Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urasilimali Uko Taabani

Milton Friedman, mwanzilishi wa uliberali mpya, aliandika katika kitabu chake juu ya Urasilimali mwaka 1981: Ni mgogoro tu – ima wa kihakika au wa kudhaniwa – huleta mabadiliko ya kweli. Wakati mgogoro huo ukitokea, hatua zinazochukliwa hutegemea fikra zilizopo.” Aliitumia fursa kikamilifu kutetea fikra hizi za soko huru za kiliberali baada ya matatizo ya kiuchumi ya miaka ya sabiini, baada ya kuwa ukingoni kwa muda mrefu. Hivi leo, Urasilimali unakabiliana na mvutano wa kubakia hai baada ya mgogoro wa kiuchumi wa kiulimwengu wa muongo mmoja uliopita na hivi sasa janga la maambukizi ya kiulimwengu yameongeza idadi kadhaa ya mienendo.  

Maandamano nchini Amerika yaliotokana na kifo cha George Floyd na polisi wa Minneapolis yameidunisha nafasi ya Amerika kiulimwengu na dai la kuwa ni nchi kwa ajili ya wote. Kwa kipindi kirefu, hadhara ya Kimagharibi imedai ubwana kwa kule kutaalamika kwake kunakoonekana kuwa kumeileta dunia kuchukukua fikra za pamoja, maadili na imani juu ya namna jamii zinapaswa kuendeshwa. Hii ilimaanisha watu kupanda kiwango cha juu zaidi na sio kufungwa katika maeneo ya kuzaliwa, rangi au kabila lakini kwa mfano ulio bora wa pamoja na maadili. Ushenzi wa zama zilizopita ambao dunia iliushuhudia ungeweza kuzuiliwa kupitia michezo badala ya viwanja vya vita na mapigano. Lakini hata kabla ya matukio nchini Amerika, sehemu kubwa ya dunia ilikuwa inaelekea kwenye siasa za utetezi wa umma, ufashisti na ubaguzi wa rangi. Raisi wa Amerika, Donald Trump, hata kabla ya madai dhidi ya waandamanaji, amewaita Wamexico kuwa ni wabakaji na Waislamu ni tishio kwa usalama wa taifa. Ulaya, ambayo ndio kitovu cha mauwaji ya kimbari ya wayahudi, ndio nyumbani kwa wafuasi shupavu wa mrengo wa kulia ambao sio tu wanafanya vizuri katika chaguzi bali wanaongeza viti vyao katika siasa za kitaifa. Kwa wengi, ubaguzi kama huo huonekana kuwa ni suluhisho la kuwasili kwa wahamiaji wengi.

Tukija kwa upande wa utawala, demokrasia pia iko katika mgogoro. Wakati raisi wa Amerika Abraham Lincoln alipotoa hotuba yake maarufu ya 'Gettysburg Speech' mwaka 1863 kuhusu ‘nidhamu ya watu, inayo endeshwa na watu na kwa ajili ya watu’, nidhamu ambayo hakuna aliye mkubwa juu ya mwengine, ambapo kila mmoja amekuwa huru na maamuzi yakifanywa kwa manufaa ya wengi na sio wachache, kasi ya msukumo wa fikra hii msingi ilikusudiwa kuifanya mifumo ya kizamani iliokuja kabla yake iwe ni historia. Lakini hivi sasa, demokrasia inazama ndani ya misingi ya nadharia yake yenyewe. Huku wengi watakubali kuwa viongozi wao wanapaswa kuchaguliwa, uhalisia wa demokrasia ni kuwa chaguzi za kawaida zinawapendelea wale wenye pesa na kuathiri utoaji wa maamuzi kwa namna mbaya. Wingi wa chaguzi umekuwa ukiwapendelea wanasiasa dhidi ya kukabiliana na changamoto za muda mrefu na badala yake kulenga umaarufu wa muda mfupi. Katika sehemu kubwa ya ulimwengu wa nchi zilizo endelea, kikundi cha watu wateule wamekuwa ni wenye kumiliki nidhamu za kisiasa: imekuwa ni nidhamu ya utawala wa wachache na kwa ajili ya wachache. Demokrasia hivi leo imekuwa ni nidhamu ambayo huwazawadia tabaka lake teule kupitia makato ya kodi. Hivi leo wanasiasa ni wenye kuogopwa zaidi ya wakusanyaji kodi wanaposhindwa kuziwakilisha. Hasira kwa tabaka la wanasiasa wateule zimechochea machafuko ya kisiasa kote duniani. Viongozi wapinzani, vyama na harakati zimeibuka kutoka pande zote mbili kulia na kushoto, za mirengo ya kisiasa, baadhi ya wakati wakipambana na maadili msingi na taasisi za demokrasia huru. Taasisi ambazo hufuatilia demokrasia zimeripoti kushuka kiulimwengu katika uhai wa demokrasia.

Tumekuwa tukiambiwa kuwa Urasilimali ni mfumo uliofanikiwa zaidi katika usimamizi wa soko katika historia. Idadi ya watu waliotolewa kwenye umasikini kwenda kwenye ustawi, kiwango kinachopanda cha utajiri duniani, kuongezeka kwa kiwango cha umri wa maisha na maendeleo ya kiteknolojia, yote yamekuwa ni shukrani kwa Ubepari na masoko huru yasiofungwa, kuvifanya vitu na shughuli kuwa ni kwa ajili ya fedha, na biashara huru. Lakini hadi usiku huu, nusu ya walimwengu, watu bilioni 3.8, hawatokuwa na cha kukila usiku huu kwa kuwa ni masikini sana. Watu wengi zaidi wanamiliki simu za mkononi kuliko vyoo. Katika hali ya kushangaza, asilimia 1 tu ya watu wote duniani hivi sasa wanamiliki asilimia 82 ya utajiri wa dunia. Bosi wa zamani wa Unilever sasa anauita ubepari kuwa ni mfumo mbovu. “Ubepari, ambao umehusika na ukuaji (wa uchumi) na mafanikio ambao umefanya mengi zaidi kuboresha maisha yetu, ni mfumo mbovu na unaohitaji kuvumbuliwa upya kwa karne ya21” [1] Kile kilichochukuwa nafasi ni uporaji ambapo imekuwa ni njia ya maisha kwa kipote teule kidogo, ambacho ndani ya mwendo wa miongo miwili wamejiundia mfumo wa kisheria ambao unatoa mamlaka na maadili ambayo yanaukuza. Kwao wao dunia imejaa nguvu kazi rahisi ambayo inapaswa kutumiwa kutengezea faida, bila kujali matokeo. Wengi hivi sasa huweza kuona serikali za kitaifa zifanya kazi kiweli kweli kwa ajili ya maslahi ya

asilimia 1 ya walio juu na kuwadhibiti waliobaki. Wengi huweza kuona sasa kuwa wameachwa nyuma wakati wachache wanaowezeshwa kutumia fursa hunufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na hasara ya waliobaki. Historia imejaa mifano ya kipote cha wateule wanaohiyari maslahi yao ya muda mfupi dhidi ya waliobaki na kukosekanwa kwa usawa huu kunapatikana kwenye kiini cha karibu kila mapinduzi katika historia.  

Fikra ya uhuru inayolenga mtu mmoja mmoja na uhuru wao imekuwa ni ya bora kwa wachache lakini ni mateso kwa wengine waliobaki. Ubepari na Demokrasia vimefeli vibaya sana, muda baada ya muda dunia inaonyesha kuwa mifumo ambayo walinganiaji wake hudai inafanya kazi kwa ajili ya wengi, kwa hakika inafanya kazi kwa ajili ya wachache. Fikra za kisiasa zinazo tokana na uliberali zimeindwa kwa ajili ya matajiri na huwadharau pakubwa masikini. Hii ndio sababu hamu ya mabadiliko inashuhudiwa kwa kukataa sura za jadi ziliojiimarisha japokuwa zimebadilishwa kwa sura nyengine mpya zilizojiimarisha. Udhaifu wa uendeshaji wa kawaida wa mifumo hii huonekana katika maandamano ya Gilet Jaunes (vizibao vya manjano) nchini Ufaransa dhidi ya kuongezeka kwa kodi, maandamano yalioenea nchini Sudan, maandamano nchini Jordan dhidi ya hatua kali zinazochukuliwa na serikali za kubana matumizi na kuongeza kodi. Hamu ya kuleta mageuzi itaongezeka pale tu hali ya uchumi itakuwa mbaya zaidi kiulimwengu na gharama za mahitaji muhimu kuwa kubwa zaidi kwa watu wengi zaidi.  

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu