Ijumaa, 04 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ash-Sham ndio Nyumba ya Khilafah
(Imetafsiriwa)

Mara nyingi nilijiuliza kuhusu Hadith ya Mtume (saw):

«هَذَا الْأَمْرُ كَائِنٌ بِالْمَدِينَةِ ثُمَّ بِالشَّامِ ثُمَّ بِالْجَزِيرَةِ ثُمَّ بِالْعِرَاقِ ثُمَّ بِالْمَدِينَةِ ثُمَّ بِبَيْتِ الْمَقْدِسِ، فَإِذَا كَانَتْ بِبَيْتِ الْمَقْدِسِ فَثَمَّ عُقْرُ دَارِهَا، وَلَنْ يُخْرِجَهَا قَوْمٌ فَتَعُودُ إِلَيْهِمْ أَبَدًا»

“Jambo hili (Khilafah) litakuwa Madina, kisha Al-Sham, kisha Jazira, kisha Iraq, kisha Madina kisha Bait ul-Maqdis. Itakapokuwa iko Bait ul-Maqdis, makao yake yatakuwa huko, kamwe watu hawataweza kuiondoa humo, kwa hivyo itarudi kwao milele.” Yaani ndio sehemu ya mwisho ya Khilafah; Khilafah haitatoka humo baada ya hapo! Swali hapa ni: Ni ipi nafasi ya Bait ul Maqdis ukilinganisha na miji mikuu ya Waislamu kama vile Makka, Madina, Damascus, Cairo, Istanbul, na Baghdad, ambayo Imam al-Shafi'i aliwahi kumwambia mmoja wa wanafunzi wake, “Je, umeiona Baghdad?” Na akasema hapana. Akasema: “Basi hujaiona dunia na hujawaona watu!” Hii ndiyo miji iliyoshuhudia sehemu kubwa ya historia ya Khilafah ya Kiislamu na bila shaka ilikuwa miongoni mwa miji mikubwa duniani. Basi kwa nini Mtume (saw) alipuuza uhalisia wao na akataja Al-Quds na akamalizia Hadith yake tukufu huko?

Iwapo tuitarudia historia yetu tukufu na sheria za Shariah ya Mola wetu, Al Aziz Al A'lim (Mwenye nguvu na Mjuzi wa yote), tutakuta kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ameifanya Sunnah ya badali kuwa ni sheria ya kudumu isiyobadilika, isiyogeuka na isiyojipendekeza kwa mtu yeyote kwa gharama ya mwengine. Kwa hivyo, mwenye kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na akavumilia mitihani yake kwa moyo mpana na akatafuta malipo ya Mwenyezi Mungu katika yale anayodaiwa na kuyapata, ndiye anayestahiki zaidi kupata radhi za Mwenyezi Mungu na hatimaye kupata malipo yake hapa duniani kabla ya akhera.

Hivi ndivyo ilivyotokea kwa watu wa Ash-Sham na watu wa Palestina haswa. Tangu mhalifu Mustafa Kemal alipoivunja Khilafah Uthmani huko Istanbul, mlezi na mtetezi wa Waislamu, na kuifukuza familia ya Uthmani barani Ulaya ili kuonja udhalilifu, ukandamizaji, kunyimwa, umasikini na ufukara, watu wa Palestina wamekuwa wakipata kila aina ya vitisho na matatizo na hatua zote za dhulma, udikteta, ukandamizaji na kunyimwa, hata kutoka kwa wale walio karibu nao zaidi miongoni mwa ndugu zao Waislamu. Tangu siku za kwanza za vita vyao na adui yao, Waingereza, na Mayahudi nyuma yao, walilazimishwa kujitegemea wenyewe kwa zaidi ya miaka sabini ya unyonge, kwa kujizatiti kwa chochote walichoweza kuanzia kwa pesa, silaha, na watu, wakijitahidi kwa jina la Mwenyezi Mungu kuiregesha Masra (mahali pa I'sra) ya Mtume wao (saw).

Hapa hatuhujumu juhudi za baadhi ya Waislamu kutoka nje ya ardhi ya Palestina waliposimama pamoja na ndugu zao kutoka Palestina mara kadhaa ambapo waliwatesa Waingereza na Mayahudi kwenye mateso mabaya.

Lakini hapa tunazungumza juu ya wengi wa wale waliopigana na kuwa na subira miongoni mwa watu wa Palestina peke yao baada ya watawala vibaraka kuwafelisha ndugu zetu huko Palestina. Watawala hawa hawakuridhika na kuwaangusha tu na kuwakatia mahitaji, lakini pia walikula njama walipofanya kazi ya kuchomoa silaha mikononi mwa wanamapinduzi kwa kisingizio kwamba majeshi yamefika na kwamba wajibu wa kupigana na Mayahudi, kuiregesha ardhi, na kulinda heshima uko tu juu ya majeshi haya pekee. Wanamapinduzi waliwaamini na kusalimisha silaha zao! Baadaye wakaingia katika hatari ya kuhamishwa, maafa (Nakba), na vikwazo (Naksa) hadi waliponaswa katika chini ya asilimia 20 ya ardhi ambayo mababu zao waliishi.

Leo hii, baada ya miaka yote hii, watu wa Palestina, hususan Waislamu wanaodhulumiwa huko Gaza, wamekabiliwa na vita viovu zaidi, vya kutisha, vya kuchukiza na vya kinyama katika historia ya sasa na ya kale. Zaidi ya Waislamu milioni mbili wanaodhulumiwa, ambao wengi wao ni wanawake na watoto, wamezingirwa kwa zaidi ya miaka kumi na sita kutoka pande zote, ikiwa ni pamoja na Misri, na leo hii wamekabiliwa na ushenzi, chuki na upotovu wa Mayahudi wanaoungwa mkono na wahalifu wote, dola dhalimu za dunia, hasa Marekani na Ulaya, ambao huwapa silaha, pesa, na chakula chote wanachohitaji. Wanaunganishwa katika hili na nchi zenye mafungamano na Waislamu, zikiongozwa na Uturuki, ambayo haikupoteza juhudi zozote katika kuwapa Mayahudi bidhaa, huduma, mafuta na vitu vinavyotokana na hayo, katika mojawapo ya misimamo ya duni kabisa na ya kufedhehesha ambayo upande wenye mafungamano na Waislamu unaweza kuchukua!

Tusisahau hapa kushindwa kwa Umma wa watu bilioni mbili kuwanusuru ndugu zao, katika mandhari ya kushangaza na ya ajabu ambayo akili haingii! Mkweli, mwaminifu, alikuwa sahihi pale aliposema: «لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ» “...hawatadhurika na wale waliowatelekeza”. Kutelekezwa katika Hadith hii kunamaanisha Waislamu kuwa na uwezo na kudra yao ya kufanya jambo kisha wasifanye! Hili, naapa kwa Mwenyezi Mungu ni janga kubwa.

Haya yote yanatokea sio kukabiliana na dola inayoweza kuwa tishio kwa umbile geni, bali dhidi ya wanawake na watoto na baadhi ya wapiganaji kutoka makundi ya Mujahidina ya Izz al-Din al-Qassam na ndugu wengine waliojiunga chini bendera ya jihad yao.

Kundi hili la waumini wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Waislamu wengine wote wa Palestina wamewasilisha kwa ulimwengu mzima, wakiwemo Waislamu ambao wanasitasita kuwaunga mkono, mifano ya ajabu sana ya subira na mapigano, kutoa roho, pesa, na familia kama muhanga kwa ajili ya ardhi ya Al-I'sra wal Mi'raj (Safari ya Usiku na Kupaa). Hawakuwa bakhili, wala hawakuwa waoga, wala hawakukata tamaa, basi Mwenyezi Mungu akawaletea hofu mikononi mwao dhidi ya umbile la Mayahudi waoga. Walithibitisha kwa pande zote kwamba umbile hili ni simba marara wa karatasi asiyeweza kukabiliana na changamoto yoyote ya kweli uwanjani, na kwamba uhai wa umbile hili usingeweza kuendelea bila ushirikiano, ubaya, uovu na usaliti wa watawala wa Waislamu na makamanda wa askari wao, ambao wameuhadaa Umma kwa miongo kadhaa kwamba jeshi la Kiyahudi halishindiki, na kwamba Waislamu hawana uwezo wa kukabiliana nalo! Lakini uongo huu ulifichuliwa mbele ya macho ya ulimwengu wote, na kafiri Magharibi ililazimika kutoa kila kitu kilichohitajika na umbile hili, hata mamluki walifika kutoka ulimwenguni kote kusimama na kupigana na ndugu za nyani na nguruwe.

Mateso, matatizo, na vitisho vinavyowapata Waislamu ndivyo vinavyonoa akili na nyoyo zao na kuimarisha imani yao kwa Mwenyezi Mungu (swt), hivyo kuwapa subira, ili wasisubiri kheri na ushindi isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), baada ya watu kukata mafungamano yao na watu hawa wanaodhulumiwa, hata na ndugu zao Waislamu! Na huuo hapa ndio msingi, yaani, hakuna kuokoka, hakuna ushindi, hakuna kufaulu, hakuna heshima, na hakuna uwezo isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Al A'li Al Adhim (Aliye Juu, Mkuu), na Yeye Peke Yake Ndiye Al Aziz Al Jabbar na ndiye pekee anayeweza kusema kitu, “Kuwa,” na kikawa.

Kwa uwepo wa kundi la waumini kutoka kwa watu wa Palestina, Ash-Sham, na watu wa Gaza, kutoka kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir, ambao wanafanya bidii na kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kusimamisha dola kwa ajili ya Waislamu ambao kwayo waumini wanaheshimika na ndani yake hutabikishwa Shariah ya Mwenyezi Mungu na vichwa vya makafiri na wanafiki vinatupwa chini kwa ajili yake. Kwa imani ya watu hawa katika ahadi ya Mola wao Mlezi (swt) na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw) ambaye alisisitiza kusimamishwa kwa dola yake ya pili ya Khilafah kwa njia ya Utume, ardhi haitapata mahali adhimu au panapstahiki zaidi kuliko Bayt ul Maqdis kuwa ndio nyumba ya Khilafah ya pili Mwenyezi Mungu akipenda.

Kutokana na hayo hapo juu, tunaweza kusema kwamba kuwasili kwa Khilafah katika Bait ul Maqdis kuna dalili zaidi ya moja. Ya kwanza ni kwamba Bait ul Maqdis ni eneo la kihistoria, kisiasa na kijografia la ulimwengu wa kale. Ni kitovu cha dini zote na kitovu cha umakini wao. Yeyote anayeidhibiti atatawala ulimwengu wa zamani. Hii ina maana kwamba pale Khilafah itakaposimamishwa, basi Waislamu watatawala ulimwengu mzima licha ya Mayahudi na Wakristo kuwa dhidi yao. Pili ni malipo kwa watu wa Ash-Sham kwa yale yaliyowapata na maumivu, kuvunjika, subira na uvumilivu waliyopitia kwa miongo mingi, hivyo Mwenyezi Mungu (swt) atawafanya mabwana wa ulimwengu mzima, naapa kwa Mwenyezi Mungu (swt) wanastahili hili na wao ndio watu wake.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ]

Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa. [Aal-i-Imran: 200].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Radio na
Rayan Adil – Wilayah Iraq

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu