Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mtazamo wa Uislamu Juu ya Upandikizaji wa Moyo wa Nguruwe kwa Binaadamu

(Imetafsiriwa)    

Gazeti la Express Tribune nchini Pakistan limeripoti mnamo tarehe 30 Januari 2022, “Upandikizaji wa mwanzo uliobadilishwa kigenetiki wa moyo wa nguruwe kwa mgonjwa anayeugua mahututi umechemsha mjadala mkali miongoni mwa Waislamu kote duniani. Kwenye mitandao ya kijamii na kwengineko, wengi wameshangazwa na kueleza shaka zao juu ya utaratibu unaoweza kupewa hadhi ya kuharamishwa ya nguruwe katika uono wa Uislamu. Katika suala hili, The Express Tribune lilimfikia Mufti Dkt. Irshad Ahmad Aijaz kutoa mwanga juu ya muendelezo huu. Mufti Aijaz ni mwanachuoni maarufu wa Sharia ambaye pia amebobea kwenye Sheria za Uislamu na Fatwa.

Katika wakati ambapo vyombo vya habari vinatumika kueneza uoni wa kiliberali wa kifisadi kote katika Ulimwengu wa Kiislamu, ni jambo la kufurahisha lisilotegemewa kuona kwamba vyombo vya habari vimemtanguliza Aalim kuzungumzia juu ya jambo linalohusiana na masuala ya Ummah wa Kiislamu. Ni hakika kuwa Dini ni njia kamili ya maisha yenye kutoa muongozo unaohusiana na kila kitendo na kila kitu, ikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji kamili. Ni hakika kuwa, ni jukumu la vyombo vya habari kutoa mtazamo wa Kiislamu kuhusiana na matukio. Pia ni jukumu la Ulamaa kuamrisha mema (ma’roof) na kukataza maovu (munkar) juu ya msingi wa Uislamu, ili watawala ndani ya Khilafah watekeleze Uislamu bila kuupindisha.

Kuhusiana na upandikizaji wa kijenetiki ulioboreshwa wa moyo wa nguruwe kwenye mgonjwa aliyeshindikana kutibika, katika Dini tukufu ya Uislamu, matumizi ya vitu vya haram na najisi vinaruhusiwa kwa ajili ya matibabu. Dalili ya matibabu kwa kutumia vitu vya haram na najisi imepatikana katika Sunnah za Mtume (saw), kwa kuwa Sunnah ni zenye kupambanua Quran Tukufu.

Hakika, nguruwe ni haram. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنْزِيرِ]

“Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe.” [Surah al-Maaidah 5: 3]. Uislamu umekataza kuchukua thamani kutokana na vitu vya haram. Abu Dawud amepokea kwa njia ya Abu Hurayrah (ra) kuwa Mtume (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ حَرَّمَ الْخَمْرَ وَثَمَنَهَا وَحَرَّمَ الْمَيْتَةَ وَثَمَنَهَا وَحَرَّمَ الْخِنْزِيرَ وَثَمَنَهُ»

“Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha ulevi na thamani yake; na ameharamisha nyamafu na thamani yake; na ameharamisha nguruwe na thamani yake” Bukhari amepokea kwa njia ya Jabir ibn Abdullah (ra) kuwa amemsikia Mtume (saw) kuwa amesema,

«إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الْخَمْرِ وَالْمَيْتَةِ وَالْخِنْزِيرِ وَالْأَصْنَامِ فَقِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرَأَيْتَ شُحُومَ الْمَيْتَةِ فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ وَيُدْهَنُ بِهَا الْجُلُودُ وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ فَقَالَ لَا هُوَ حَرَامٌ ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ قَاتَلَ اللَّهُ الْيَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ ثُمَّ بَاعُوهُ فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ»

“Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mwaka wa Fathu Makkah, akisema, “Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameharamisha mauzo ya ulevi na nyamafu na nguruwe na masanamu.” Watu wakauliza, ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Unaonaje kuhusu mafuta ya nyamafu, kwani yanatumika kwa kulainishia boti na ngozi; na watu hutumia kwa kuwashia taa?’ Akasema, “Hapana, hiyo ni haram.” Kisha akasema Mtume (saw) kuhusu hilo, “Mwenyezi Mungu (swt) amewalaani Mayahudi, Mwenyezi Mungu alipowaharamishia mafuta waliyayeyusha kisha wakayauza na kula thamani yake.”

Ama kwa vitu vilivyoharamishwa sio haram kwa ajili ya matibabu, dalili yake ni katika Sunnah ya Mtume (saw). Muslim amepokea kuwa Anas (ra) amesema kuwa,

«رَخَّصَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَوْ رُخِّصَ لِلزُّبَيْرِ بْنِ الْعَوَّامِ وَعَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ فِي لُبْسِ الْحَرِيرِ لِحِكَّةٍ كَانَتْ بِهِمَا»

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameruhusu, au amewapatia ruhusa Zubair b. Awwam na ‘Abd Al-Rahman b. Auf , ya kuvaa hariri kutokana na muwasho waliokuwa nao.” Kuvaa hariri kumeharamishwa kwa wanaume, lakini inaruhusiwa kwa sababu za kitabibu. An-Nisa’i amepokea kutoka kwa 'Arafah bin As'ad kuwa,

«أَنَّهُ أُصِيبَ أَنْفُهُ يَوْمَ الْكُلاَبِ فِي الْجَاهِلِيَّةِ فَاتَّخَذَ أَنْفًا مِنْ وَرِقٍ فَأَنْتَنَ عَلَيْهِ فَأَمَرَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَتَّخِذَ أَنْفًا مِنْ ذَهَبٍ»

“Pua yake ilikatwa katika Vita vya Al-Kulab katika zama za Jahiliya hivyo akaweka pua ya fedha, lakini ikaanza kuharibika, Mtume (saw) akamtaka kuweka pua ya dhahabu.” Dhahabu imeharamishwa kwa wanaume, lakini inaruhusiwa kutumika kwa sababu za kimatibabu.

Pia, kuhusu matumizi ya vitu vya najisi sio haramu kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu, imeelezwa vile vile katika Sunnah za Mtume (saw). Bukhari amepokea kutoka kwa Anas (ra),

«أَنَّ نَاسًا، اجْتَوَوْا فِي الْمَدِينَةِ فَأَمَرَهُمُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَلْحَقُوا بِرَاعِيهِ ـ يَعْنِي الإِبِلَ ـ فَيَشْرَبُوا مِنْ أَلْبَانِهَا وَأَبْوَالِهَا، فَلَحِقُوا بِرَاعِيهِ فَشَرِبُوا مِنْ أَلْبَانِهَا وَأَبْوَالِهَا، حَتَّى صَلَحَتْ أَبْدَانُهُمْ»‏

“Hali ya hewa ya Madinah haikuwafaa baadhi ya watu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akawaamrisha kumfuata mfugaji, yaani ngamia wake ili wanywe maziwa na mikojo yao (kwa ajili ya tiba). Wakawafuata na wakanywa maziwa na mikojo yao hadi miili yao ikawa yenye afya.” Baadhi ya watu walikuwa wagonjwa, hivyo Mtume (saw) aliwaruhusu kutumia mkojo (بَوْل), kama tiba, licha ya kuwa ni najisi.

Ni hakika kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha na panapotokea mvutano katika jambo, ni juu ya Waislamu kuielekea Quran Tukufu na Sunnah za Mtume (saw) kutatua hitilafu hizo. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ]

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume.” [Surah an-Nisa’a 4:59]. Mtume (saw) amesema,

«تَرَكْتُ فِيكُمْ أَمْرَيْنِ لَنْ تَضِلُّوا مَا تَمَسَّكْتُمْ بِهِمَا كِتَابَ اللهِ وسُنَّةَ نَبِيِّهِ»

“Nimekuachieni vitu viwili mkishikamana navyo hamtapotea, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake.” (Imam Maalik katika Muwatta).

Waislamu kwa ujumla na maulamaa wao na kwa waandishi wa habari hasa, ni juu yao kuangalia masuala yote ya Waislamu kwa uoni wa uteremsho wa Wahyi. Na wachunguze kwa makini nususi za kisharia, huku wakinufaika kwa ukamilifu na utajiri wa urithi wa sheria za karne nyingi za Khilafah. Na wasafishe jamii za Waislamu kutokana na ushawishi mbaya wa falsafa ya Kigiriki, mtazamo wa Mustashrikin, Falsafa ya mantiki ya Wamagharibi, falsafa ya kirasilimali ya kuwaridhisha watu wengi zaidi, usasa uliopotoka na fikra ya kuangalia zaidi uhuru wa mwanadamu. Ni msimamo huu pekee wa kuzawadiwa ndio utaochangia kuleta mazingira imara kuelekea katika mabadiliko yanayohitajiwa katika Ulimwengu wa Kiislamu, kuirejesha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie utiifu wetu wote ili tuwe katika watu wa safu za mwanzo za utiifu, huku tukiepuka kuangukia katika madhambi kutokana na dharau na ukimya.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu