Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sheria ya Kuzuia Ufanyishwaji Kazi kwa Nguvu wa Uyghur:
Ukweli Nyuma ya Uamuzi wa Amerika

(Imetafsiriwa)

Kwa sasa, kitisho ambacho Waislamu wa Uyghur wanakabiliana nacho nchini China ni maarufu; mateso, utoaji mimba wa lazima kwa wanawake wa Uyghur, kutenganishwa kwa nguvu na kufanyishwa kazi kwa nguvu. Kuhusiana na kufanyishwa kazi kwa nguvu, Amerika imeanzisha msururu wa miswada ya sheria, wa karibuni zaidi umeitwa “sheria ya kuzuia Ufanyishwaji Kazi kwa Nguvu.” unasubiri kukubaliwa na Seneti, ukiwa umekubaliwa na wengi katika Baraza la Wawakilishi mwezi Septemba kwa ushindi wa kishindo wa kura 406 dhidi ya 3. Mswada wa ufanyishwaji kazi kwa nguvu utakataza waagizaji bidhaa wa Amerika kununua bidhaa zozote zinazotokea Xinjiang hadi ithibitike kwa ushahidi madhubuti kuwa kufanyishwa kazi kwa nguvu hakukutumika katika uzalishaji wake.

Mnamo mwezi wa Mei 2020, Nancy Pelosi, Spika wa Bunge, alijaribu kuunda mpango wa Amerika kwa msingi wa maadili aliposema, “Kama Amerika haitazungumzia juu ya haki za binaadamu nchini China kwa sababu ya maslahi ya kibiashara, tutapoteza mamlaka yote ya kimaadili kuzungumzia kuhusu haki za binaadamu popote pale duniani.”

Kuamini kuwa msimamo wa Amerika umetokana na kujali kikweli juu ya Waislamu wa Uyghur ni kutofahamu. Uamuzi wa kuweka mswada huu ni ubinafsi wa moja kwa moja. Inahifadhi uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kuendeleza sera ya Amerika ya kuidhibiti China, kupunguza tishio lake kama mshindani.

Lakini hatuwezi kusahau kuwa Amerika haitumii maadili kama msingi wa maamuzi yake. Kila uamuzi unaofanywa na Amerika ni kwa msingi wa manufaa. Hutumia maneno kama maadili na haki za binaadamu ili kufanya maamuzi yake yakubalike.

Amerika iko Dhidi ya Ulazimishwaji wa Kazi kwa Nguvu Pale Inaponufaika tu

Mwaka huu, Amerika imepitisha miswada miwili inayolenga ulazimishwaji wa kazi kwa kushughulikia mlolongo wa usambazaji wa bidhaa ulimwenguni. Kama Sheria ya tatu ambayo ni ya karibuni zaidi itapitishwa na Seneti, itamaanisha kuwa bidhaa zinazotengenezwa Xinjiang ni kwa kutumikishwa kwa nguvu, isipokuwa kamishna wa Idara ya Forodha wa Amerika na Uhifadhi wa Mpaka aseme vyenginevyo.

Huku mswada huu ukiwa umekusanya uungaji mkono kutoka makundi ya haki za binaadamu, hatutopuuza ukweli kuwa sheria zinaelekea kuilenga China. Zaidi ni kuwa, inalenga juu ya kazi za kulazimishwa katika eneo ambalo lina faida kubwa za kiuchumi kwa China, Xinjiang.

Hasa wakati wana historia ya kuzembea juu ya masuala ya kazi za kulazimishwa. Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Ukaguzi ya Amerika, kutoka 2014, mamlaka za Amerika “zimekuwa na rikodi dhaifu za kutoa shinikizo, kutokana na matakwa ambayo sheria za mamlaka za ushurutishaji wa sheria za Amerika lazima zipate taarifa za kuaminika na za moja kwa moja … kuwa bidhaa zinazoshukiwa zinazalishwa na magereza, watumwa, au wafanya kazi wa kulazimishwa ili kukataza uingiaji wake nchini Amerika”

Hii inatufanya tushangae kuna nini nyuma ya maamuzi haya ya sasa. Hasa, wakati yana uungwaji mkono wa vyama vyote viwili (Democrats, cha Biden, na Republican cha Donald Trump).

Ukweli wa kuwa miswada hii inasukumwa na Donald Trump sio jambo la kushangaza. Kwa zaidi ya miaka minne iliyopita, utawala wake umepitisha maamuzi mengi ambayo yameifanya kuwa na mivutano mingi na China. Ameweka kodi juu ya bidhaa zinazotoka China na kuzuia uwezo wa biashara za Wachina kununua teknolojia ya Amerika, miongoni mwa mengine.

Raisi ajaye, Joe Biden, amependekeza kuwa atakuwa muangalifu zaidi juu ya kuanzisha vita vya kibiashara na China. Hata hivyo, hiyo haina maana kuwa utawala wake hautasaidia sera za kuipinga China. Ameelezea kuwa “atahakikisha kuwa vyama vya wafanya kazi na makundi ya mazingira watakuwa mezani katika kujadili makubaliano yoyote na kuisaidia Amerika kuliko China, kuweka kanuni za biashara za kilimwengu, vikiambatana na masuala mengine ya kidemokrasia” (Chanzo nytimes). Ikiifuatilia China juu ya ukiukwaji wa haki za binaadamu ni njia ya kufikia lengo kwa Amerika, njia ya kukabiliana na ushawishi wa China na kuuvuruga uchumi wake, ili ijihakikishie kuwa Amerika inadhibiti hadhi yake ya kuwa ni taifa linaloongoza duniani.

Kuilenga Xinjiang 

Xinjiang ni sehemu muhimu ya mnyororo wa usambazaji bidhaa wa mashirika ya kimataifa. Inazalisha aina tofauti ya bidhaa na ni kitovu cha sekta ya pamba. Uzalishaji wa pamba na nguo bado ni muhimu kwa uchumi wa China. China ni moja ya wazalishaji wakubwa wa pamba, inazalisha kiasi cha asilimia 20 ya pamba yote duniani. Wazalishaji wengine ni India, huku Amerika yenyewe, Pakistan, Brazil, Uzbekistan na Uturuki zikiifuata kwa karibu. Nchini China, kiasi cha “asilimia 84 ya pamba ya China inatoka Xinjiang” (chanzo: BBC). Mauzo haya ya nje yanasaidia kuinua pato lake la taifa GDP. Hivyo, kama Amerika inataka kuulenga uchumi wa China, kama ilivyofanya kwa uwazi katika miaka minne iliopita ya Trump – kisha ikiielekea Xinjiang, ikiyabana makampuni kufanya kazi katika eneo hilo, ni njia bora kwake ya utekelezaji huo.

Itapunguza mauzo ya nje ya China na kuyafanya makampuni kuelekea kwengine – India ikiwa ni mbadala, na Amerika imeonyesha hamu katika kuyasaidia kujikuza kiuchumi ili yaweze kuwa kama ni wakala wa Amerika dhidi ya China na Waislamu wa eneo. Pia kuna ukweli kuwa kuyarudisha makampuni nyumbani, yaani Amerika, itasaidia kuutuliza uchumi wao. Hii ni muhimu kwa sababu kwa mujibu wa Muungano wa Haki za Wafanyakazi, “kiasi cha 1 kati ya 5 ya nguo za pamba zinazouzwa Amerika zina nyenzo kutoka eneo la Uyghur.” Yote haya yanaelezea kwa nini Democrats na Republican wamekuwa tayari kuweka pembeni mivutano yao ya ndani na kufanya kazi pamoja.

Wanasema ndio Njia Pekee. Lakini Hapana.

Katikati ya habari za makampuni kama kampuni fedhuli ya Nike, ikifanya ushawishi dhidi ya mswada, habari za wawakilishi wa haki za binaadamu zinajitokeza, zikieleza kuwa mswada huo ndio njia pekee ya kusitisha ulazimishwaji wa kazi wa nguvu katika eneo hilo. Peter Irwin, afisa mkuu wa mipango wa Mradi wa Haki za Binaadamu wa Uyghur, ameiambia Business Insider kuwa msimamo wa Coca-Cola unaonyesha, “hawana fikra yoyote juu ya namna bora ya kuondoa kabisa ufanyishwaji kazi wa nguvu unaohusiana na eneo la Uyghur” na “Kuliwacha eneo la Uyghur moja kwa moja ni njia pekee ilio bora ya kuhakikisha kuwa uko ndani ya mipaka ya sheria.” Makundi ya haki za binaadamu yanadai kuwa hadi pale tu makampuni makubwa yatakapokata mahusiano yote na viwanda na njia za usambazaji kutoka Xinjiang, uvunjaji wa haki za binaadamu utaendelea.

Ukiweka kando suala la kuwa ni wazi kwamba Amerika inasimama kunufaika na pande zote za mswada, hebu tuzingatie madai.

Je, maovu nchini China yanahitajika kumalizwa? Bila shaka.

Je, Amerika na mswada wake wa kufanyishwa kazi kinguvu utapelekea kuyamaliza maovu dhidi ya Waislamu? Hapana.

Amerika, China na mataifa mengine ya kikoloni yote ni yenye hatia ya uovu dhidi ya Waislamu. Ni suala la kiwango tu au ni suala lipi la kuzingatiwa katika nukta na muda maalum. Lakini zingatia haya – wakati Amerika inalenga ufanyishwaji kazi wa lazima nchini China, China imeruhusiwa kudhibiti mahusiano mapana na mataifa kote duniani. Amerika inajadili hata uwezekano wa kukuza mahusiano na China kwa baadaye. Ikiwa hili kweli ni suala la kimaadili, basi tukio la kuogofya linalohitaji jibu la haraka, kiko wapi kitendo cha maamuzi, ya ushupavu? Kwa nini China bado inaubeba uchumi wa Amerika kwa kuyachukua madeni yake na kuwa na akiba kubwa ya dolari? Kwa nini China bado ni sehemu ya WTO?

Hatutapaswi kushangaa – Amerika yenyewe ina historia ya kutekeleza uhalifu, sasa kwa nini yenyewe ichukue hatua za kimaamuzi kuizuia China kufanya jambo lile lile?

Ndani ya Amerika, Waamerika wenyeji na wenye asili ya Kiafrika wana historia iliojaa vifo na utumwa kwa sababu ya Amerika. Nje ya Amerika, Amerika imeanzisha vita vya kutisha na Iraq – ni hivi karibuni tu imetoa msamaha kwa kampuni binafsi ya wahandisi wa kijeshi iliouwa Wairaqi wanaume, wanawake na watoto. Amerika imetuma droni Afghanistan, hali iliyopelekea watoto wa Kiafghani kuhofia mawingu safi ya kibuluu, ambayo ni hali halisi kwa mashambulizi ya droni. Wanaunga mkono ‘Israel’ na India zinazowashambulia Wapalestina na Waislamu wa Kashmir. Msururu ni mrefu lakini tunapaswa kufahamu kadhia hii kwa undani na kutokea kila upande – kuishutumu China sio jibu kwa suala la haki za binaadamu, na sio kwa sababu ya kuwa ni suala la kimaadili. Ni njia ya kufikia lengo – Amerika inataka kuhakikisha kuwa inadhibiti nguvu zake za kisiasa na kiuchumi, na kuiendea Xinjiang ni namna ya kutekeleza hilo.

Kusuluhisha tatizo hili na kuleta mabadiliko ya kweli, ni lazima tufahamu kuwa uhalisia wa Waislamu hautobadilika hadi nidhamu ya utawala katika ulimwengu wa Kiislamu ibadilike, na tusimamishe tena Dola ya Kiislamu kwa njia ya Utume. Ni wakati huo tu ndipo nidhamu itakapokuweko, ambapo mtawala atafahamu wajibu wake wa kuwalinda Waislamu na sio kulinda maslahi ya kisiasa na kiuchumi.

Hivyo, wakati tunalazimika kuwa na ufahamu na kuleta mwamko kuhusu maovu yanayofanywa dhidi ya Waislamu, kupata ufumbuzi wa tatizo ni lazima tutake mabadiliko. Mabadiliko haya yatakuwa yenye maana pindi yakijengwa juu ya hukumu ambazo Mwenyezi Mungu (swt) ametupatia – katika hali hii, kuangalia namna ambayo tutaweza kuishughulikia China, nchi iliyo na historia ya kuvunja haki za raia wake, na namna Waislamu wanapaswa kuishughulikia nchi inayo wanyanyasa ndugu zao.

Ni lazima tufahamu kuwa hairuhusiki kufunga mkataba wowote wa kudumu pamoja na nchi adui, kiuchumi, kisiasa, kijeshi au kiutamaduni. Waislamu wanaruhusika kukubali sitisho la muda tu la mapigano na nchi kama hizo adui tulizo na vita nazo, katika hali ambapo kuna haja kufanya matayarisho ya vita, au sababu yoyote inayolazimisha haja hiyo. China ni kama nchi hizo, kama ilivyo Amerika. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

   [إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale waliokupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalim.”  [Al-Mumtahina 60:9].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu