- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kwa nini Mahusiano na Syria Yanarekebishwa?
(Imetafsiriwa)
Mnamo mwezi Mei, kiongozi wa Syria anayezozana, Bashar al-Assad alizuru Saudi Arabia kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Nchi za Kiarabu. Haya yalikuwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia kwa al-Assad ambaye amekabiliwa na machafuko ya muda mrefu yaliyosababisha utawala wake kutengwa katika eneo hilo. Ziara yake nchini Saudi Arabia ni sehemu ya mchakato wa kuhalalishwa kwa jumla ambao umeifanya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuitambua tena Syria katika boma lake. Baada ya kuukashifu utawala wa Baath wa Syria kwa muda mrefu, baada ya mauaji, uchinjaji na uhamisho wa mamilioni ya watu wa Syria al-Assad unakaribishwa kwa mikono miwili. Hivyo, ni kwa nini Al-Assad sasa anakaribishwa tena?
Wakati Mapinduzi ya Kiarabu yalipokuja Syria mwaka 2011, mahusiano ya magharibi na Syria yalikuwa yanapitia awamu ya uchumba. Marekani ilikuwa inaandaa mazungumzo kwa siri kati ya Syria na 'Israel' ili kusuluhisha suala la Milima ya Golan. Syria ilikuwa inacheza dori changamfu katika kupenyeza vikundi vinavyopigana na jeshi la Marekani nchini Iraq na kupitisha ujasusi muhimu kwa Amerika. Bashar al-Assad, utawala wake na mkewe walikuwa wakionyeshwa kama wanamageuzi katika eneo hilo na walikuwa wakinyweshwa na kulishwa nchini Uingereza huko 10 Downing Street, huku Seneta wa Marekani John Kerry akifanya ziara za mara kwa mara jijini Damascus. Hilary Clinton aliweka msimamo wa Marekani kwa uwazi sana wakati maandamano yalipozuka kwa mara ya kwanza nchini Syria mwaka 2011: "Kuna wasiwasi mkubwa kuhusu kile kinachoendelea nchini Syria, na tunaisukuma kwa nguvu serikali ya Syria kutekeleza ahadi yake yenyewe iliyoielezwa kwa mageuzi. Ninachojua ni kwamba wangali wana fursa ya kuleta ajenda ya mageuzi. Hakuna aliyeamini kuwa Qaddafi angefanya hivyo. Watu wanaamini kuwa kuna njia inayowezekana ya kusonga mbele pamoja na Syria. Kwa hivyo tutaendelea kuungana na washirika wetu wote ili kuendelea kusisitiza sana hilo.” [1]
Wakati Mapinduzi ya Kiarabu yalipowasili nchini Syria hili lilileta changamoto kubwa kwa Marekani. Hapo awali Marekani iliamini kwamba Basher al-Assad angeweza kustahimili uasi huo na ilimpa maficho mingi kupitia Umoja wa Nchi za Kiarabu na misheni ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa ili kuzima ghasia hizo. Kwa Marekani, uasi huo ulikuwa wa watu wa Syria dhidi ya utawala, mafanikio yake hayakuwa kwa maslahi ya Marekani, kwa kweli ilikuwa tishio kwa usanifu wa Marekani katika eneo hilo baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Marekani ilishirikisha mataifa mengi ya eneo hilo ambayo katika sehemu mbalimbali za Syria wangeunga mkono makundi mbalimbali ya waasi. Hakuna taifa moja lililokuwepo katika maeneo mingi ya Syria. Marekani ilianzisha makongamano na mikutano iliyoanzia Vienna, Geneva hadi Riyadh. Kiini cha mikutano na mazungumzo yote kilikuwa ni upinzani kufanya mazungumzo na utawala wa al-Assad na kuunda uwezekano wa serikali ya mpito. Mialiko ambayo ilitumwa kwa ajili ya makongamano kama hayo mara zote ilikuwa na mipaka na ililengwa makundi machache ya upinzani yaliyounga mkono ajenda hii. Kujumuika kwa wanachama wa zamani wa serikali na kutengwa kwa vikundi vyenye ushawishi vinavyodai mabadiliko ya serikali kulionyesha kuwa mazungumzo yalikuwa kulinda serikali ya al-Assad na wale waliopinga ajenda hii walibandikwa kibandiko cha magaidi. Hili liliangaziwa na al Jazeera wakati huo: “Mwanzoni mwa mzozo, Marekani ilisimama hadharani kumpinga (Rais wa Syria) Bashar al-Assad. Lakini wakati huo huo waliendelea kutoa ahadi za uwongo kwa upinzani. Na sasa nafasi yao ya kweli iko wazi. Marekani haina msimamo dhidi ya Assad. Wanamkubali kwenye meza ya mazungumzo na wanamwona kuwa kiongozi.” [2]
Hili linazua swali, kwa nini Marekani haikupindua tu utawala wa al-Assad ambao haukupendwa na watu wengi na kuubadilisha na utawala unaokubalika zaidi na Marekani na watu wote? Ushawishi wa Amerika nchini Syria ulikuwa wa muda mrefu kutokana na uhusiano wake na utawala wa Baath. Huku katika maeneo kama vile Pakistan na Misri Marekani imepanua uhusiano wake na vyama vyengine vya kisiasa, taasisi, mashirika ya kiraia na watu binafsi katika suala la Syria Marekani kwa muda mrefu ilidumisha mahusiano kupitia utawala huo. Matokeo yake, Marekani haikuwa na mtu wa kuchukua nafasi ya serikali. Hii ndiyo sababu watunga sera wakuu wa Marekani waliendelea kusema wakati wa uasi kwamba utawala unahitaji kubakia, hata kama Bashar al-Assad angeondoka. Ingawa hakuna shaka kulikuwa na wengi ambao wangekuwa tayari kufanya kazi na Marekani nchini Syria, Marekani haikuona mtu yeyote ambaye angeweza kuchukua nafasi ya utawala. Matokeo yake, Marekani ilihakikisha utawala huo unadumishwa na sio kupinduliwa, licha ya taarifa zake za hadharani kinyume chake.
Kulikuwa na matukio mawili ambapo serikali ilikuwa karibu kuanguka. La kwanza kati ya haya lilikuwa mwaka wa 2013 wakati utawala ulipolemewa baada ya karibu miaka miwili ya kujaribu kukabiliana na machafuko kwa marefu na mapana ya nchi. Utawala huo ulikata tamaa ya kuiregesha kaskazini ya Syria kwa vile haikuwa na vikosi tena, kutokana na idadi ya walioasi ndani ya jeshi la kitaifa. Ni hapa ambapo kundi la wafungwa, ambao walikuwa katika gereza la Marekani nchini Iraq katika miaka ya 2000 walikusanyika pamoja na kuichukua Mosul katika mazingira ambayo bado yanachukuliwa kuwa ya kushukiwa. Walijiunda na kuwa ISIS na wakahamia kaskazini mwa Syria. Hii ilisaidia serikali ya Damascus kwani iliwalazimu vikundi vya waasi nchini Syria ambao walikuwa wakipanga kushambulia Damascus kuregea kutetea eneo ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wao.
Tukio la pili lilikuwa mwaka 2015 wakati utawala wa Damascus ulipochoka na kuishiwa na watu na nyenzo. Mambo yalikuwa mabaya sana, Bashar al Assad mnamo Juni 2015 alitoa hotuba huko Damascus ambapo alikiri kuwa alikuwa amepoteza nusu ya nchi na hakuweza kuiregesha. Hii ilikuwa wakati Urusi ilipoingilia kati kuvijenga vikosi vyake nchini. Marekani iliikashifu kwa maneno kuingia kwa Urusi, lakini ilifanya machache kuizuia, licha ya uwepo wake wa kijeshi katika eneo hilo. Kisha Marekani ilishirikiana na Urusi kwa kukubaliana juu ya itifaki ya anga na kushirikiana ujasusi. Matukio yote mawili yalishuhudia Marekani ima moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhakikisha kuwa utawala wa Damascus ulisalia madarakani.
Imarati, Saudi Arabia, Uturuki, Jordan na Qatar zilivipa silaha vikundi tofauti vya waasi na kuwalazimisha wote kujiunga na mazungumzo ya amani na utawala huo. Makundi ya waasi yaliyokataa kufanya hivyo yaliachwa kujihami yenyewe dhidi ya utawala, ISIS na mashambulizi ya anga ya Urusi. Kufikia mwaka wa 2020 huku nchi hiyo ikiwa imeharibiwa na takriban muongo mmoja wa vita na ikiwa na upinzani pekee katika Idlib, utawala huo umenusurika kwa usaidizi wa mataifa ya kikanda na dola kuu za kiulimwengu.
Imarati, Saudia na Jordan tangu 2021 zimekuwa zikitoa wito hadharani wa kuregea kwa Syria kwenye mashirika ya kikanda. Lakini hii ilikuwa baada ya Marekani kuifikia Syria mwishoni mwa 2020. Ikulu ya White House ilikubali mkutano wa Oktoba 2020, kati ya maafisa wawili wa Marekani huko Damascus na maafisa wa serikali. Kash Patel, afisa mkuu wa Rais Donald Trump wa kukabiliana na ugaidi katika Ikulu ya White House alihudhuria mkutano huo kama msaidizi mkuu wa White House. Patel alikiri jinsi mshirika mmoja wa Marekani ambaye hakutambulishwa katika eneo hilo alivyotoa msaada wa matibabu ya saratani kwa mke wa Rais Bashar Assad. Hivi majuzi ilifichuliwa na afisa mwandamizi wa kidiplomasia katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba Marekani imekuwa katika mazungumzo ya moja kwa moja na Syria kwa miaka mingi, mazungumzo ya hivi karibuni zaidi "yalifanyika katika mji mkuu wa Oman Muscat, 'mji wa mazungumzo ya siri' kati ya Washington na mataifa kadhaa ya Asia Magharibi.” Pia alisema kwamba "mikutano hiyo ilijumuisha takwimu za usalama kutoka nchi zote mbili na wawakilishi wa Wizara za kigeni." [3]
Marekani kwa mara nyingine tena inaukosoa hadharani utawala wa Damascus, wakati kwa siri imekuwa ikijihusisha na mazungumzo ya moja kwa moja na utawala huo. Kwa watawala wa Kiarabu utawala wa al-Assad umepata kitu ambacho wanaweza kukabiliana nacho wakati wowote. Katika Mashariki ya Kati, Lebanon imeporomoka, uchumi wa Misri unadorora, uchumi wa Iran uko katika hali mbaya na huko Algeria na Sudan tawala za zamani zinaendelea kupingwa na watu. Kwa kumleta Bashar al-Assad kutoka kwenye baridi wanapiga mpira hatua zake kubaki madarakani, jambo ambalo wote wanaweza kukumbana nalo siku moja.
Marekani kwa mara nyengine tena inaukashifu hadharani utawala wa Damascus, huku kisiri imekuwa ikijihusisha na mazungumzo ya moja kwa moja na utawala huo. Kwa watawala wa Kiarabu utawala wa al-Assad umepata kitu ambacho wanaweza kukabiliana nacho wakati wowote. Katika Mashariki ya Kati, Lebanon imeporomoka, uchumi wa Misri unadorora, uchumi wa Iran uko katika hali mbaya na nchini Algeria na Sudan tawala za zamani zinaendelea kupingwa na watu. Kwa kumleta Bashar al-Assad kutoka kwenye baridi wanaidhinisha hatua zake kubaki madarakani, jambo ambalo wote wanaweza kukumbana nalo siku moja.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan
[1] US Dept. of State, Hilary Clinton interview with Lucia Annunziata of "In Mezz'Ora," May 2011.
[2] The shifting lines in Syria | Features | Al Jazeera
[3] EXCLUSIVE: US and Syria holding secret talks in Oman (thecradle.co)