Jumamosi, 25 Rajab 1446 | 2025/01/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Enyi watu wa Nusra! Kama hamtatoa Nusra katika Kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume Hivi sasa, basi Lini Tena?!

Mwenyezi Mungu ameteremsha Dini tukufu ya Uislamu kwa mwanadamu bora zaidi, Mtume Muhammad (saw). Yeye (swt) amesimamishia utawala kwake (saw) juu ya ardhi. Yeye (swt) ameteremsha Quran kupitia Mtume (saw), kuhukumu baina ya watu, kuwa ni msingi wa katiba ya dola ya kisiasa. Mwenyezi Mungu (swt) ametayarisha mandhari za ndani, kieneo na kimataifa kwa kuzaliwa dola hii ya kisiasa ambayo ilisimamishwa bila ya matakwa ya dola yoyote ya kikafiri na watu wake.

Mwenyezi Mungu (swt) ametengeneza mazingira mazuri ya kusimamisha Dola ya Haki juu ya ardhi, katika Madina Al-Munawwara. Mwenyezi Mungu (swt) ametufahamisha aina ya mazingira ya wakati huo, ya mivutano baina ya milingoti miwili, Wafursi na Warumi.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

    (الم * غُلِبَتِ الرُّومُ * فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ * فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ ۚ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

“Alif Laam Miim. Warumi wameshindwa, katika nchi ilio karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndie Mwenye nguvu Mwenye kurehemu”. [TMQ 30:1-5].

Aya hizi tukufu ziliteremshwa kwa Mtume (saw), wakati alipokuwa Makkah Al-Mukarramah. Zinaeleza kuwa Roma ilishindwa katika ardhi ilio karibu, ardhi ilio karibu zaidi na Hijaz, ambayo ni ardhi ya ash-Sham, hasa Jerusalem. Ziliteremshwa baada ya Roma kushindwa mwanzoni nchini Misri, mwaka 621 Miladi, baadaye Mfalme wa Roma, Heraclius, alilijenga upya jeshi lake, mwaka 622 Miladi. Aya zilishuka wakati wa Hijrah ya Mtume na kabla ya Hijrah. Wafursi walikuwa washindi katika vita vyote dhidi ya Warumi na Warumi hawakuwa na matumaini yoyote ya ushindi. Vita vya Badri vilikuwa mwaka 624 Miladi na wakati huo huo, Roma ilipata ushindi dhidi ya Fursi, waliishikilia Azerbaijan na kulivunja hekalu la zamani zaidi la Majusi. Kama Wafursi walivyoibuka washindi mwaka 614 Hijri na kuishikilia Jerusalem, Warumi nao walikuwa washindi mwaka 624, wakashikilia mahala pa uzawa kwa Majusi na Hekalu lao la ibada ya moto. Hii imesadifu na furaha ya Waislamu katika ushindi wao dhidi ya Washirikina katika Badri. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ

“Na siku hiyo waumini watafurahi, kwa nusura ya Mwenyezi Mungu”

Na vita vya wazi baina ya Wafursi na Warumi vilitokea mwishoni mwa 627 katika Nineveh, ambapo Warumi walishinda katika vita muhimu zaidi. Miezi minne baadaye, Mkataba wa Al-Hudaibiyah ulifanyika mwaka 628. Wafursi walitia saini mkataba wa amani na Warumi, baada ya mtoto wa Khosrow wa II Sheroe (Kavid II) aliyekuwa amefungwa, kumfunga na kumuua Khosrow wa II. Hivyo, wakati mataifa haya makuu mawili yakishindana, huku ikiwa mizani ya nguvu ikihama kutoka kwa Wafursi kuelekea kwa Warumi, Waislamu walikuwa wakisimamisha dola yao. Wakati milingoti miwili hii yenye kubeba mandhari ya kimataifa ikishughulishwa na kupigania ushawishi wa maeneo tofauti tofauti ya dunia, Waislamu walikuwa wameshughulishwa na kuimarisha dola yao katika Bara Arabu.

Ama kwa upande wa mazingira ya kisiasa miongoni mwa mataifa ya Ulaya, yaliyo kaskazini mwa Ulaya na Magharibi, yalikuwa yamegubikwa katika giza nene, ujinga uliotopea na vita vya mauwaji baina ya Ukristo mpya ulioibuka na upagani uliotopea. Hakukuwa na Ujumbe katika dini, wala muwekaji wa uzani katika siasa. H.G. Wells amesema katika kitabu chake, 'A Short History of the World', “Hakukuwa na alama ya utaratibu au umoja katika Ulaya ya Magharibi, na Himaya za Byzantini na Fursi zikiegemea juu ya uharibifu.”  Robert Briffault amesema katika kitabu chake, 'The Making of Humanity', “Kwa udanganyifu wa macho mwangaza unaoangaza kabla na baada unaelekea kupungua juu ya pengo la giza. Kutoka karne ya tano hadi ya kumi Ulaya ilizama ndani ya usiku wa kishenzi ambapo ulikuwa ni wa kiza na kiza zaidi. Ulikuwa ni ushenzi mbaya sana na wa kutisha zaidi ya ushenzi wa kale, kwani ulikuwa ni ushenzi muovu zaidi na wa kuchukiza kushinda unyama wa kale, ilikuwa ni mwili unaooza wa iliyokuwa hadhara kubwa. Maumbile na kivutio cha hadhara hiyo yalikuwa umefutwa kabisa. Ambapo maendeleo yake yalifikia kilele, nchini Italy na Gaul (Ufaransa ya sasa), yote yalikuwa ni maangamivu, uchafu, uharibifu.”

Ama kwa hali ya kisiasa katika Bara Hindi, India ilisambaratika kutokana na vita vya ndani na nje katika kipindi hicho. Hatimaye, haikuwa katika hali bora kuliko mataifa mengine na vita hivi vilileta idadi kubwa ya watumwa. Wahindi waliamini kuwa watumwa wameumbwa kutokana na Miguu ya Mungu. Waliamini kwamba walikuwa ni wenye ufahamu mdogo na wenye hadhi ya chini katika kuumbwa kwao na hivyo hawawezi kuinuliwa kutoka tabaka lao la chini, isipokuwa kwa kukumbana na dharau na shida, ili nafsi zao ziweze kufufuliwa na kuwa katika viumbe bora baada ya kufa!!

Kwa namna hii, laana ya kiroho iliongezewa juu ya laana ya hali mbaya walioishi nayo, iliowalazimisha kutosheka na kudharauliwa bila upinzani. Hivyo, kuamiliwa kwa watumwa India hakukuwa tofauti sana na hali ya kawaida ya wakati huo, kwa upande wa kuondolewa utu wa watumwa kabisa, kuwabebesha majukumu mazito, bila kuwapatia haki zozote badala yake!!

Ama kwa hali ya kisiasa katika Bara Arabu, yakiwemo makabila ya Kiarabu Makkah na maeneo yaliyoizunguka, dosari za kiroho zilikuwa kubwa miongoni mwa Waarabu kabla ya Uislamu. Makosa haya yalitokea kwa kiasi kikubwa wakati wa vita vya ndani vya kikabila ambavyo vilizuka kwa sababu zisizo na msingi, kama Vita vya Al-Basus vilivyotokea baina ya Bakr na Taghlib kwa sababu ya kujeruhiwa kwa ngamia na Vita vya Dahis na Ghabra baina ya Abs na Dhibyan. Vita vyote hivi viliendelea kwa zaidi ya miaka arubaini. Pia vita virefu vilitokea baina ya Aws na Khazraj, ambao walikuwa ndugu baina yao na mashuhuri zaidi katika hivyo ni vya Siku ya Buath, vilivyomalizika kwa ushindi wa Aws. Moja ya vita maarufu vya Waarabu vilikuwa ni Vita vya Fijar, vilivyopiganwa baina ya Maquraysh na Kinanah kwa upande mmoja na Qays na Aiylan kwa upande mwengine. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuwa kijana mdogo wakati huo na vita viliitwa Fijar, baada ya pande mbili, Kinanah na Qays, kutenda matendo yaliokatazwa.

Uzito wa vita baina ya Waarabu unaonyeshwa na Ibn Atheer aliyevitaja vita vya Waarabu katika Masiku ya Ujinga kwa kusema, “Tunakumbuka siku maarufu na kutaja hali zilizojumuisha mikusanyiko mingi na vita vikali. Sikuepuka kutaja mashambulizi yaliochochewa na sababu zisizo na msingi, kwa sababu yalikuwa mengi, yaliovuka mipaka.” Walikuwa wamefungika zaidi kwenye vita na mapigano, ambayo yalichipuka miongoni mwao. Mshairi wao Amr ibn Kulthum ameandika shairi, likielezea muelekeo mgumu na fikra za kijinga:

أَلاَ لاَ يَجْهَلَنْ أَحَدٌ عَلَيْنَا *** فَنَجْهَلَ فَوْقَ جَهْلِ الْجَاهِلِينَ

“Bila shaka, hakuna alie mjinga zaidi yetu. Na tulikuwa wajinga zaidi ya ujinga wa wajinga.”

Hii ilikuwa ndio hali ya mazingira jumla yaliokuwa wakati wa Utume na uwezeshaji wake. Kulikuwa na mivutano na mapigano miongoni mwa milingoti miwili ya medani ya kimataifa, mashindano katika Ulaya pamoja na ujinga na mapigano katika Bara Arabu na Bara Hindi. Hadhara tukufu ya Kiislamu uliibuka katika wakati na mahala muwafaka, huku mataifa makubwa ya kiulimwengu na kieneo yakiwa yameshughulishwa na vita. Mwanya wa hadhara ulikuwa ni kubwa sana, huku wanaadamu wakiwa wenye kuhitajia zaidi mfumo ili kuwavua kutoka katika hali mbaya, ambapo watu waovu walitawala.

Majaaliwa haya ni katika matayarisho ya Mwenyezi Mungu (swt), Mjuzi Zaidi na Mwenye Hikma na hayakutokea haya kwa bahati nasibu. Kwa hivyo kusimamishwa kwa Dola ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) haikuwa ni miujiza, nje ya kanuni za kidunia ambazo hulazimishwa kwa wanaadamu. Badala yake, ilisimamishwa kimaumbile, ikiwiana na kanuni za mabadiliko ya jamii na usimamishaji wa dola na sio miujiza ya ki-Uungu.

Kwa kuangalia mandhari za sasa juu ya viwango tofauti, vya kimataifa, vya kimahali, kieneo na kihadhara, mtu anaweza kuona ufananaji mkubwa unaofikia kiwango cha kulingana, baina ya mandhari ambazo Mtume (saw) alisimamisha Dola ya Kiislamu na mandhari ambazo leo tunaishi ndani yake. Ni ishara kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ameirudia tena historia, ili watu wenye akili miongoni mwa Ummah wa Kiislamu kuitumia fursa hii kwa kureiregelea Sera ya Mtume (saw). Hii ni kwa sababu ili wasimamishe dola, ambayo Mtume (saw) ametoa bishara njema ya kusimama kwake, kama ambavyo yeye (saw) aliisimamisha kwa mara ya kwanza. Mandhari mbili hizi ni zinafanana na hivyo basi na waisimamishe Khilafah Rashidah ya Pili kwa Njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ametueleza katika hadith, iliopokewa na Hudhayfa (ra), ambapo Mtume (saw) amesema,

   «تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا عَاضًّا فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“Kutakuwa na Utume kwenu kwa muda atakao Mwenyezi Mungu uwe, kisha atauondosha atapotaka kuuondosha, kisha kutakuwa na Khilafah kwa Njia ya Utume na itakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka iwepo, kisha ataiondosha anapotaka kuiondosha kisha kutakuwa na ufalme wenye kuuma kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka uwepo, kisha atauondosha muda anaotaka kuuondosha, kisha kutakuwepo na utawala wa kimabavu kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka uwepo, kisha atauondosha wakati anaotaka kuuondosha, kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume” kisha akanyamaza” (Ahmad)

Ni jambo lililo wazi kwa mtu mwenye kutafakari kuwa mivutano baina ya mataifa yenye nguvu, Amerika kwa upande mmoja na China kwa upande mwengine, umezichosha zote kiuchumi na kijeshi, huku zikishughulishwa kisiasa na kiutamaduni. Hali hiyo pia inapatikana katika vita baridi vinavyoendelea baina ya Amerika na Ulaya, pamoja na baina ya Ulaya na Urusi. Zaidi ya hayo, tusishindwe kuzingatia kuwa mandhari za ndani ya Amerika na Ulaya ni za mgawanyiko wa kiutamaduni. Hivyo, usekula, demokrasia na msingi wa haki za binaadamu yamechuliwa, kuwa ni yenye kuwatwisha mzigo watu, yamewaingiza kwenye umasikini na kuwagawanya kikabila, kijamii na kiitikadi. Maradhi yote ya kijamii na kibinaadamu kama ukabila, utaifa, uzalendo na ubinafsi, miongoni mwa mengine yako wazi. Hivyo, kuna mwanya mkubwa wa kihadhara, unaosubiria hadhara yoyote nyengine kuujaza.

Ama kwa upande wa mandhari ya kisiasa katika mataifa ya Mashariki ya Kati, yakiwemo mataifa ya Kiarabu, hali yao sio tofauti na ile ya dola za Ghassanid na Lakhmid (al-Manādhirah au Banu Lakhm) zilizokuwepo Mashariki ya Kati, wakati wa mzozo baina ya Wafursi na Warumi. Mmoja wao alikuwa ni wakala mtiifu kwa Wafursi, na mwengine kwa Warumi. Hali hii ni sawa na dola ovu za sasa katika ulimwengu wa Kiarabu na Mashariki ya Kati yote, ambapo baadhi ni tiifu kwa Ulaya, ikiongozwa na kichwa cha nyoka, Uingereza, na mengine ni wakala watiifu wa n’gombe mkali, Amerika. Mvutano wa sasa baina ya Amerika na China ambao umepelekea mvutano baina ya China na India ni ishara kubwa mno ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa watu wenye kumiliki nguvu na mamlaka katika ulimwengu wa Kiislamu, hasa wale walioko nchini Pakistan na Bangladesh.

Mwenyezi Mungu (swt) amezirejesha zama za nyuma, kwenye nyakati za mapambazuko ya Uislamu. Yeye (swt) ametengeneza mazingira mwanana kwa usimamishwaji wa Khilafah Rashidah ya Pili kwa Njia ya Utume, kwa namna ile ile Yeye (saw) alipounda mandhari kwa mara ya kwanza, hakuna nguvu katika uso wa dunia inayoweza na katika mazingira ambayo itaweza kusimama dhidi ya Khilafah, itakayowakilisha takriban Waislamu bilioni mbili. Waislamu wana kheri, utajiri, uwezo na kujimakini ambayo hayapo katika taifa lolote lililo katika uso wa dunia.

Hata hivyo, uwezo wote huo unatumika katika kujenga dola hizi za kijambazi, za kigeni. Wakati dola ya Waislamu itakaposimashwa, uwezo huu kimaumbile utaondolewa kutoka kwazo na kurejea kwenye nyumba ya Waislamu, hivyo mataifa haya yatavunjika kimaumbile, kuanzia kindani. Endapo mandhari hizi hazitajumuisha fursa adhimu kwa watu wenye nguvu na mamlaka kutoa Nusrah kwa ajili ya Uislamu na kwa ajili ya kusimamisha Dola ya Kiislam juu ya ardhi hivi sasa, basi lini tena?!

Enyi Answar! Tuna hakika kuwa Mwenyezi Mungu (swt) ndiye aliye jaalia jambo hili kama apendavyo na Yeye ndiye anayeunda mandhari. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا

“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [TMQ 65:3]. Yeye (swt) amewatayarishieni mandhari kwenu kuweza kuitumia fursa kwayo. Itumieni fursa hii na wala msiipoteze, vyenginevyo Mwenyezi Mungu (swt) amekuonyeni kwa kusema,

وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ

“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [TMQ 47:38]. Tumeweka wazi kile kilicho bora kwenu na kwa Ummah hadi siku ya Hukumu. Yeyote ambaye ni miongoni mwa vijukuu vya Khalid (ra), Qa’qa’ ibn Amr (ra), Salah ud-Diin na Muhammad bin Qasim, lazima ashabihiane nao ili wahesabiwe kuwa hao ni babu zao. Yeyote ambaye ni miongoni mwa vijukuu vya Khadija bint Khuwaylid (ra), al-Khansaa (ra) na mama wa Muhammad Ali Johar, Bi Amma, kuna kina mama katika Ummah huu, wanaoweza kuzaa viongozi wakubwa kama wale waliokuwa kabla yao. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, toa Nusra kwa ajili ya Dini yako.

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Bilal Al-Muhajer – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 05 Agosti 2020 11:17

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu