Jumanne, 07 Rajab 1446 | 2025/01/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Enyi Waislamu, Zikingeni Familia zenu na Moto kwa Kutimiza Ahadi zenu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Kusimamisha Khilafah

(Imetafsiriwa)

(يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًۭا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَـٰٓئِكَةٌ غِلَاظٌۭ شِدَادٌۭ لَّا يَعْصُونَ ٱللَّهَ مَآ أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ)

“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi senu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.” [Surah At-Tahrim: 6]

Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha waja Wake kuzikinga familia zao kutokana na Moto kwa kujifunga juu ya yale Aliyotuamrisha kuyafanya na kwa kujiepusha kutokana na yale Aliyotukataza. Sisi tukiwa Waislamu, tumeweka ahadi kwa Mwenyezi Mungu (swt) kufanya kile kitakachotubakisha kuwa juu ya njia iliyo nyooka katika maisha haya na kuzilea familia zetu zishikamane na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa bahati mbaya, tokea kuangushwa kwa Khilafah mwaka 1924, hili limekuwa gumu zaidi kufanyika na kukaribia kutowezekana katika dunia ya baada ya 9/11 ambapo Waislamu na Uislamu, wamefanywa zaidi kuliko muda mwengine wowote kuwa maadui wa umma nambari 1.

Baada ya 9/11, Amerika na Magharibi ilitangaza “Vita dhidi ya Ugaidi”, ambapo imewawezesha kuweka sheria ‘dhidi ya ugaidi’ kwa msingi wa usalama. Kusikiliza habari kwa siri, upelelezi, na masuala ya mitego yamekuwa ni ada katika misikiti kote katika nchi za Magharibi, pamoja na uanzishwaji wa Upambanaji wa Siasa Kali (CVE) ambazo zimetumika kuwalenga vijana wa Kiislamu.

Wametumia vyombo vya habari na Hollywood kueneza msemo wa kuwa Waislamu wanachukia “uhuru” wa Wamagharibi, ni wenye asili ya vurugu, na kisirisiri wanapanga shambulizi jengine muda wowote. Propaganda imepata kasi haraka kwa kuwashawishi watu kuwa misingi ya Uislamu ya kiasili kama jihad, taasisi za ndoa, sheria za mirathi, usimamizi wa wanawake kwa mahram zao … nk. kuwa ni kuwa nyuma na ukandamizaji.

Na mara moja wakawaonyesha wanawake waliojivika maguo ya kufunika uso, au waliovaa hijab wakidhalilishwa na wakihitajia maadili ya Kimagharibi ya kudai haki za wanawake kuwakomboa kutokana na makucha ya Uislamu, Astaghfirullah! Nadharia ya usawa wa wanawake imekuwa na taathira yake iliyo na dhara juu ya Waislamu, ambapo wanaume na wanawake wamekuwa washindani baina yao katika nyanja zote za maisha, kinyume na kuwa washirika wanaofanya kazi pamoja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Imemtoa mama nje ya nyumba, ambapo yeye ni moyo wa nyumba, na kumpeleka kuwa nguvu kazi, sio kumletea usawa wake na heshima, bali kumfanya kuwa ni mzalishaji na mlaji wa manufaa ya kipote cha warasilimali.

Uingizwaji wa urasilimali na usekula kwa Waislamu Mashariki na Magharibi umetuhamasisha kuwa wenye kujali vitu na kuwa wabinafsi. Kulenga kwetu kumehama kutoka Akhera kuelekea starehe za kidunia za simu mpya, magari ya mwendo kasi, nyumba kubwa, likizo za gharama, na mitindo ya mavazi.

Hata kama mtu hamudu, ushawishi wa mikopo ya benki na kadi za mikopo zipo kuhudumia mahitaji hayo.

Mashambulizi ya kuendelea dhidi ya njia yetu ya maisha na kuingiziwa fikra za kinyume na Uislamu zimewapelekea Waislamu hasa wale wanaoishi nchi za Magharibi, kuwa wasio na kinga na wasio na mtetezi juu ya Dini yetu. Kwa kuwa kwetu Waamerika zaidi au Waingereza zaidi, kwa kupitikiwa tumeanza kujenga mazoea ya hofu kutokana na kuwa kwetu Waislamu ambayo imepandikizwa kwetu na serikali za Kimagharibi, vibaraka wao katika ardhi za Waislamu, na vyombo vya habari. Hatuhitaji tena uhakikisho wa Mwenyezi Mungu (swt), bali tunahitaji ule wa makafiri. Aina hii ya kufikiri na kuishi imekuwa na athari mbaya kwa Waislamu, hasa kwa vijana, ambao wamechanganyikiwa kuhusiana na utambulisho wao na uoni wao juu ya maisha kwamba utokee wapi.

Vipi tunaweza kuhifadhi familia zetu kutokana na moto wakati jamii tunazoishi nazo zinatufanya tuishi kana kwamba utambulisho wetu tukiwa Waislamu tunaoutekeleza Uislamu kuwa ni “wenye msimamo mkali”, lakini kama tukikubali maadili ya kigeni ya kisekula, kama LGBTQ+, zinaa, fikra ya usawa wa kijinsia, uhuru wa kuchagua, nk., ndio tunaruhusiwa kiti  mezani? Yote haya hatimaye yanatufanya tupoteze utambulisho wetu kama Waislamu moja kwa moja, na kuufanya Uislamu si zaidi ya mkusanyiko wa ibada za kiroho tulizo nazo kuliko kuwa kile ambacho Uislamu umekuja nacho, nao ni mfumo kamili wa sheria zinazopaswa kutekelezwa na kuwa ni rehema kwa wanadamu.

Hii ndio sababu ya kuwa kutekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) kuzikinga familia zetu kutokana na moto, tunahitaji kufanya kazi kutekeleza jukumu la Khilafah, ambapo itahakikisha kuwa Waislamu wanaishi katika jamii kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na Muumba wetu.

Sambamba na kuweza kutekeleza ahadi yetu kwa Mwenyezi Mungu (swt), tutaweza kupitia kutekeleza Sharia za Mwenyezi Mungu (swt), kuleta haki, kuwalinda wasio na hatia, na kuihifadhi Dini yetu katika maisha haya kwa matumaini ya kupata Pepo ya daraja ya juu zaidi Akhera.

Abu Huraira (ra) amepokea kwa Mtume (saw) kwamba amesema,

«إنَّما الإمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِن ورَائِهِ ويُتَّقَى به»

“Hakika si vyenginevyo, Imamu ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujikinga kwake.” [Muslim]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Sarah Mohammed – Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu