Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sheria ya Kiislamu Inakataza Makubaliano ya Amani na Umbile la Kiyahudi

Kufanya makubaliano ya amani na umbile la Kiyahudi imekuwa ni jambo linalojadiliwa kwa muda mrefu na Ummah tokea kuanzishwa kwake. Kila wakati makubaliano ya amani yanapo fanywa pamoja na umbile la Kiyahudi, yalikuwa yakihalalishwa kwa kunukuu mkataba wa Hudaybia kama ushahidi wa kuwa na makubaliano ya amani na umbile haramu la Kiyahudi. Kwa kweli, Sheria ya Kiislamu inakataza kufunga mkataba wowote na maumbile haramu kama umbile la Kiyahudi ambapo Waislamu wananyanyaswa na kutawaliwa na maadui. Mkataba wa Hudaybia ulikuwa si chengine bali ni ushindi kwa Waislamu na udhalilifu kwa maadui wa Mwenyezi Mungu. Zifuatazo ni dondoo za tafsiri zilizotolewa na mwanachuoni maarufu Sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah (hz) katika Surah Baqarah, aya ya 208 ambayo inafafanua kukatazwa kufunga mikataba ya amani na umbile la Kiyahudi. Dondoo hizi ni:

2- Sio sahihi kutafsiri neno (السِّلْمِ), hapa, katika aya hiyo tukufu kwa maana ya “kuweka amani” (المسالمة) na maadui. Hii sio sawa hata kama neno (السِّلْمِ) lina maana zote mbili yaani ‘Uislamu’ na ‘kuweka amani’ yaani neno (السِّلْمِ) lina maana nyingi. Kwa sababu hiyo, hili ni neno tata (mushtarak), lina maana zaidi ya moja, na hivyo ni mutashabih (kufanana), linabeba tafsiri nyingi. Kusudio ni kubaini ipi kati ya maana hizo itakayoweza kueleweka kutoka katika muktadha (umoja: qarinah, wingi: qaraa’in) yenye kuhusiana na hili katika aya ambazo ni Muhkam (sahihi au zenye maana moja tu).

Kama neno (السِّلْمِ) hapo ilimaanisha ‘kuweka amani,’ hivyo maana ingelikuwa ‘ingieni katika amani na maadui kikamilifu.’ Agizo (amri) ingelikuwa ni ya ulazima (wajiib), kutokana na muktadha (qarinah) kwa aya hii[وَلاَ تَتَّبِعُواْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ]  “Wala msifuate nyayo za Shetani kwani huyo ni adui wa wazi” kwa hiyo, kuweka amani kikamilifu na adui ingelikuwa ni wajibu (faradhi) kwa waumini. Hata hivyo, maana hii inapingana na aya za muhkam zinazohusiana na uwajibu wa kupigana waumini dhidi ya makafiri, hadi Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) iwe juu, ima waingie katika Uislamu au kulipa Jizya ili kujisalimisha katika Mamlaka ya Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

 [وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلّه]

 “Na piganeni nao mpaka isiwepo na fitina na hadi Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” [Quran 8:39]Na Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[قَاتِلُواْ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلاَ بِالْيَوْمِ الآخِرِ وَلاَ يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللّهُ وَرَسُولُهُ وَلاَ يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حَتَّى يُعْطُواْ الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ]

“Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho, wala hawaharamishi alivyo haramisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawashiki Dini ya haki, miongoni mwa walio pewa kitabu, mpaka watoe jizyah kwa khiyari yao, hali wametii” [Quran 9:29]. Na hadithi,

«الجهاد ماض إلى يوم القيامة»

“Jihad ni endelevu hadi siku ya kiama” [Bukhari 3/1048; Abu Dawud: 2532; Bayhaqi: 9/156]. Hizi zote ni muktadha juu ya kuendeleza mapigano dhidi ya makafiri hadi neno la Mwenyezi Mungu (swt) liwe juu, kwa kujisalimisha makafiri katika utawala wa Uislamu. Hii inabainisha kuwa neno (السِّلْمِ) katika aya tukufu limekuja na maana ya Uislamu na sio kuweka amani (Musalama) na maadui, kutokana na kukinzana na aya za Muhkam za kupigana dhidi ya maadui. Aya za Muhkam zinazizidi nguvu aya za Mutashabihati (zenye maana zaidi ya moja) na hivyo maana ya aya inatakiwa iwe ‘Uislamu’ yaani kuingia katika Uislamu kikamilifu.

3- Ama kuhusu neno (السِّلْمِ) Silm ambalo limekuja katika Quran kwa maana ya ‘kuweka amani’ (Musaalama), (المسالمة) limetokea katika aya mbili: moja ni katka Surat al-Anfal na nyengine katika Surah Muhammad. Tunapo chunguza aya hizi mbili, tunaona kuwa zinaonyesha hali (حال) ya neno (السِّلْمِ) kuwa na maana ya ‘kuweka amani’:

a-Ayah hii katika Surat al-Anfal,

[وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ]

“Na wakielekea amani (سَّلْمِ), nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika yeye ndie mwenye kusikia mwenye kujua” [Surat Anfal; 61]. Ayah hii inatoa maana ya kuwa ‘kama makafiri wataelekea na kuhitaji kuweka amani, basi wakubalie na mtegemee Mwenyezi Mungu (swt) katika hayo yote’. Uunganishaji wa kuwa na Tawakkul na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kuridhia amani pindi watakapo hitaji, ni Qarinah kuwa Waislamu wanatakiwa wakubali katika hali ya kuwa na nguvu. Hii iko wazi katika aya za nyuma:

 [الَّذِينَ عَاهَدتَّ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِي كُلِّ مَرَّةٍ وَهُمْ لاَ يَتَّقُونَ * فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ * وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَانبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَى سَوَاء إِنَّ اللّهَ لاَ يُحِبُّ الخَائِنِينَ * وَلاَ يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ سَبَقُواْ إِنَّهُمْ لاَ يُعْجِزُونَ * وَأَعِدُّواْ لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدْوَّ اللّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لاَ تَعْلَمُونَهُمُ اللّهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لاَ تُظْلَمُونَ]

“Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila mara, wala hawamchi Mungu. (56). Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka. (57). Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini. (58). Wala wasidhanie wale walio kufuru kwamba wao wametangulia mbele. La, wao hawatashinda. (59). Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa. (60)” [Surah al-Anfal: 56-60].

Yaani, pigana na makafiri kwa ukali hadi uoga na hofu viwaingie katika nyoyo za maadui ambao hata watakao sikia tu, mpaka wakimbie kwa uoga katika mapigano hayo kabla hayaja wafikia. Yote haya yanakuja kwa kuingiza hofu katika nyoyo za maadui wa wazi na waliojificha kupitia nguvu ya maandalizi.

Baada ya kupitishia kipigo kikali dhidi ya adui, ikiwa adui atahitaji kufanya amani kutokana na kile kilichomtokea cha kuanguka na kusambaratika, basi mkubalie, kwani atakuwa ameshajisalimisha kwako na silaha zake kuvunjika.

b-Na katika aya nyingine, ni katika Surat Muhammad,

[فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ]

“Basi msiregee na kutaka suluhu (السَّلْمِ), maana nyinyi ndio mtakaoshinda, na Mwenyezi Mungu yupo pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu” [Quran Surat Muhammad: 35]

Ayah hii inaonesha kukatazwa (tahrim) kuitisha makubaliano ya amani na adui, kwani ni aibu na udhalili, ilhali Waislamu ni wenye nguvu. Ndio maana Mwenyezi Mungu (swt) yupo pamoja nao. Naye (swt) hatopunguza chochote katika malipo yao, kutokana na ushupavu wao katika kupigana dhidi ya adui, bila ya kuweka amani nao. 

Hiki ndicho Qur-an ilichokileta kwa pamoja katika aya mbili hizi

[وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلْمِ]

  “Na kama wataelekea kutaka amani…” [Qur-an 8:61] 

Na aya                         

[فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ]

   “Wala msiregee na kutaka sulhu” [Qur-an 47:35]

Hukumu ya kuweka amani na adui itakubaliwa kama:

Kwanza; Kama adui ameomba kupata amani, kutokana na udhaifu wake na kuharibikiwa kwake kwa sababu ya nguvu ya Waislamu na ushindi wao.

Pili; Kama itapelekea utukufu wa Waislamu na kusafisha njia yao ya ushindi, na kwa kuwadhalilisha maadui na kusafisha njia yao ya kushindwa.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amefafanua mukhtasari huu katika mkataba wa Hudaibiyah;

A-Kabla hajaenda Umrah, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alijuwa kwamba mayahudi wa Kikuraishi walitaka kutengeneza muungano na Makuraishi ili wapigane na Mtukufu Mtume (saw).

Hivyo, kuwadhoofisha Makuraishi ulikuwa ni ushindi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Hivyo basi hatua ya mwanzo ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliitekeleza baada ya kurudi Madina, ilikuwa ni kuivamia Khaybar na kuwatenga Mayahudi, baada ya Yeye (saw) kuwa amewadhoofisha Makuraishi kwenye Mkataba wa Hudaibiyah katika kuungana Khaybar.

Wakati (saw) alipokuwa anarudi kutoka Hudaibiyah kuelekea Madina njiani, aya ifuatayo ikateremshwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w)

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿

“Hakika tumekufungulia wewe {Muhammad}, ushindi wa dhaahir” [Surah Al-Fath 48:1].  Mkataba wa Hudaibiyah, ukifuatiwa na ushindi wa Khaybar, ulikuwa ni ushindi wa wazi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kulipatikana izza kubwa kwa Waislamu na udhaifu mkubwa kwa makafiri katika Mkataba wa Hudaibiyah.

B-Kupitia khofu kwa Makuraishi, makabila ya Kiarabu yaliogopa kuingia katika Dini ya Muhammad (saw) na agano lake. Hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliweza kuondosha khofu hii kwa makabila ya Kiarabu, khofu ambayo iliwazuia kuingia katika Uislamu kupitia mkataba huu. Hivyo Khuza’a (Kabila la Kiarabu) wakaja chini ya agano la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na wengi wakawa Waislamu, kupitia mtu mmoja mmoja na pia kwa makabila yote, bila kuogopa kuvamiwa na Makuraishi. Hii ilikuwa ni nguvu kwa Waislamu na utukufu kwa dini ya Mwenyezi Mungu (swt).

C-Mkataba huu, yaani kufanya amani (Musalama) na maadui ulikuwa wa muda mfupi kwa sababu kusimamisha au kuifuta Jihad hairuhusiwi ndani ya Uislamu. Zaidi ya hayo, ni dhambi kubwa kama ilivyoonyeshwa na maandiko matukufu tulioyataja.

D-Pia, mkataba huu wa muda mfupi ulihitimishwa/ulifungwa na makafiri wa vita, waliokuwa ni watawala juu ya ardhi yao. Haukuhitimishwa na umbile lililotawala ardhi za Waislam, kwani mkataba huo ungeidhinisha utawala wao.  Na hii ni kwa sababu mkataba wa Hudaibiyah ulihitimishwa na makafiri wa Kikuraishi. Umbile lao (utawala wao) kwa zama hizo ulikuwa katika ardhi ambayo haijachukuliwa na Waislamu. Badala yake, ardhi yenyewe ilikuwa chini ya utawala wao kabla ya kuchukuliwa na Waislamu. Ama kuhitimisha mkataba wa umbile linalokalia ardhi za Waislamu, kama vile umbile la Kiyahudi ndani ya Palestina, si sawa kwa kuwa jambo hilo litaidhinisha utawala wa makafiri juu ya ardhi za Waislamu. Na inapingana na aya za kufanya amani ndani ya Surah Al-Anfal na Surah Muhammad na pia inapingana na Mkataba wa Hudaibiyah.

Hivyo hairuhusiwi kufanya amani kabisa na adui, bila ya masharti ambayo yamefafanuliwa ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Ni muhimu kuzingatiwa kuwa mkataba huu ulikuwa ni wa kuwadhoofisha Makuraishi kutokana na Mayahudi wa Khaybar, ili Mtume wa Mwenyezi Mungu ajitoe yeye mwenyewe kupigana na Mayahudi wa Khaybar, lakini wanachuoni wa serikali wananukuu ushahidi wa mkataba huu ili kufanya amani na Mayahudi na kumaliza hali ya vita nao!!

Hivyo, imefafanuliwa hapa kuwa neno (السَّلْمِ) huja katika Quran likiwa na maana ya “kuweka amani” na adui, ambayo ni haramu isipokuwa inapopelekea utukufu wa Uislamu na Waislamu na wakati adui ni dhaifu na silaha zake zimevunjika. Kuweka amani ni lazima kuwe kwa muda mfupi na inaweza kuhitimishwa tu (yaani kufanywa mkataba huo tu) na adui ambaye haanzishi umbile lake (utawala wake) kwenye ardhi iliyo porwa kutoka kwa Waislamu, ya kwamba mkataba huo utaidhinisha utawala wao. Haya ndiyo ambayo aya katika Surah al-Anfal na Surah Muhammad zimeonyesha kama uhalisia wa Mkataba wa Hudaibiyah…” Mwisho wa Kunukuu.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammed bin Farooq

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu