Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dola ya Kitaifa, ni Fikra Duni, Yenye Athari ya Maangamivu kwa Wanadamu

Mwishoni mwa karne ya 19, wito wa fikra ya utaifa wa dola ya wasomi bandia wa wakati huo, ambayo imesababishwa na hadhara ya Kimagharibi, imekuwa na athari haribifu katika taasisi ya kisiasa ya Khilafah. Dhana ya utaifa wa dola ilikuwa nyuma ya uundwaji wa katiba ya Uthmaniya ya 1876. Katiba hii ilipelekea kupatikana fungamano la Uthmaniya kama ni msingi wa fungamano hili jipya ambao, licha ya kuwepo kwa utaifa na lugha tofauti, zilizowa fungamanisha raia wote na Ummah kuwa wao ni raia wa Uthmaniya, bila ya kubagua. Katiba hii iliwezesha mafungamano ya kikabila kuchipuza, iliyopelekea kuenea kwa utaifa wa Turania na Waarabu mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Hali hii haikushangaza kwa sababu wale waliojifanya warekebishaji waliopumbazwa na fikra za Kimagharibi walielezewa vyema na mwanafikra kutoka Austria Bischoff kuwa wanajaribu “kufunga ndoa ya moto na maji”. Wamedai kuwa wanataka kuinyanyua na kuimarisha dola ya Uthmaniya kupitia hadhara ya Kimagharibi, lakini mafanikio yao pekee yalikuwa ni kuigeuza Khilafah kutoka kuwa dola iliyokuwa ikitekeleza Uislamu juu ya watu wake na kuwa ni dola sawa na dola ya Kirumi. Walikosa ufahamu msingi wa fikra ya kuwa Dola ya Kiislamu ni kwa watu wote, ambapo hakuna jamii iliyo juu wala kuwa bora zaidi ya nyingine, wala dola kufungamana na taifa au jamii maalumu, kitu ambacho walijaribu kukifanikisha kupitia Katiba ya 1876. Kulingana na sheria hii iliyotangazwa, raia wote wa dola walitakiwa kujulikana kama ni wa Uthmaniya, dini ya dola ikiwa ni Uislamu na lugha yake Kituruki. Haya yote yakifanyika katika kufuata kiupofu dhana ya Kimagharibi ya “dola ya kitaifa.”

Japokuwa Sultan Abdul Hamid II aliipindua katiba hiyo mwanzoni mwa utawala wake, lakini fungamano lililowekwa baina ya watu wa Dola ya Kiislamu mwishoni mwa wakati wake liliathiri fikra zake pia. Ili kuihifadhi Dola ya Uthmaniya kutokana nayo, Sultan Abdul Hamid II alikusudia kubadilisha mshikamano wa Uthmaniya kwa Umoja wa Kiislamu au Mshikamano wa Kiislamu kuwa ndio msingi, lakini hii yenyewe inaonyesha upeo wa athari ya fikra za Kimagharibi juu yake. Hii ni kwa sababu Dola ya Kiislamu haikupanga au kuhisi haja ya kusimama juu ya mshikamano kama huo. Waislamu hawakuhitaji kuwa na wasi wasi wa uhai wa “Dola” yao muda wowote, kwa sababu Uislamu ukizingatiwa kuwa ni mfumo wa maisha, dola kimsingi ikiwa ni sehemu yake, na Uislamu haukutekelezwa isipokuwa kwa uwepo wa mtawala muadilifu. Ni kutokana na fikra hizi na imani ni kuwa Waislamu walihakikisha ulinzi wa dola yao na kubakia watiifu kwake. Fikra kama ya Shirikisho la Kiislamu imekuwa ni zao la ziada la mtiririko wa ushawishi wa fikra za Kimagharibi ndani ya ufahamu wa Waislamu.

Mwanzoni, jaribio la kuunda mshikamano wa Uthmaniya ulikuwa ni kuziba viraka, juhudi za kupatanisha fikra zisizopatana za Kiislamu na za Dola ya kitaifa, ambayo kwa wakati huo, ilikuwa katika kilele chake Magharibi mwa Ulaya. Fikra sawa pia ikipata nguvu katika Ulaya Mashariki, ikikusanya maeneo ya Balkan watu waliozingatiwa kama watumishi wa Dola ya Uthmaniya. Zaidi ya hayo, hili lilikuwa ni jaribio la wazi la kuzipindua hukmu za kisheria zinazofungamana na uendeshaji wa mahusiano baina ya Dola na raia wake. Uzalendo uliwekewa sheria chini ya msingi wa fungamano, ambayo yenyewe imetokana na Kanuni ya Kijamii ikionyesha mahusiano ya kisiasa yaliyopangwa na dola. Ukuzaji wa utaifa wa Uthmaniya katika Dola ya Uthmaniya huku ikifuata dola ya kitaifa imewafanya wana mageuzi kuipeleka Dola ya Kiislamu ukingoni mwa kuanguka. Ilikuwa kwa sababu hiyo ndio, uwepo wa Dola ya Kiislamu haukuweza kufungamanishwa na fikra za Kiislamu zinazo sisitiza uwepo wa dola wa kutekeleza Uislamu na kuueneza ujumbe huu ulimwenguni. Hapa dola ilihalalisha uwepo wake juu ya uzalendo na misingi ya kizalendo ambapo Sultani au mtawala huwa ni mwakilishi wa watu au Ummah, kama ile namna iliyotumika katika dola za kitaifa za Magharibi. Ubunifu huu ulitoa njia kwa wazalendo na harakati za kitaifa kunyanyua miito yao ya kizalendo na kitaifa. Zaidi ya hayo, ilishajiisha siasa ya ubaguzi wa rangi pia, kwa sababu fungamano la Kiuthmaniya, ambalo halikuwa na msingi kwa hakika, halikuweza kujidhihirisha lenyewe bila ya kuchochea uundaji wa fungamano la kikabila, linalokuza udororaji wa Ummah wa Waislamu. Katiba ya 1876, kwa kukiri fungamano la Kiuthmaniya, japokuwa bila kukusudia, limefanya familia na makabila ndio msingi wa muundo wake wa kisiasa ndani ya mfumo wa bodi ya utendaji ya Dola.

Baada ya kuanguka kwa Khilafah ya Uthmaniya, miito ya kizalendo na ya kitaifa ikachochea uharibifu wa fikra za dola ya kitaifa miongoni mwa Waislamu, kwa sababu dola zote ndogo ndogo zisizo na umuhimu mkubwa ambazo wakoloni wasio Waislamu wameruhusu kubuniwa juu ya mabaki ya Khilafah, zimetangaza fikra ya utaifa na uzalendo kuwa ni msingi wa sababu ya mabadiliko ya kisiasa, pamoja na kuwa pia ni msingi wa sheria zao za ummah. Kwa hivyo, ilikuwa rahisi kwa makafiri wakoloni kunufaika kutokana na wingi wa makundi ndani ya dola hizi kwa kuingilia masuala ya dola, kimsingi ni kutokana na udhaifu uliofuatia, ambao baadaye ulizalisha hali ya kutokuwepo utulivu ndani ya dola hizi.

Dondoo kutoka katika muhadhara “Iraq baina ya 1920 na 1930” wa msomi wa Kiingereza Roger Ovine, aliyeiwakilisha 1993 katika kongamano lenye kichwa cha “Utaifa: Malezi yake, maoni, vizuizi na changamoto” lililoandaliwa na jukwaa la utamaduni la Iraq, alisema: “Wakati Waingereza wakitangaza taifa la kisasa baada ya vita vya kwanza vya dunia, tatizo la wengi na wachache lilichipuza. Sawia na tofauti baina ya tafsiri ya wanajamii na makisio ya utambulisho wao mpya ukajitokeza”. Alisema: “Iraq ilikubaliwa rasmi baada ya 1930 na tatizo la utambulisho lilijitokeza tena”.

Dola ya kitaifa ikatafsiriwa kuwa, “Mpangilio wa kisiasa wa taifa maalumu katika nidhamu ya dola”.

Wataalamu na wabobezi wa kisheria wa Kimagharibi wa nidhamu za kisiasa wamekubali kuwa dola lazima ikusanye mambo matatu: watu, ardhi na mamlaka jumla juu ya yote hayo mawili. Na dola ya kitaifa inaundwa kwa muungano wa mambo matatu:

Inaundwa ndani ya mipaka ya kisiasa ya kijiografia, inayowezesha kuhakikisha umiliki wa nguvu zote za kimada, kupanga mahusiano na kuwa na mamlaka ya kutatua mizozo.

Uwepo wa historia au tamaduni au kipengee cha hadhara.

Haki ya kulinda, elimu ya lazima na kupokea kodi jumla.

Kihistoria, dola ya kitaifa ya kwanza iliyoundwa ni Uingereza mnamo karne ya 17. Kisha Ufaransa mwishoni mwa karne ya 18 na Ujerumani na Italia katika karne ya 19.  Hata hivyo, maandalizi ya dola ya kitaifa yalikuwa kabla ya 1648 katika kongamano la Westphalia wakati fikra ya kimataifa ya uzani wa nguvu tayari imeshakubalika. Kulingana na hili, kama dola inahatarisha uwepo wa mataifa mengine kupitia aina ya kujipanua, basi dola zote zijifunge kujilinda dhidi yake, na kuchukua hatua zote kuizuwia, ili uzani wa kimataifa uweze kubakia ambao wenyewe umehakikishwa dhidi ya vita na ndipo uweze kuleta amani.

Kwa mujibu wa nadharia ya Marx, dola ya kitaifa ni matokeo ya machafuko ya ummah dhidi ya uovu wa ubepari unaoweka jukwaa kwa mabwanyenye wa kitaifa wa dola ya kibepari. Katika hatua hii ya ukombozi wa kitaifa, ni muhimu kwa tabaka la wafanyikazi chini ya uongozi wa kikomunisti kuwa waunganishe nguvu pamoja na walio wengi, kwa sababu wao ni kundi lenye nguvu zaidi. Kwa mujibu wa mafundisho yao, dola ya taifa la kibepari linaelemea ukoloni kwa nje na ukandamizaji kwa ndani. Hii ndio sababu ya ukombozi wa kitaifa na uondoshaji wa mipaka baina ya dola za kitaifa huwezekana tu kupitia kundi la wafanyikazi (tabaka la wafanyikazi) kuchukua madaraka. Hii pia inaelezea matendo ya dola za kiujamaa (kisosholist) katika kuunga mkono harakati za uhuru za kitaifa za nchi nyingine.

Utafiti wa kiakili wa uhalisia unatupelekea kwenye hitimisho sahihi, yaani ni utafiti unaofanya kufikiri kuwa ni msingi wa hisia za ukweli na uunganishaji wa taarifa za awali pamoja nayo, badala ya mada, kama wafanyavyo wakomunisti. Sawia na hivyo uhalisia wa dola ya kitaifa ni lazima utathminiwe juu ya msingi huu. Haichukui muda kuelewa kuwa fikra ya dola ya kitaifa ni fikra isiyopevuka inayowasukuma wanadamu kwenye mahusiano ya kitaifa na kikabila, bila kujali kiasi gani tunajaribu kutoona ukweli, kuelekea Ufashisti na Unazi.

Hakuna shaka kuwa fikra ya dola ya kitaifa yenyewe imebeba mbegu za uharibifu pamoja nayo. Hii huonekana kupitia matatizo yote hayo yanayoibuka wakati pakijaribiwa kuitekeleza fikra hii katika uhalisia. Wanadamu wameendeleza fikra ya muundo wa dola ili kupangilia mahusiano ya wanadamu, lakini kwa kutekeleza fikra ya dola ya kitaifa, ima kwa kutafakari ama la juu ya haki za wachache, mkusanyiko wa matatizo tofauti huchomoza. Hii ni kwa sababu haiwezekani kwa nchi kuwa huru kutokana na tofauti za nchi. Neno utaifa linatokana na neno la Kilatini “Natio”, lenye maana ya taifa au linalohusiana na taifa. Kwa msingi huu, kama tafsiri ya watu wa Ulaya iliyotajwa juu, dola ya kitaifa ni dola ya taifa ambapo hakuna taifa jingine linaloheshimiwa ndani ya mpaka wa kijiografia wa taifa hilo, na kuwa mpaka wa kudumu ni jambo la mwanzo wa mambo yote ambayo kukamilishwa kwake ni lazima kwa taifa kuwa dola la kitaifa. 

Ili kutimiza mambo mengine kama ya hadhara na utamaduni, yanayojumuisha lugha na historia, ni lazima kuwa dola za kitaifa kufanya usafishaji wa kikabila kwa wachache au kuyaondoa au kuyabadili, ima yawe machache kiasili yanayoishi katika nchi zamani, pengine kabla ya uundwaji wa dola ya kitaifa, kama Wajerumani walio wachache wa Ulaya Mashariki, wahamiaji wazururaji au Mayahudi wanaoishi Ulaya nk., au wale waliohamia kwenye dola za kitaifa karibuni, kama Waislamu wanaoishi ulimwengu wa Magharibi hivi leo.

Walio wengi hufaidi ubwana na uongozi katika kila dola ya kitaifa. Usalama wa ustaarabu wao, utamaduni, historia na lugha ikiwemo, inayopelekea mfanano wa kulazimisha na mchanganyiko wa wachache. Zaidi ya hayo, istilahi ya mkataba wa kijamii pamoja na dola ya kitaifa pia imetokana na fikra ya Kimagharibi na ni nguzo ya msingi ya mahusiano yote baina ya mtawala na watu wenyewe, miongoni mwa wana demokrasia wengi ndani ya muundo wa mfumo wa kibepari. Kulingana na mkataba huu wa kijamii, watu wana haki ya kuwa na mahusiano huru na ya kiungwana baina yao. Rousseau ndiye aliyeutaja muundo huu kuwa ni Mkataba wa Kijamii. Juu ya msingi wa mkataba baina ya dola na watu, uaminifu kwa dola hupatikana juu ya mahusiano baina ya pande zote mbili. Hata hivyo, mahusiano haya yaani uzalendo, hupingana na fikra ya dola ya kitaifa, yenye kuwakilisha mshikamano wa kikabila na kitaifa. Hii ndio moja ya sababu kuwa tunaona wakati wa mapinduzi ya Ufaransa, yalikusudiwa kubadilisha kabisa tafsiri ya utaifa. Kwa haya, wana fikra wa mapinduzi walijaribu kupatanisha fikra ya dola ya kitaifa na fikra ya mkataba wa kijamii. Kwa hivyo, Mapinduzi ya Ufaransa yalionekana kuwa ni msingi wa taifa la kisasa, lisiloungana na chimbuko la kibayolojia, bali ni maamuzi huru ya wananchi, wanaotaka kuishi maisha yao ya pamoja chini ya sheria zao bila vikwazo. Hii ndio inayojulikana sasa kuwa ni ubwana wa watu katika fikra ya kisiasa ya Kimagharibi. Juu ya msingi wa fikra hii, mapinduzi ya kitaifa ya Ufaransa yamekuza utaifa wa jamii ya kimfumo, utaifa wenye mamlaka yasiyo na fungamano, utaifa wa wananchi wenzao, ambao sio utaifa uliounganishwa na jamii maalumu, na pia utaifa wa watu wazima. Hii ndio namna ya Mapinduzi ya Ufaransa yaliwaingiza Wafaransa wa Kiyahudi kuwa ni Watu wa Ufaransa au Raia wa Ufaransa, kwa kuunda upya maana ya utaifa wa Kifaransa.

Hii haimaanishi kuwa matatizo mengine yenye kujitokeza kupitia utekelezaji wa dola ya kitaifa utateketea kabisa kupitia uundwaji huu mpya wa maana ya utaifa, ambao wenyewe unajikanganya na uhalisia wa ukabila au utaifa wa kibaguzi. Hata baada ya haya, hasa katika dola kama Ufaransa, suala la usalama wa hadhara na utamaduni kwa taifa la Ufaransa umeendelea kubakia. Hii inaunda msingi wa sera za Wazungu, hasa Wafaransa, kwa ajili ya Waislamu pia. Hutaka utekelezaji wa sheria za Kifaransa juu yao kulingana na katiba ya Kifaransa, na pia wameshajiisha uundaji wa mshikamano wa kizalendo baina yao na dola ya Kifaransa kuwa ni mkataba. Lakini ukweli halisi ni kuwa tunaona msukumo wa serikali na vyombo vya habari kuwaingiza Waislamu ndani ya jamii kubwa ya Kifaransa na kuwashurutisha kubeba utaifa wa Kifaransa kwa mujibu wa tafsiri yao. Kwa dhumuni hili, dola ya Ufaransa imebadili kanuni za miongozo moja kwa moja. Dola iliamini kuwa Waislamu hawana budi kuchanganywa kitamaduni na jamii ya Wafaransa kupitia utenzaji nguvu za kisheria, na hatimaye masharti mapya yaliundwa kuhakikisha uzalendo na utiifu. Waislamuu wa Ufaransa walipewa chaguzi mbili nchini Ufaransa, ima wakubali ushawishi wa sheria za kizalendo au warudi nyuma kuachana na uzalendo, na kwa hilo, waachane na uraia. Kwa upande mmoja inadaiwa kuwa ubwana uko kwa watu, kama kuwa watungaji wa sheria; basi inawezekana vipi chapa mpya ya utaifa wa mjumuisho kuwa umefikiwa baada ya mapinduzi ya Ufaransa, itatengwa kwa namna ambayo, sehemu kubwa ya jamii inapingana nayo, itawekwa kando nayo kwa namna ya kikatili? Hili liliwezekana tu kwa sababu jamii iliyohodhi madaraka ya Kifaransa ilitaka kumiliki jamii kwa mujibu wa hadhara na utamaduni wao. Kwa kuwa hili lilikuwa ndio sharti pekee lililohakikisha nguvu ya utamaduni wa Wafaransa asilia. Hili kwa hakika linaonyesha kuwa makubaliano juu ya tafsiri mpya ya utaifa wa kuunganisha dola ya kitaifa na mkataba wa kijamii halikusuluhisha tatizo msingi. Hii inaonyesha tu kuwa fikra ya dola ya kitaifa kuwa si ya kiakili na ni uongo, sio tu katika msingi wake lakini pia katika utekelezaji wake.

Dola ya kitaifa yenyewe ni fikra duni, inayowabagua watu kwa misingi ya kijamii na kikabila na inaleta matatizo na maafa kwa watu katika ardhi. Inakuza majivuno ya taifa, inafundisha hisia za kitaifa na kizalendo kwa wananchi wengine, na kwa walio katika mamlaka kwa kuwaingiza katika vita kwa sababu ya manufaa ya warasilimali makafiri wenye nguvu. Hii ikapelekea kuzalisha matatizo kama uangamizaji wa kikabila na uunganishaji wa nguvu wa kitamaduni.

Hivyo, fikra ya dola ya kitaifa ni ya kiunyonyaji, kutumia nguvu na uvamizi, na hii ndio pia ikawa msingi wa mahusiano baina ya mataifa.

Uislamu unaangazia lengo la mataifa na makabila kuwa ni kujuana au kutambuana. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran,

(يَـٰٓأَيُّھَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ۬ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَـٰكُمۡ شُعُوبً۬ا وَقَبَآٮِٕلَ لِتَعَارَفُوٓاْ‌ۚ إِنَّ أَڪۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَٮٰكُمۡ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ۬)

“Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [Al-Hujraat:13]

Vile vile, utaifa umechangia dhima muhimu katika kuivunja Dola ya Khilafah. Ndani ya dola mpya za kitaifa zilizoibuka, zilizoletwa na wakoloni makafiri juu ya vifusi vya Dola ya Kiislamu, tatizo jipya la wachache liliibuka katika ulimwengu wa Waislamu. Tatizo hili la wachache lilifungua milango kwa wakoloni makafiri kuingiliakati mataifa hayo. Lengo la uingiliajikati huu ulikuwa ni kuwagawa zaidi vipande vipande na kuhakikisha uwepo wa uvamizi wao katika ulimwengu wa Waislamu.

Katika utofauti wa wazi wa dola duni ya kitaifa, sheria za Kiislamu huzingatia wanadamu wote kuwa ni sawa kwa uoni wa dola. Hakuna jamii iliyo juu ya nyingine wala taifa lolote juu ya jingine. Hakuna Muarabu aliye juu ya asiyekuwa Muarabu, isipokuwa kwa taqwa yake na kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt). Katika Dola ya Khilafah, wasiokuwa Waislamu huamiliwa sawa na Waislamu. Hairuhusiki kwa dola kubagua baina ya watu wake katika masuala ya utawala, sheria au ustawi, bali ni wajibu kuwachukulia kwa usawa bila ya kuzingatia utaifa, dini, kabila au rangi.

Kwa kuwa Dola ya Kiislamu “Khilafah” ni dola ya kibinadamu kwa watu wote, sio dola ya kidini wala ya kitaifa chini ya vidokezo vya Kimagharibi. Hivyo, itakuwa ni mdhamini wa amani, yenye kutangulia katika uadilifu, na mtoaji wa haki kwa wote, kutoka siku ya kwanza itakayosimamishwa, kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu (swt). Watu watafuata Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa makundi na umati, kama ni matokeo ya utekelezaji sahihi wa Uislamu na kueneza uadilifu na utulivu katika ardhi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuharakisha nuru ya siku hii. Amiin.

Ewe Mola wetu! Tukubalie, na dua yetu ya mwisho ni kuwa shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wa Ulimwengu wote (Duniani na Akhera).        

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari a Hizb ut Tahrir na

Bilal Al-Muhajir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 10 Mei 2020 11:42

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu