- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kukubali Suluhisho la Dola Mbili kwa Suala la Palestina ni Jambo Kubwa Sana Linalodhuru Mno
Suala la Palestina limewachosha Wamagharibi katika jitihada zao za kuweka ‘suluhisho,’ tokea kuundwa kwa umbile la Kiyahudi katika Ardhi Tukufu ya Palestina. Wamagharibi hawakuweza kupandikiza umbile hili kimaumbile ndani ya umbo safi la Ummah wa Kiislamu, bila kupingwa. Hii ni licha ya urahisi wa kusawazisha mahusiano ya kawaida ambayo Wamagharibi wameyatengeneza baina ya umbile la Kiyahudi na watawala wa Waislamu, ambao wameyalazimisha juu ya shingo za Ummah na makafiri wakoloni, ima iwe ni hali ya watawala duni wa Imarati na Bahrain, au wengineo ambao wanafuatia baada ya Mkataba wa Abraham wa Septemba 15, 2020.
Hata hivyo, katika hali tofauti, Wamagharibi na watawala vibaraka hawakuweza kuleta usawazishaji wa mahusiano ya kawaida ndani ya Ummah wa Waislamu kwa ajili ya umbile la Kiyahudi. Wala hawatoweza kufanya hivyo. Zaidi ya hayo, kutoweza kwa Wamagharibi kupandikiza umbile la Kiyahudi ndani ya Ummah, kunathibitisha kipingamizi kisichoweza kushindwa. Mkwamo uko wazi kwa kila mtu anayechunguza vikundi vinavyojishughulisha na kutengeneza hali za kimataifa na kieneo, zinazohusu suala la Palestina. Kuna mkanganyiko wa wazi unaofikia kiwango cha kutapatapa. Unaofichua ombwe, lililotengenezwa kupitia kutoweza kuendelea kwenye njia zote mbili, iliopendekezwa na mapendekezo yaliokusudiwa kutatua masuala hayo.
Kutapatapa huku kwa kuchanganyikiwa kulihisiwa hata wakati wa miaka ya mwanzo ya utawala wa sasa wa Trump. Tokea mwanzoni, utawala wa Trump umeelezea hamu ya utatuzi kuunda suluhisho la ubunifu, ukiyaelezea kuwa ni fikra za nje ya makubaliano kutatua mzozo juu ya Palestina, kwa majivuno kuhusu “Mpango wa Karne.” Bado, yote haya baadaye, lengo la mkataba, achilia mbali utekelezaji halisi wa kivitendo, bado haujaonekana kupatikana. Masuala yamebaki yamesimama kama yalivyosimama wakati wa nyuma wa utawala wa Obama. Ikichukuliwa kwamba mkwamo ulikuwa pia kwa sehemu unatokana na mazingira yanayozunguka, kama kukosekana kwa kipaumbele cha utawala wa Amerika na msimamo wa Netanyahu.
Hata hivyo, kukosekana kwa mshikamano na uwazi ni dhahiri, kutokana na mgawanyiko wa waziwazi katika jukwaa la kisiasa katika Amerika kuhusiana na maelezo, taratibu na ratiba, za suluhisho lolote. Hivyo, utawala wa Trump umetangaza kwa shida suluhisho la dola mbili, kabla kulikuwa na kukiri kwa ukweli wa shaka juu ya msisitizo wa hilo, unaotokana na matokeo ya ahadi ndefu za fikra za nje ya makubaliano.
Kutapatapa kwa karibuni ni sawa na wakati wa kutangazwa kwa uanzishwaji wa umbile la Kiyahudi mwaka 1948. Kufikiria suluhisho katika wakati wa sasa ni tofauti kabisa na msimamo wa kisiasa uliochukuliwa na utawala wa Amerika katika miaka ya 1950, kama kufanya upya suluhisho la dola moja, badala ya suluhisho la dola mbili. Profesa Emeritus Muamerika mwenye asili ya Kiyahudi mtaalamu wa Sheria za Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Princeton, na aliyekuwa Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binaadamu kwa Wapalestina, Richard Falk wametangaza kuwa muundo wa Afrika Kusini wa kuzindua mapambano yaliokusudia kutoa haki za Wapalestina, ima iwe kwenye ardhi zao au katika “Israel,” ukienda sambamba na uwepo wa taasisi za kuishinikiza dunia dhidi ya Tel Aviv. Msimamo huu unashabihiana na ule wa Saeb Erekat, Katibu wa zamani wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina. Bwana Erekat alisema katikati ya mwezi Februari kuwa njia mbadala ya suluhisho la dola mbili ni kuwa na dola moja ya kidemokrasia itakayotoa haki sawa kwa raia wote, Wakristo, Waislamu na Mayahudi, huku akiongeza kuwa suluhisho la dola moja la mifumo miwili, linalokuzwa na umbile la Kiyahudi halikubaliwi. Hivyo, hali ya kisiasa juu ya suala la Palestina limezuka ambapo upinzani na kutapatapa kumeshuhudiwa miongoni mwa wahusika na watoaji maamuzi. Watekelezaji na vikundi husika wote wamekosa uoni wa dira yoyote au utambulisho.
Kinyume chake, Ummah wa Kiislamu umeshikilia msimamo unaozingatia kuwa Ardhi Tukufu ya Palestina moja kwa moja ni yake. Hakuna shaka yoyote hata kwa wasio na uelewa wa kisiasa kuwa suluhisho linalozingatia mipaka ya kabla ya 1967 kwa dola ya Palestina haliwezekani. Mataifa makuu ya ulimwengu hayawezi kudhamini suluhisho isipokuwa kwa kulitambua umbile la Kiyahudi ndani ya Palestina kwa kuingia katika maelewano ya kawaida na umbile hili, yanayosimamiwa na makubaliano ya kimataifa ambayo yanafungwa juu ya utambulisho unaoahidiwa wa Wapalestina na mataifa ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu. Hata hivyo, yote haya yanapingwa na Ummah moja kwa moja. Uhalalisho wa kisiasa na wa vyombo vya habari kuhusu kukubali na kuhalalisha mapendekezo ya wakoloni wa Kimagharibi ni usio na msingi. Suala la kuirahisisha siasa pia halitofanya kazi, ima iwe ni wito wa “kukataa utambulisho lakini kukubali dola” au wito kwa ajili ya “umuhimu wa kukubali Mayahudi sambamba na Mpango wa Amani ya Waarabu 2007.” Uhalalisho wote unaibuka kutoka kwa waandishi mahiri na au kauli fasaha za wanasiasa, kuanzisha kukubalika kwa makaazi ya kabla ya mipaka ya 1967, inayopelekea ghilba za kisiasa. Kauli zinazohusiana na kukubalika kwa suluhisho la dola mbili kuko nje ya mipaka ya majadiliano makini. Ni yenye kupinzana kabisa na misingi yote iliozinduliwa ya upinzani wa Wapalestina, wa mrengo wa Kiislamu na wa kisekula. Yanapingana na mikataba walioitangaza, pamoja na fungamano la itikadi la Ummah wa Kiislamu kwa Ardhi Tukufu ya Palestina na chuki yao kubwa kuelekea Mayahudi, wauwaji wa Mitume (as).
Majaribio kwa ajili ya kukubalika kwa suluhisho la dola mbili yamekuwa ni mafanikio yasio fanikiwa kusafisha muendelezo wa kiusaliti kuelekea ‘jamii ya kimataifa’ na usawazishaji wa mahusiano ya kawaida na umbile la Kiyahudi. Hata hivyo, majaribio haya ni ya lazima mbele ya watu, kama ni utendaji wa kimaonyesho kuuza mtazamo mpya wa kisiasa, wa ndani. Wanasiasa wa Kimagharibi wanafahamu fika juu ya umuhimu wa kauli hizi za ndani.
Kwa mfano, baada ya mikutano pamoja na viongozi wa Hamas, Cairo na Damascus, aliyekuwa raisi wa Amerika Jimmy Carter kwa kujiamini alidai mnamo April 21, 2008 kuwa Hamas itakubali mipaka ya 1967. Alitamka kuwa, “Kama Raisi Abbas atashinda katika kujadili hali ya mwisho ya makubaliano na “Israel,” Hamas itakubali maamuzi yatayofanywa na watu wa Palestina na matakwa yao kupitia kura ya maoni.” Hivyo, viongozi hawatokataa bila utata mtazamo huo, kwa kuwa vitendo vinatangulia maneno. Badala yake, hawashindwi kuwa na kauli kuhusu kukubali dola ya Palestina katika kila fursa inayomkinika.
Bila shaka, suluhisho la dola mbili na kutambuliwa dola kwa ajili ya Mayahudi, hata kama ilikuwa ni eneo linalohusisha Kijiji kidogo cha Tiyaha katika viunga vya mji wa Acre, achilia mbali sehemu kubwa ya ardhi ya Palestina, sio halali kisiasa na kwa mujibu wa kisheria kwa Ummah. sio halali hata kama ni jambo la mpito au la muda, kwa kuwa baadhi ya viongozi wananyanyua bango la Uislamu hivi sasa, kama PLO ilivyodai mwanzoni mwa kuzama kwake ndani ya dimbwi la “kuitambua,” wakati ikitangaza sera ya “chukua kisha omba.” Hukumu za Sheria zinatoa umiliki wa Ardhi Tukufu kwa Ummah wa Kiislamu pekee, zikiutaka Ummah kuelekea mara moja kuikomboa Ardhi Tukufu kwa kuliondoa umbile la Kiyahudi. Hukumu za Sheria zinawapatia umiliki wa Ardhi Tukufu ya Palestina kwa Ummah wa Kiislamu, zikionyesha kuwa ni Ardhi ya Kharaj. Hukumu za Sheria zinaishurutisha Jihad kwa kulishajiisha jeshi la Kiislamu kuwa ni njia pekee ya kuikomboa ardhi, na kuiokoa kutokana na uvamizi. Haki ya Mwenyezi Mungu, ilioifanya Ardhi Tukufu kuwa ni ya Ummah wa Kiislamu, haitoweza kurejeshwa isipokuwa kupitia hukumu za Kisheria. Palestina inaweza kukombolewa tu kwa kulishajiisha jeshi la Kiislamu ambalo linadhamira ya kutekeleza wajibu wa Sharia ambao unaliangukia juu ya mabega yake. Njia na zana zinazochukuliwa kutoka kwa Wamagharibi zikidai haki ndio milango ya kusimamisha umbile la Kiyahudi pekee, inaimarisha misingi yake kwa njia ya mikataba ya kimataifa.
Uvamizi wa Mayahudi unachukua uhalali wake kutokana na maazimio na sheria za jamii ya kimataifa, ambayo inaunda “haki” bandia kwa uvamizi wa Ardhi Tukufu. Uhalali huu ni kupitia; utambulisho, usawazishaji wa mahusiano ya kawaida, kutoa “haki” kwa ajili ya uvamizi ili kubakia katika Ardhi Tukufu, usuluhishi unaoegemea maazimio ya kimataifa juu ya suala la Palestina na wito kwa ajili ya ulinzi kutoka jamii ya kimataifa. Uhalali huu wote umesimamishwa juu ya usuluhishi wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (swt) na hivyo unakataliwa katika pande zote. Zaidi ya hayo, ni usuluhishi kutoka kwa wale ambao awali kwa hakika wametoa “haki” kwa umbile la Kiyahudi juu ya ardhi yetu. Usuluhishi huu utaibua maafa tu ya Hasira za Mwenyezi Mungu (swt), usaliti na kuitelekeza Ardhi Tukufu kwa wavamizi wa umbile la Kiyahudi. Je, inawezekana kupata haki za ardhi kutoka kwa mtu asiyemiliki ardhi, lakini badala yake akaitoa ardhi ambayo hawaimiliki kwa Mayahudi wageni wasio na ardhi?! Hivyo inaweza kufikiriwa kuwa mipango tu iliochorwa kwa ajili ya kulimakinisha umbile la Kiyahudi, iwe ni njia ya kuikomboa ardhi?! Hivyo watu wenye akili hutaka kugonga mlango wa wakoloni Wamagharbi au vyombo vya kikhabithi vya kimataifa, kama Baraza la Usalama, kupata haki zilizonyakuliwa?! Je, njia za mashetani zitatoa njia ya kurejesha haki za Kiungu?!
Suala hili ni hatari zaidi kuliko watawala, Ulamaa na vikundi vyote vya Palestina. Bila shaka, ni muhimu zaidi kuliko hasira za jamii ya kimataifa au kukubali kwake. Mwenendo wa watawala dhaifu, PLO, Utawala wa Palestina na vikundi vya kitaifa umeelekezwa kwenye suluhisho la dola mbili, kuwa ni mwanzo wa jitihada za kila jitihada. Hivyo, Imarati na Bahrain zimefanya usawazishaji wa mahusiano ya kawaida na umbile la Kiyahudi kupitia Mkataba wa Abraham. Hata hivyo, mwenendo wa kuelekea usawazishaji wa mahusiano ya kawaida na umbile la Kiyahudi unawachunga watu wa Palestina na Ummah wa Kiislamu kuelekea katika njia isiyoleta manufaa yoyote, ambayo inatoa uhalali kwa umbile la Kiyahudi na kulifanya mshirika asiyestahili katika Ardhi Tukufu. Kukemea tu juu ya makaazi katika Ukingo wa Magharibi pekee kunafanya kuachia nyingi ya Ardhi Tukufu ilionyakuliwa mwaka 1948. Takwa la kuanzisha dola chini ya mipaka ya mwaka1967 itaweza kuitambua haki ya umbo lililoporwa kuwepo juu ya ilichonyakuliwa kutokana na ardhi kabla na baada ya 1967, ambayo inajumuisha kuachana na Al-Quds Ash-Sharif na Al-Masjid Al-Aqsa. Kuwachunga watu kwenye maandamano ya amani yanayolingania Palestina kuwa ni suala la Wapalestina wenyewe, na sio suala la Ummah wa Kiislamu, kunapelekea wito wa kuirejesha haki iwe ni kulingana na maazimio ya kimataifa. Kunapelekea kuachana na haki za Ummah kuhamasisha majeshi kuikomboa Palestina moja kwa moja, kuirejesha ili iukumbatie Ummah. Kutengwa kwa chaguo la kijeshi, la kuomba Nusra kutoka kwa majeshi ya Ummah kuhamasisha ukombozi, kunafanya kuachana na ukombozi wa Ardhi Tukufu katika njia ambayo huhalalisha tu uwepo wa umbile la Kiyahudi na kuliimarisha.
Hivyo, ni muda sasa kwa wale walio waaminifu kuvunja ukimya na kudai tena, bali kuthibitisha, msingi wa kweli wa mahusiano na wavamizi, ambao ni hali ya vita vya kudumu hadi ukombozi kamili. Je, Maulamaa, viongozi, na vyama hamtovunja mchakato wa usawazishaji wa mahusiano ya kawaida kabla ya kukosekana muda wa kuokoka?! Hivyo watu hawa ndio wazikwe chini ya mchanga wa hila za Wamagharibi chini ya kauli mbiu ya “kuweka imani kwa viongozi” na kuwaheshimu Maulamaa,” wanaotoa matamko na fatwa kwa maslahi ya wale wanaotengeneza mahusiano ya kawaida na umbile la Kiyahudi; Mayahudi waliovunja mikataba na Mtume Muhammad (saw) na kuwaua Mitume wengine?!
Kwa mujibu wa Dini tukufu ya Uislamu, suluhisho pekee linalokubalika kwa suala la Palestina ni ukombozi wake kamili kutokana na uvamizi, ambao utapatikana tu kwa kuhamasisha majeshi ya Waislamu, ikiwemo jeshi lenye nguvu la Pakistan, kuisaidia Palestina na watu wake. Hakuna upenyo wa mazungumzo kuhusiana na hali nyenginezo, kama suluhisho za dola moja au dola mbili, kama wanavyojadili maadui wa Ummah au wale wasio na utambulisho na kukosa dira, kama watawala Waislamu wa Kiarabu na kisekula. Watawala hawa wa Waislamu wamejiengua kabisa kutokana na Ummah wao wa Kiislamu na hivi sasa wako kama mamluki wasio waaminifu ambao wanajiuza kwa bei yoyote, wakikubali suluhisho lolote kwa mrejesho wa kuhifadhiwa viti vyao vya utawala, uporaji na utajiri.
Uislamu umekwisha amua kuwa suala la Palestina ni suala la Uislamu, na sio suala lililojifunga kwa Wapalestina tu au makubaliano ya Waarabu. Ardhi yake iko kwa Ummah wa Kiislamu hadi Siku ya Hukumu. Kuikomboa Ardhi yote Takatifu ni wajibu juu ya vizazi vya Kiislamu wenye uwezo, wale wanajeshi wa Kiislamu. Ni haram kuiwacha hata inchi moja ya ardhi chini ya wavamizi, licha ya mazingira yoyote au idadi yoyote ya uhalali wa kidunia. Hakuna haja kwa Ummah hata ya kuzingatia maazimio ya makafiri waovu kwa ajili ya Ardhi Tukufu ya Palestina. Mwenyezi Mungu (swt) amesema
(أَفَمَن يَمْشِي مُكِبّاً عَلَى وَجْهِهِ أَهْدَى أَمَّن يَمْشِي سَوِيّاً عَلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ)
“Je, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawa sawa katika Njia Ilionyooka?” [TMQ 67:22]
Hakika, ahadi ya ukombozi ni yenye kushuka juu ya Palestina, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kupitia ukombozi kwa mikono ya majeshi ya Ummah, yatakayohamasishwa na Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ambayo kusimama kwake kuko karibu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,
(فَإِذَا جَاء وَعْدُ الآخِرَةِ لِيَسُوؤُواْ وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُواْ الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُواْ مَا عَلَوْاْ تَتْبِيراً)
“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza, na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.” [TMQ 17:7]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Pakistan