudiwa wakati huo, alizionya nchi za kikoloni za Kimagharibi kujitayarisha kwa hatari ya Dola ya Khilafah ijayo kabla ya kupitwa na muda. Alitathmini uhalisia na matarajio, ikiwemo yafuatayo:

“Fikra ambayo wengi ya wapinzani wetu wanaipigania ni ya kulazimisha. Wanaamini kuwa kuna Mungu Mmoja tu, Allah; na kuwa Muhammad ni Mtume wake; kwamba Uislamu, au kujisalimisha kwa Quran, ni njia pekee ya kwenda peponi; na kuwa jamii ya Kiwahyi itawaliwe kwa mujibu wa Shariah, sheria za Uislamu. Kwamba wamejaribu njia nyengine na kushindwa, sasa wanarejea nyumbani kwenye Uislamu”. 

Aliuliza kwa kuhoji:

“Fikra gani tunapaswa kuitoa? Wamarekani wanaamini kuwa uhuru unachukuana na heshima ya mwanaadamu, kuwa mfumo wa kidemokrasia tu na soko huru uwezao kuhakikisha maisha bora kwa wote, kama inavyofanyika Magharibi na inavyofanyika sasa Asia. Kutoka wakati wa Ataturk na kuendelea, mamilioni ya Waislamu wameshikamana na mbadala huu Umagharibi. Lakini hivi sasa, makumi ya mamilioni ya Waislamu wanaonekana kuukataa, wanarejea kwenye mizizi yao kwenye Uislamu safi zaidi. Kwa kweli, kubakia kwa imani ya Kiislamu ni suala la kushangaza.

Uislamu umehimili karne mbili za kushindwa na kudhalilishwa kwa Himaya ya Uthmaniya na kuvunjwa kwa Khilafah na Ataturk. Umevumilia vizazi vya utawala wa Wamagharibi. Umedumu kuliko falme za zamani za Wamagharibi nchini Misri, Iraq, Libya, Ethiopia na Iran. Uislamu umejikinga kiurahisi na Ukomunisti, umeendelea kusalia baada ya kushindwa kipindi cha utawala wa Nassir mnamo 1967, na umekuwa mvumilivu zaidi ya utaifa wa Yassir Arafat au Saddam. Hivi sasa, unakinzana na dola kuu ya mwisho ya dunia.” Huenda kilio cha onyo kilichofanywa na makumi ya mihimili ya vituo vya fikra za Kimagharibi akiwemo Buchanan, kwa niaba ya Mmagharibi mkoloni, kwa hitajio lake la sera mpya kuzuia fikra ya utawala wa Kiislamu na Khilafah, ambayo imekuwa imara miongoni mwa umma wa Kiislamu, ndio kile kilichozaa ujanja mpya wa kisiasa na mipango ya muda mrefu katika jaribio la kuzing’oa fikra na kutia wasiwasi fikra ya Khilafah katika nyoyo za Waislamu, kuwahofisha juu ya kuilingania kwa kuielezea kuwa ni kurudi nyuma, ukatili na ugaidi.

Miongoni mwa sera hizi za kiujanja ni kuiepuka kwake kwa kuingiza kile kiitwacho maadili ya kidemokrasia moja kwa moja, ambapo inaonyesha kufeli kwake kwa uwazi na kutoridhika kwa Waislamu kwayo, wakati wa uvamizi wa Afghanistan na Iraq. Wamewapatia kazi hii katika Waislamu kama wanazuoni wa watawala, taasisi za Kiislamu na baadhi ya vyama vya Kiislamu, na kuwapatia majukwaa masekula na wanaliberali na kuendeleza ukandamizaji na kunyamazishwa na watawala vibaraka. Wanajaribu kuishambulia fikra ya kurejea Dola ya Khilafah kwa kusema kuwa ni ndoto, na haiwezekani kupatikana kipindi hichi, kuiweka mbali kutokana na ubainisho wa Shariah na ulazima wake ambao wanazuoni kwa pamoja wamekubaliana juu yake. Wanadai kuwa Uislamu haukufanya kuwa ni wajibu, bali ilijuzu wakati fulani lakini sio leo, na kuwa aina ya serikali katika Uislamu haihitaji Dola ya Khilafah. Wengi walio katika vyama vya Kiislamu vilivyoshika mamlaka au kushiriki katika utawala wa kisekula wameachana na fikra ya kutekeleza Shariah katika Dola ya Khilafah ili kuzififilisha na kuziweka mbali kutokana na jambo la Waislamu la kuwa ni wajibu.

Ama kwa kafiri laghai, mkoloni wa Kimagharibi, ameikunjua mikono yake kwa siri na kuwapatia silaha watetezi wa utumiaji nguvu katika makundi ya Kiislamu, ambayo yamekuja kuhusishwa na matukio ya mauwaji na kukata watu vichwa, alama inayotolewa na vyombo vya habari kwa wale waliodai usimamishaji wa Khilafah wakati hawakuisimamisha. Hata hivyo Wamagharibi wamenufaika kutokana na kulihusisha jina la Khilafah na makundi haya, ambapo imepelekea kupotosha sura yake kwa watu na kwa baadhi ya Waislamu katika mipango yao michafu, ambapo kumeongeza ugumu wa kazi ya chama chenye uaminifu kinachofanya kazi kwa ajili ya kuirejesha na ambayo jina lake linahusishwa nacho, kuwa Hizb ut Tahrir ni Khilafah na Khilafah ni Hizb ut Tahrir, lakini vyombo vya kikoloni vya Kimagharibi na mashini zao za kielektroniki za utafutaji vinaunganisha jina la Khilafah na Dola ya Kiislamu na ISIS na sura nyengine potofu katika jaribio ovu kuficha usafi wake, nguvu, na wajibu katika Uislamu, na kukificha chama ambacho kinaifanyia kazi.

Pili: Kituo cha Masomo ya Kimkakati cha Marine Analytics cha Virginia, Amerika, kwa ushirikiano na Kituo cha Wilton Park cha Uingereza cha Afisi ya Mambo ya Nje nchini Uingereza, ambacho kinatumika kama jukwaa la dunia kwa mijadala ya kimkakati, kilifanya kongamano katika makao yake makuu Uingereza mnamo 3/5/2007 kwa muda wa siku 3, lenye anuani, The Struggle for Unity and Authority in Islam: Reviving the Caliphate?’

Kila kituo kati ya hivyo viwili kilitoa ripoti ambayo ilijumuisha nukta 81 zilizozunguka kwenye nukta kuu iliyozungumzwa, ambazo zilizunguka kwenye: Umoja na Utawala katika Zama za Makhalifah Waongofu, Khilafah na Mamlaka katika Mfumo wa Kisiasa wa Kiislamu baina ya Nadharia na Matendo, Kuhuisha Wito wa Khilafah katika Karne ya Ishirini, Vizuizi kwenye Umoja katika Umma wa Kiislamu, Uoni wa Kikanda juu ya Khilafah, Maelezo Jumla ya Makundi Yanayokuza Fikra ya Khilafah, Fikra Kupitia Utekelezaji na Kigezo cha Hizb ut Tahrir, Da’wah, Vyombo vya Habari na Ujumbe, na mwishowe ni juu ya Mitazamo Mengine ya Kiislamu.

Kongamano hili liliamua mwanzoni kabisa kuwa vyama vinavyolingania Khilafah ni vya siasa kali.

Zifuatazo ni nukta muhimu juu ya ripoti:

- Kongamano hili liliwaleta pamoja wataalamu, wasomi, weledi, na viongozi katika jamii za Waislamu kujadili umoja na mamlaka katika ulimwengu wa Kiislamu hivi leo. Ilikuwa ni mahsusi kwamba, washiriki walizingatia masuala haya ndani ya muktadha wa “mjadala wa sasa wa khilafah” – mjadala unaoendelea miongoni mwa baadhi ya wanachama wa jamii ya Waislamu juu ya usimamishaji wa khilafah mpya ya sasa.

- Inaonekana kuwa ni idadi ndogo tu, na zaidi wenye msimamo mkali, walio wachache ni wenye kukuza khilafah kuwa ni taasisi ya kuweza kuwepo kwa karne ya 21. Katika kuleta maono kutoka kote katika ulimwengu wa Kiislamu – kutokea Afrika na Mashariki ya Kati hadi Indonesia – kuyaleta mezani, tumeweza kuyaweka maono ya wenye msimamo mkali ndani ya taswira pana ya fikra za Kiislamu juu ya masuala haya.

- Hata hivyo, tunapozingatia taasisi ya khilafah hii leo, hali iliopita lazima izingatiwe kwa sababu hakuna nyanja ya imani ya Kiislamu inayoweza kufahamika sawa sawa bila kuzingatia historia.

- Mapambano ya leo kwa ajili ya umoja na mamlaka katika Uislamu yamefika kikomo, kwa kiasi fulani, katika mjadala mpya wa leo

- Hata vikundi vipya vya sasa vinavyotetea mpango wa khilafah

- Hasa Hizb ut Tahrir – vinaelekea havichunguzi dhana zinazojitokeza katika uoni wao. Baadhi ya dhana hizi ni masuala ya usasa, mfumo wa ki-nchi ambao upo hivi sasa.

- Kuhangaikia umoja na mamlaka ni mpambano unaopambanulika katika historia ya ukuaji wa dola au taifa lolote. Tokea kufariki kwa Mtume, masuala mawili msingi yahusuyo siasa za kidini kwa Waislamu yamekuwepo: Nani anayesimama nafasi ya Mtume baada ya kifo chake? Mamlaka gani mtu huyu awe nayo?

Majibu hayajatolewa na Quran au kuachwa na Mtume. Matokeo yake, nadharia tupu ya mfumo wa kisiasa katika Uislamu ulioibuka umetoa si zaidi ya usomaji wa kiufuasi wa historia ya mwanzo ya Kiislamu, yenye kuakisi tafsiri zilizotafautiana za matukio mbali mbali ya wakati.

Hakuna upekee, mfumo ulioelezewa, unaotoa maagizo ya hatua kwa hatua kwa ajili ya utawala katika Uislamu.

Historia haitojirejea: Haiwezekani kuurejesha mfumo ulioishi kwa miongo michache tu karne 15 zilizopita. Waislamu wachache tu ndio wenye kutaka kivitendo kurejea kwa mfumo wa kale, wa kabla ya mfumo wa sasa wa kisiasa ambao umepatikana karne ya 7.

Kuna vizuizi msingi kwa umoja wa Waislamu wa kiulimwengu, au khilafah mpya ya kisasa. Vingi ya vikwazo hivi vimesimama kutoka mfumo wa dola za kitaifa.

Ni vigumu kufikiria namna mtu atavyofanikiwa kutekeleza aina hii ya mfumo katika mfumo mpya wa kisasa wa dola za kitaifa uliojitanua, ulioundwa kwa maelfu ya makundi, makabila, madhehebu, nk. Umoja wa Waislamu haujadumu kwa muda mrefu sana, kama uliwahi kuwepo.

Hata kama Waislamu wamekubaliana juu ya haja ya khalifah au kiongozi rasmi wa umma, kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mivutano juu ya masuala ya kiutendaji kama wapi khalifah atakuwepo, wapi “mji mkuu” utakuwa, aina ya mfuatano wa makhalifa utakuwaje, na masafa ya mamlaka ya khalifah yatakuwa vipi.

-Hizb ut Tahrir huenda ni kundi ambalo linajulikana zaidi kwa utetezi wake hasa kutokana na harakati zake kwenye vyombo vya habari na kusikika kwake’

Kundi hili ni taasisi isiyonyambulika. Hivi leo Hizb ut Tahrir iko huru kwa kiasi fulani katika kila nchi. Hakuna chombo kilicho chini ya uongozi mmoja kinachoidhinisha harakati za kila tawi.

-Hizb ut Tahrir imeweka wazi uoni wa namna ya khilafah itakavyoundika kama ingetekelezwa. Kwa mujibu wa kundi, wanatamani kuwa na dola ya Kiislamu itayoongozwa na khalifa atayetekeleza Uislamu. Hatotawala kifalme bali ataongoza dola. Kuna nafasi nyengine tatu tu za utawala katika dola: wasaidizi (ambao wana nguvu sawa na khalifa, lakini kwa kuwakilishwa), na magavana wa wilaya na mikoa.

-Pia, khalifa atachukua hatua zifuatazo mara tu atakapotawazwa: ataifanya lugha ya Kiarabu kuwa lugha ya dola; atayachukulia mataifa yote ya Waislamu kuwa ni sehemu ya utawala wake moja kwa moja; atasimamisha mahusiano ya kidiplomasia na mataifa ya kikoloni na yale yasiyokuwa na mikataba nayo; kuweka mazingira ya kivita na mataifa adui; kujitoa kutoka taasisi zote za kimataifa zisizoegemea kwenye Uislamu (kama, UN, IMF); na kufanya ulinganizi wa Uislamu duniani kote.

- Intaneti imepanua mawanda ya kueneza wito wa Khilafah. Tovuti ya Hizb ut Tahrir, Khilafah.com pia ni ya kisasa, imekamilisha muundo wa taasisi za dola. Kuna msongamano mkubwa kwenye eneo hili, na mara nyingi huonekana katika vyombo vya habari.

- Makundi yanayotetea khilafah hivi leo yapo pembezoni; uoni wao sio wa walio wengi. Hata hivyo, Hizb ut Tahrir mara nyingi hufikiriwa kuwa haifanyi kazi vizuri na wanachama wa Al-Qaida huonekana kama wamepotoka.

Kinyume na masuala haya ya pembeni, hivi sasa kuna idadi ya viongozi wa Kiislamu wenye ushawishi ambao maoni yao kwenye siasa, uongozi, na mamlaka katika imani yanavuma kwenye pote la ulimwengu wa Waislamu.

Sio Quran wala Sunnah iliyotoa jina kwa aina ya serikali bali wanafikra wenye ushawishi wa Kiislamu wanaelezea kwa ufasaha misingi kwa ajili ya aina mpya za serikali za Kiislamu.

Wa mwanzo ni Rashid Ghannouchi; yeye anasema kuwa Waislamu washiriki katika serikali zisizo za Kiislamu, na wa pili ni Tariq Ramadhan; hoja yake imekwenda mbali zaidi ya Ghannouchi. Anadai kuwa “[Waislamu] wanahitaji kuigawa misingi ya Kiislamu kutoka kwenye tamaduni za asili na kuzitia katika utamaduni wa kweli wa Ulaya Magharibi.” Ni jambo la kuangaliwa hapa kuwa hakuna mwanachuoni yeyote katika hawa wanaokubali fikra ya kurejesha khilafah, wala hakuna mwanachuoni yeyote aliyeiwakilisha katika kongamano hili. 

Japokuwa kuna mjadala wa wazi juu ya umoja na mamlaka katika ulimwengu wa Kiislamu – katika uwanja mpana wa mitazamo na maoni – wengi ya watu hawajafikiria wazo la kuirejesha khilafah.

Bali, inaonekana ni makundi yenye msimamo mkali ndio wanaotetea urejeshwaji wa khilafah.

Hizb ut Tahrir, kwa upande mwengine, walinganizi wa kundi lisilotumia nguvu, likiwa ni msukumaji mkuu katika kuziondoa serikali zilizopo kusimamisha khilafah. Japokuwa wanaonekana kuwa na mpango ulio wa wazi juu ya namna ya kuitekeleza khilafah hii, kuna ushahidi mdogo wa kuwa wana maendeleo yoyote kwa hilo. Wengi wanafikiri kuwa wazo la kuirejesha khilafah ni chombo cha kutia madaha kinachotumika kuingiza, kupata huruma, kuhamasisha wafuasi, kuwakera maadui, na kupata uhalali. (Mwisho wa Ripoti)

Mchunguzi na mfuatiliaji hahitajii kutumia bidii kubwa ili kufahamu ujumbe wa kongamano hili kutokana na mijadala yake juu ya kile kiitwacho mpambano kwa ajili ya umoja na utawala katika Uislamu, hasa (Uhuishaji wa Dola ya Khilafah) ambao unajaribu kuongeza uaminifu kwa mapendekezo yake kupitia uwepo wa kundi la waitwao wataalamu, wanazuoni, wanaharakati na viongozi katika nchi za Kiislamu. Walichaguliwa kuakisi uoni unaouvua ulinganizi kwa ajili ya kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida. Ukweli ndani ya ripoti, kupitia wao, ni kupotosha na kuchafua na kujaribu kuvamia nchi za Kiislamu kifikra na kisiasa kuzitenga na uungaji mkono wa ummah kwenye fikra ya kuisimamisha Khilafah na kuifanyia kazi.

Umetoa hukumu kiholela bila msingi maalum na bila ushahidi kuwa makundi yanayolingania Khilafah kuwa ni wachache na haukujadili uhalali na nguvu ya fikra. Kwa hivyo, umeelezea makundi haya kuwa ni ya misimamo mikali, japokuwa yanaonyesha maoni yao, hasa maoni ya Hizb ut Tahrir, ambayo inasisitiza kuwa si yenye kutumia nguvu, ikimaanisha kuwa ni chama cha kisiasa cha Kiislamu chenye programu za wazi zilizofafanuliwa juu ya namna ya kusimamisha dola ya Khilafah na kina kielelezo cha katiba na programu za wazi juu ya kutekeleza Uislamu baada ya kusimamishwa, basi ni upi msimamo mkali unaoelezewa na ripoti yao hiyo?

Upotoshaji uliotajwa katika nukta za ripoti hii unaweza tu kuelezewa katika muktadha wa kazi yao isiyowachosha, kama taasisi za ushirikiano za uchunguzi wa kifikra baina ya Amerika na Uingereza zikiwa ni vichwa viwili vya ukafiri na ukoloni, wakijaribu kuweka vizingiti kwenye kile wanachokiona kuwa ni jambo lisiloepukika la kurejea kwa Dola ya Khilafah na utekelezaji wa Uislamu wenye maadili yake bora ya uwanaadamu ambayo yameshinda na kuzitenga fikra za kinyama, madili fisidifu ya kirasilimali na kisekula, kama ambavyo watu wanashuhudia hivi leo. Kushindwa kwao kisiasa kunaonekana ukubwa wake kwenye upeo wa kifikra; wanaendelea kudanganya, kughushi na kupotosha kwa miongo kadhaa. Kampeni hii huipa nguvu kila wanapogundua kudhihiri wazi kwa usimamishaji wa Khilafah, hutumia vyombo mbali mbali vya habari na njia za kisiasa na semina za kifikra pamoja na zana zao za kuikomesha; watawala vibaraka Waislamu, na wasomi wa Kiislamu kuwa ni njia za karibu kwa ajili ya mchafuko wa kifikra na kisiasa kuhusiana na mfumo wa serikali ya Kiislamu. Wamefikia hatua ya kuyatumia na kuyasukuma makundi yanayobeba harakati za utumiaji nguvu kama mauwaji na uhamisho chini ya jina la Khilafah kwa madaha, upotoshaji na mfarakano.

Wamagharibi hawakuwa wenye kufafanua zaidi kuhusu nia zao mbaya kwa Ummah wa Kiislamu na hasa dhidi ya kurejea kwa Dola ya Khilafah. Wakiwa ni wenye ufahamu na hofu juu ya kutoepukika kurejea kwake wakati wanapouliza, na kuonya, mwishoni mwa ripoti: “Je ufahamu wa ndani wa wito wa makundi ya siasa kali juu ya khilafah mpya unaweza kutumika kuwajuvya watungaji sera kuhusiana na kupambana na siasa kali na ugaidi?”

Tatu: Makala (Khilafah ya Kiislam au Dola ya Kitaifa?) ya tarehe 11/9/2020, kwenye tovuti ya Al-Hurra ya mwana habari Imran Salman, Mmarekani mwenye asili ya Bahrain, aliyefanya kazi za miradi mbali mbali na taasisi za uchunguzi za Amerika, ikiwemo Taasisi ya Ulinzi wa Demokrasia, ambapo alikuwa mhariri mkuu wa “Democracy Papers” juu ya Iraq.

Tunakuletea dondoo kutoka Makala hii, ambayo imejaa uadui, upotoshaji na chuki dhidi ya kazi ya kurejesha Dola ya Khilafah:

Khilafah ya Kiislamu ni ya zamani, kama himaya za kale, rikodi yake ya maisha imefikia mwisho, utamu na uchungu, na lazima ielezwe wazi katika mitaala ya shule kuwa haistahili kuwepo katika zama hizi mpya kwa kuwa inapingana na uhalisia wa nchi za sasa. Kuisomesha ni kuionyesha kihistoria tu, na haina chochote katika mustakbali wa watu hawa.

Kuna dhana nyengine isiyo sahihi, ambayo ni kuwa ili nchi za Kiarabu ziweze kuendelea; lazima ziungane. Nchi za Kiarabu hazihitaji kuungana ili zihuike. Kwanza, inahitajika kujenga dola za kitaifa za kisasa zinazoegemea dola za kiraia, utawala wa sheria, na kuhudumia maslahi ya watu wao.

Wito wa umoja unaotolewa kwa zaidi ya miaka mia moja iliopita haukuwa chochote zaidi ya kuwa ni fikra ya kihisia, ikiwa ni kivutio kwa wengi na kitamanisho cha dhana zao, lakini wamekosa utambuzi wa manufaa, na hivyo kuishia kuwa ni jaribio la kuiangusha chini fikra inayowazwa.

Ndoto ya kuwa na dola moja ya Kiarabu inaweza kuwa ni hitajio (ijapokuwa haina uhalisia) kwa wale wanaoamini katika uwezekano wa umoja huo, japokuwa historia ya sasa na ya zamani haijalitukuza hilo kwa namna yoyote. Ama kwa ndoto ya Khilafah ya Kiislamu, inakuwa ni balaa na jinamizi lenye kutatiza, na hatutaki yeyote kuiendea. Bila shaka, wito wa umoja wa Waarabu, licha ya kuwa ni jambo la kishamba na ni balaa, ni jambo lisilovumilika kwa wepesi kuliko suala la Khilafah ya Kiislamu. Khilafah imetupeleka miaka mingi nyuma katika wakati uliopita; zama za zamani za kufikirika, kila dhehebu la Kiislamu linaiwaza hata hivyo linaitaka au iko pamoja na hamu yake ya kisiasa, na makundi mengine yanaikataa na kuiona kuwa ni uovu usiofaa.

Kwa maana nyengine, tusiangalie tena juu ya Khilafah ya Kiislamu kama Wamagharibi hivi leo wanavyoangalia hadhara ya Wagiriki au Waroma… tunanufaika kutokana na mazuri yao kuhusiana na yetu ya leo, sio kuwa tunayaelekea, Mungu apishie mbali!

Ni wazi kutokana na makala hii ukubwa wa uadui wake kwa kurejea Khilafah kupitia upotofu wa kifikra na kisiasa, ambao upo wazi kupitia nafasi alizochukua na alizoajiriwa kwazo na taasisi za kidemokrasia za Kimagharibi.

Nne: Ama picha ya nne kuhusu kuangazia juu ya Khilafah, ni kutoka kwenye kitabu “Madhehebu na Harakati za Kiislamu” kilichotoka 2021, sura ya kumi na saba ya kitabu inazungumzia kuhusu: “Hizb ut Tahrir: Ndoto ya Khilafah” imeandikwa na Mkazakhstan, Miriam Aitkulova. Katika kitabu hichi, Hizb ut Tahrir imewekwa katika sehemu ya tatu chini ya anuani “Waumini Wakereketwa na wenye Siasa Kali” na kwa mujibu wa madai ya kitabu, kinaelezea wenye siasa kali ni wale wanaotumia vurugu kufikia malengo yao. Hata hivyo, imewakusanya Hizb ut Tahrir chini ya kifungu hichi ili kuiweka katika kivuta macho cha mapambano ya wenye msimamo mkali, kwa uwongo na kukashifu. Inakieleza chama kuwa ni cha kisiasa na kisichotumia nguvu.

Tunaangaza mawazo muhimu zaidi yaliyojengwa ndani yake:  

Dhidi ya kuongezeka kwa zahama katika nchi zenye Waislamu wengi, mchakato wa kujiondoa kwenye ukoloni na mapambano ya ndani baina ya mataifa ya Kiarabu, kuibuka kwa harakati ya Kiislamu kama Hizb ut Tahrir, ambayo inapambana na uoni wake juu ya haki, haikuwa ni jambo lisilotarajiwa; hata hivyo, katika dunia ambapo ushirikiano wa dini na siasa umekuwa ukikataliwa kwa kipindi, na kuonekana kuwa ni kuwa nyuma, fikra za harakati mpya zimekuwa zikidaiwa kuwa ni za chama cha kisiasa, lakini zinapigana kwa ukaidi kwa ajili ya Khilafah ya Kiislamu kwa njia ya Mtume Muhammad (saw) kwa uaminifu.

Ipo chini ya kivuta macho na kituo cha uangalizi maalum na idara za usalama na taasisi za kijamii na kisiasa katika Asia ya Kati, ambapo Hizb ut Tahrir imepata umaarufu mkubwa tokea kuvunjika kwa utawala wa Kisovieti. Hata hivyo, Hizb ut Tahrir imepata uangalifu mdogo wa kimataifa kuliko harakati nyengine za siasa kali za Kiislamu, na utafiti juu ya chama hichi mara nyingi ni wenye kuleta hali ya mbishano, unayumba baina ya kuwa “wenye msimamo mkali” au kundi la “amani”. Katika kuzingatia haya, sura hii inajaribu kutoa umaizi zaidi kwenye historia na fikra ya Hizb ut Tahrir na msimamo inayouchukua kuhusiana na suala la vurugu.

Hizb ut Tahrir imejipanga vyema na fikra yake imefafanuliwa kwa uwazi. Fikra hii inashajiisha kuufufua Ummah wa Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah, mfano wa ile ya zama za Mtume Muhammad (saw) na Makhalifah wake wanne wa mwanzo. Chama kinaangalia kasoro za harakati nyengine za Kiislamu katika kukosa programu imara za kisiasa na ushirikiano wao na ma-sekula, na inajitangaza yenyewe kuwa sio taasisi isiyo na doa, bali ni harakati ya kisiasa yenye msukumo wa Uislamu. Kwa hiyo, inapingana na mifumo mengine – ima iwe ukomunisti, urasilimali au mwengine wowote – ukiwa uko kinyume na Uislamu.

Kwa Hizb ut Tahrir, Uislamu ni fikra na njia (twariqa) na unajitegemea, ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) na hauwezi kupatana na mifumo ya wanaadamu. Kanuni msingi za Hizb ut Tahrir hazikubadilika tokea siku ilipoanzishwa licha ya mabadiliko yanayotokea ya uongozi na kubadilika hali katika dunia ya sasa, fikra za mwanzo za Nabhani kutokea kwenye kiini cha Hizb ut Tahrir, bado zinaendelea kuwavutia Waislamu wengi hivi leo. Jina la chama linaakisi lengo lake msingi la kuzikomboa nchi za Waislamu kutoka kwenye ushawishi wa tawala za kikafiri. Muhammad Iqbal na Zulkifl Zulkifl wanaizingatia Hizb ut Tahrir kuwa ni kundi lenye sifa zote za harakati yenye kutaka mabadilliko msingi, japokuwa mara nyingi inachanganywa na kundi la “magaidi” kimakosa.

Hivi leo, Hizb ut Tahrir inazingatiwa ni moja ya harakati kubwa kabisa ya Kiislamu duniani. Kutokea kuanzishwa kwake katika hali duni nchini Palestina, fikra za Hizb ut Tahrir zilienea kwa haraka katika nchi nyingi, shukrani kwa sehemu kubwa ya mikakati ya Nabhani iliyowashajiisha wafuasi wake kusafiri kwa umbali mkubwa, haiba yake na ukaribu mwema kwa Waislamu wote bila kujali makabila, jinsia au madhehebu waliokuwa nayo (Othman 2012: 90)

Hizb ut Tahrir kwa ushujaa inatawanya fikra zake kupitia vipeperushi, mihadhara na mikutano ya kawaida. Hivi leo, kitengo chake cha habari huenda ndicho kilichojipanga vyema zaidi na cha kisasa, kwa kulinganisha na vyombo vyengine vya habari vya harakati nyengine za Kiislamu. Wakati wa muongo wa kwanza wa harakati zake, Hizb ut Tahrir ilipata mafanikio si haba katika nyingi ya nchi za Kiarabu.

Hivi sasa ipo ima rasmi au kwa siri katika nchi zaidi ya arubaini. Moja ya sifa zake bainifu ni utumiaji bora wa uwezo katika nyanja za habari; zimefanikishwa katika njia za kisasa zaidi za mawasiliano, kupitia ubunifu wa uchapaji kitaalamu na brosha za taarifa, kurasa rasmi na zisizo rasmi za habari, na tovuti katika nchi ambazo Hizb ipo. Kwa mfano, kwa kipindi kirefu, afisi ya Hizb ut Tahrir katika Asia ya Kati imekuwa na kurasa kwenye mitandao ya kijamii, hadi ilipofungwa na taasisi za usalama. Hata hivyo, wepesi wa kupatikana mitandao ya kijamii imewawezesha kuendelea na harakati zao.

Kutokana na uoni wa Nabhani, Uislamu ni mfumo kamili na wenye fikra ilioshikana unaoweza kusimamia nyanja zote za maisha. Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Hizb ut Tahrir, lengo lake ni kurejesha maisha kamili ya Kiislamu na kueneza ulinganizi wa Kiislamu kote duniani. Lengo hili maana yake ni kuwarejesha Waislamu kuishi maisha ya Kiislamu katika Dar ul Islam (makao ya Uislamu) na katika jamii ya Kiislamu ili masuala yote ya maisha katika jamii yaweze kushughulikiwa.

Kwa mujibu wa hukmu za Shariah, na katika uoni wake juu ya Halali na Haram, chini ya dola ya Kiislamu, ambayo ni Dola ya Khilafah, nayo ni hali ambapo Waislamu humchagua Khalifah na kumpa bay’ah (kiapo cha utiifu) ya kumsikiza na kumtii, ilimradi anatawala kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume (saw), na kwamba Uislamu ulinganiwe kuwa ni ujumbe kwa walimwengu kupitia Da’wah na Jihad.

An-Nabhani ameandika kuhusu Dola ya Kiislamu kuwa “sio jambo la kubuniwa wala ndoto za madhania, kwa kuwa imeweza kutawala na kuathiri historia kwa zaidi ya karne kumi na tatu.” An-Nabhani alitabiri kuwa mwanzoni Khilafah itaweza kusimamishwa katika moja ya nchi za Kiarabu na hatimaye kuziiingiza nchi zote za Waislamu. Hata hivyo, fikra yake baadaye ilionekana kujenga ushawishi zaidi maeneo mengine.

An-Nabhani alichanganya Uislamu wa dhati na siasa za kisasa, iliopelekea kupatikana kielelezo cha katiba (1953) kwa ajili ya Khilafah ijayo iliyosheheni mkusanyiko wa sheria katika nidhamu za kisiasa, kiuchumi na kijamii za dola na sera yake ya kigeni. Kwa mujibu wa katiba, kiongozi wa dola, khalifah huchaguliwa; lazima awe muaminifu na mwenye kuwajibishwa.

Aitkulova pia ameandika uoni ulioelezewa na idadi kadhaa ya wataalamu wanaopambana na ugaidi ambapo harakati huweza kwa hatua ya mwanzo kuwa katika njia ya kuelekea kwenye msimamo mkali.

Ndio, Waislamu wana ndoto ya kuishi kwenye Khilafah, lakini hawaoti juu ya uwezekano wa kurejea kwake, kwa sababu kurejea kwake ni ahadi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume (saw) ametoa bishara njema. Taswira za dola ya uadilifu na huruma, utekelezaji wa hukmu za Kiislamu, na aina maalum ya maisha ambayo yanasifika na dola ya Khilafah, inapita kwenye macho yao kila siku, na kumuona Khalifah anayepewa bay’ah kwa kukubaliwa na kuchaguliwa na kumpatia utiifu wao kutawaliwa na sheria za Mwenyezi Mungu (swt), na wanaona mali zao za ummah zikigaiwa kwa usawa baina yao, na wanaona haki zao za kuishi zikilindwa kwa usimamizi bora zaidi unaowezekana, na wanaona namna wanavyoikimbilia jihad kuliondoa umbile la Kiyahudi, na kutoona balozi za Wamagharibi au ushawishi wao wa kikoloni katika ardhi zao, na wanakwenda kutoka ncha moja hadi nyengine katika nchi yao bila Hati ya kusafiria au mipaka, na umoja wao ni wenye kupatikana kivitendo katika dola unaohofiwa na mataifa, na kumuona Khalifah akihutubia mataifa na kubeba ujumbe wa Uislamu kwao kuwatoa katika kiza na kuwapeleka kwenye nuru na kutoka kwenye uonevu wa imani yao na maadili kwenda kwenye uadilifu na huruma ya Uislamu.

Kwa yote haya, maadui wa Uislamu wanafanya kazi ya kuchelewesha kurejea kwa Khilafah kupitia njia zote za kishetani. Wanafahamu uhakika wake sana na wanaipigia taswira kichwani kama watu wanaoifanyia kazi ya kusimama kwake wanavyoipigia taswira.

Je, Waislamu wanafahamu uwajibu wa kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha dola ya Khilafah na kutoa muhanga kwa chenye thamani kwa ajili yake? Inaegemea juu ya ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema za Mtume Wake (saw), hivyo yeye ni kutoka kwa walio washindi, Mwenyezi Mungu akipenda.

Enyi Ummah wa Kiislamu: Utekelezaji wa Uislamu ni wajibu juu yenu katika umbo la Kiislamu na dola kwa sababu Uislamu haupatikani isipokuwa katika umbo lenye mamlaka ambalo linatekeleza hukmu zake. Na aina ya serikali katika umbo hili ni Dola ya Kiislamu ya Khilafah, ambayo dalili zake kwa upana zinatolewa na Sunnah na Ijmaa ya Maswahaba, ikiwa ni wajibu wa utekelezaji wa Uislamu na hukmu zake zikitajwa katika Kitabu katika tamko lake Yeye (swt):

(فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجاً مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيماً)

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayotoa, na wanyenyekee kabisa.” [An-Nisaa: 65].

Kwa vipi kafiri mkoloni atambue umuhimu wa Khilafah na kutafiti na kuwachunguza wale wanaoifanyia kazi na kuwaelezea kuwa magaidi na wenye siasa kali na kuwapiga vita moja kwa moja na kwa kupitia zana zao na njama dhidi yao katika hatua zote, na wewe ukawa bado hujatambua kuwa hilo ni suala lako la kufa na kupona ambalo muda wake umefika? Na kuchukua hatua muhimu kuhusiana nayo, na kutowafanya makafiri kuwa na njia juu yetu au kututawala?! Usifanya kumbukumbu ya kuanguka kwake kujirudia tena mwaka ujao, bali ifanye iwepo, Mwenyezi Mungu ajaalie, mwaka wa kusimamishwa kwake, ili dunia itingishike chini ya miguu ya dhalimu kafiri, na kisha walimwengu wafurahie uadilifu wake uliongojewa kwa muda mrefu na huruma.

#أقيموا_الخلافة      #الخلافة_101

#ReturnTheKhilafah             #YenidenHilafet         #TurudisheniKhilafah

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Ahmad Hassouna

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu