Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuanguka kwa Dini Katika Mfumo wa Kisekula sio Ajabu, ni Jambo Lakutarajiwa

Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa kuna muanguko wa dini kiulimwengu. Ikiangaliwa katika jamii za Kimagharibi, na kukua kwa uliberali wa kisekula, hili halishangazi. Kwa mujibu wa makala katika Wizara za Mambo ya Nje, kuna idadi inayoongezeka ya watu ambao “hawaioni dini kuwa ni chanzo muhimu cha usaidizi na cha maana katika maisha yao.” Wao “wamekuwa ni watu wasioibeba sana dini kwa sehemu fulani kwa sababu hawaihitajii tena katika kuzingatia aina za maadili ya kijinsia na ya kingono ambapo dini kubwa ulimwenguni zimekuwa zikisisitiza kwa karne nyingi.” Makala ya Wizara za Mambo ya Nje imelenga juu ya kuanguka kwa dini katika Ulaya na Asia. Lakini kwa mujibu wa BBC, muanguko huu pia unaonekana katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ambako kuna ongezeko la idadi ya watu wasioshikamana dini sana.

 Je, muanguko huu unapaswa kutushangaza?

Hapana, muanguko huu katika dini haukuja kama mshangao. Msingi hasa wa usekula wa kiliberali ni kuwa dini imejifunga na ibada ya kibinafsi na kwa hivyo, haina jukumu katika kupanga na kutawala masuala ya kijamii. Dini inaonekana kuwa ni suala la imani ya kibinafsi ambayo hutekelezwa kibinafsi. Kwa hiyo, tunaishi katika dunia ambayo usekula unaongezeka  na kutoa “kipaumbele kikubwa kinachoongezeka cha kujieleza na chaguo huru, pamoja na msisitizo unaoongezeka juu ya haki za binaadamu, uvumilivu kwa walio nje, uhifadhi wa mazingira, usawa wa kijinsia na uhuru wa kusema.” (Chanzo: Wizara ya Mambo ya Nje)

Tatizo ni hili; kama tunaitenga dini na maisha ya kibinafsi, basi vipi tutachora mstari? Je, tutaruhusu dini kufundishwa katika mfumo wetu wa elimu? Tutaruhusu dini kuongoza matendo yetu wakati tunashughulika na marafiki zetu na familia, au ni kuiruhusu dini kuelekea zaidi katika kuifunga kwenye maisha yetu ya kibinafsi. Kama tunaruhusu dini kuongoza maisha yetu hapa, itakwenda kwa umbali gani? Je, itumike kama msingi wa maamuzi yetu wakati tunapokabiliana na sintofahamu? Itakuwaje kama sintofahamu hii ni katika masuala ya kisheria?

Ukweli ni huu – kuanguka kwa dini katika jamii inayoelekea zaidi kwenye uliberali isitushangaze. Wanayo jamii ambayo wazo la kuwa na dini sio msingi wa fikra na matendo, bali uliberali ndio msingi. Matokeo yake, dini sio sehemu ya maisha ya watu. Manufaa ya kiuchumi ni nukta inayolengwa katika kufanya maamuzi. Maadili ni suala linaloweza kujadiliwa kulingana na manufaa na ubinafsi. Na dini hutumika kama ni chombo cha wanasiasa; ili kudumisha uungaji mkono wa mfumo wa kiliberali katika nchi ambazo awali zilishikamana sana na dini, kuhakikisha mshikamano wa kijamii kwa kuwa ubinafsi katika uliberali huvunja fungamano la kijamii na kueneza fikra kama ‘maisha ni kwa wenye kustahiki’.

Usekula huu haukupelekea kwenye jamii ilio imara. Ni kinyume kabisa, umetengeneza na kuongeza matatizo ya aina mbali mbali bila ya utatuzi wowote. Ubaguzi wa rangi, taasubi ya kijinsia, uchukivu kwa wanaovunja maadili, unyanyasaji wa kijinsia, vurugu za utumiaji wa silaha, mauaji, mateso, mauwaji ya halaiki; hii ni mifano michache tu ya matatizo ambayo jamii ya kiliberali imeshindwa kuyatatua.

Takwimu kuhusiana na kuanguka kwa dini zisitufadhaishe, zitufanye tufikiri. Ongezeko la kutoridhika kwa jamii ya Wamagharibi na athari ya COVID, imetufanya tuwe kwenye hatua ya mabadiliko katika historia. Mfumo wa Kimagharibi umejaa nyufa na nyufa hizo zinaongezeka na kuwa wazi zaidi. Wanatafuta njia ya kuziba nyufa hizo, au kugeuza mazingatio yetu kwa kueneza hisia zinazopingana na dini, hisia zinazopingana na uhamiaji. Ni mbinu ambayo daima wamekuwa wakiitumia wanapokuwa na matatizo – tengeneza adui ili Ummah wa Kiislamu pamoja na watu wao wenyewe wasitafute badali na kutafuta masuluhisho ya matatizo yao katika Uislamu. Lakini hii itukumbushe sisi kwa nini tunahitaji kufanya kazi ya kusimamisha Dola ya Kiislamu na kutazama uhalisia wa leo kama fursa.

Tunahitaji kukumbuka kuwa Uislamu sio kama dini nyengine – inakusanya fikra na masuluhisho ya matatizo ya wanaadamu kwa kina na kuathiri kila kipengele cha maisha yetu. Historia ya Uislamu na mafanikio ya Dola ya Kiislamu ni ushuhuda kwa hili. Hali ya sasa ya mambo na kuanguka kwa dini ni jambo likutarajiwa kwa sababu Uislamu hautekelezwi kwa ukamilifu wake.

Tunahitaji kusimamisha tena Dola ya Kiislamu

Kwa kweli hatuwezi kuitenganisha dini na dola – tunahitaji msingi wa kuongoza matendo yetu na kama uhalisia wa sasa unavyoonyesha, akili zetu wanaadamu zikiwa na haja na matashi, sio msingi wa kuhukumu kilicho kizuri na kibaya. Kwa hivyo, dini sio kitu ambacho kinaweza kutengwa katika maisha yetu ya kibinafsi, kuna matatizo mengi sana na mivutano ambayo inayowasili. Dini haiwezi kufungwa na kipengele kimoja cha maisha yetu. Hilo halitakuwa tatizo la Uislamu – pindi utapotekelezwa kama inavyopasa, kwa usimamishaji tena wa Dola ya Kiislamu.

(الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا)

”Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndio Dini” [Al-Maida: 3]

Pia ni muhimu kukumbuka kuwa wakati mfumo wa Kimagharibi na wafuasi wao wamejaribu kutusukuma kuubeba uliberali, Ummah wa Kiislamu umedumisha mshikamano wao kwa Uislamu.

Lakini ni lazima tusisahau kuwa Uislamu hautekelezwi kama inavyotakiwa. Kuisimamisha Dola ya Kiislamu humaanisha kukubali kuwa Sheria za Mwenyezi Mungu ndio msingi wa maamuzi yetu yote. Hatuwezi kuwa na mfumo wa kisekula, na baadaye kutarajia Uislamu uafikiane nao. Chini ya Uislamu, maadili sio kitu cha kujadiliwa. Mwenyezi Mungu, Muumba wetu, ambaye anatuelewa sisi zaidi ametupatia sheria juu ya namna ya kuamiliana baina yetu.

Masuala ya dini na dola lazima yaunganishwe na kuenezwa kwenye kila kipengele cha maisha yetu, na kuathiri jamii na mtu binafsi. Sheria ambazo zinatuongoza, katika kila kipengele cha maisha yetu, na kuwaongoza watawala wetu kuhakikisha kuwa watu wanalindwa na kupewa haki zao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 22 Oktoba 2020 12:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu