Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Bishara Njema ya Kurudi Khilafah Inatutaka Tufanye Matendo Mema ili Tupate Ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt)

(Imetafsiriwa)

Ahmed amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye huwasilisha maana hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) katika maneno yake mwenyewe (saw) kama sehemu ya Sunnah yake, ambaye hazungumzi isipokuwa yale aliyoteremshiwa (saw) kutoka kwa Mola wake, ametangaza, «تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِننْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًاا عَاضًّا فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّة» “Utume utakuwepo kwenu kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume, itakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu iwepo kisha ataiondoa apendapo kuiondoa. Kisha utakuwepo utawala wa kurithishana, utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha utakuwepo utawala wa utenzaji nguvu, utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” Baada ya maneno yake haya, kisha, akanyamaza (saw).

Katika zama za utawala wa kidhalimu katika Ulimwengu wa Kiislamu, ni chanzo cha matumaini na msukumo kwamba bushra (bishara njema) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) inaashiria kwamba hakika Khilafah itaregea. Zaidi ya hayo, Khilafah itakayoregea itakuwa na sifa makhsusi. Itakuwa kama Khilafah ya kwanza, iliyoanzishwa na Maswahaba wakubwa (ra) wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Khilafah kwa Njia ya Utume. Kwa hivyo, si katika utawala wa kurithishana, kwani Khilafah zilizo kuja baada ya Khulafa’a Rashidina. Sifa ya urithi ya utawala imeelezewa katika Hadith kuwa ni kuuma, kumaanisha kung'ang'ania utawala, kwa namna ambavyo nasaba hushikamana. Katika zama hizi, Khalifa alipokaribia kifo alimteua mrithi wake kutoka katika nasaba yake na angeomba apewe Bayah. Kisha Bayah ya uteuzi ingechukuliwa juu ya Khalifa huyo baada ya kifo cha Khalifa. Hivyo, tunayachukulia maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuwa ni bushra (bishara njema), yakizitoa nyoyo zetu kutokana na huzuni kutokana na hali ya kusikitisha ya Umma chini ya utawala dhalimu.

Hata hivyo, wakati huo huo, bishara njema ya Mtume (saw) haimaanishi kwamba tunaichukulie kama kisingizio cha kutotenda. Hapana, la hasha, kwani Hadith hiyo tukufu sio tu bishara njema, bali pia ni khabar (habari) kwa maana ya kitendo kwetu kukifanya. Vile vile Hadith hii ni sawa na Hadith, , «لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ، فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا، وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ» “Kwa yakini mtaikomboa Konstantinopoli. Amiri bora zaidi atakuwa Amiri wake na jeshi bora zaidi litakuwa jeshi lake.” [Ahmad.] Hapa pia, tunazo habari (khabar), katika muundo wa ombi la kutenda (Talab bil fa’il). Kwa hivyo, kwa karne nyingi, kila Muislamu alikuwa na shauku ya kushuhudia bishara njema lakini hakukubali kujiuzu kwa maafa, uvivu au kuridhika. Waislamu walikuwa na shauku ya kuwa na bishara njema ya Mtume (saw) itimie mikononi mwao. Kwa hiyo, watawala wa Kiislamu walifanya juhudi zao za kuwa Amiri bora, mtiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kutekeleza amri Zake (swt), na kuandaa jeshi bora zaidi, kuwatayarisha juu ya Uislamu na kuwapa silaha bora kabisa. Kisha Mwenyezi Mungu (swt) akampa Nasr (Ushindi) wake Sultan Muhammad al-Fatih, aliyeifungua Konstantinopoli.

Basi ni lipi liko juu yetu, enyi Waislamu, miaka mia moja ya Hijria tangu kuondolewa kwa Khilafah, katika kipindi cha mpito cha utawala wa kidhalimu, kabla ya kuregea Khilafah kwa Njia ya Utume? Ingawa tunatamani sana kuiona, je, hatupaswi kuchukua hatua ili kuifanikisha? Ni lazima tuchukue hatua kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah, kwani Hadith ya kuregea Khilafah kwa Njia ya Utume pia ni khabar kwa maana ya kitendo. Hivyo, tumeamrishwa pia kusimamisha Khilafah, tukitafuta kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa miongoni mwa waliokirimiwa kuisimamisha. Ni lazima tuwe Waislamu bora tunaoweza kuwa na kujizatiti na elimu ya Uislamu ipasavyo, ili tuwe wenye kustahiki ubora huo wa juu wa Khilafah. Hatunyenyekei tu kwa hali yetu, tukifanya Dua peke yake, bila ya kutenda kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt). Hakika uzito wa maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wapasa kuzingatiwa, «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ الْمُنْكَرِ أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْ عِنْدِهِ ثُمَّ لَتَدْعُنَّهُ فَلَا يَسْتَجِيبُ لَكُمْ»  “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mokononi mwake, hamtaacha kuamrisha mema na hamtaacha kukataza maovu isipokuwa Mwenyezi Mungu atakuteremshieni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba dua wala hatakujibuni.” [Ahmad] Basi ikiwa tutatenda, ni matendo gani yanayotakiwa kwetu, sawa yawe ni matendo ya moyo au matendo ya viungo?

Ama matendo ya moyo, Iman yetu ni kwamba Nasr (Ushindi) inatoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake, asiye na mshirika. Baada ya makafiri kutushinda waliposhirikiana na wasaliti kutoka miongoni mwa viongozi wa Waarabu na Waturuki kuivunja Khilafah, ushindi wetu juu yao, kupitia kuiregesha Khilafah, unategemea Nasr kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[وَمَا جَعَلَهُ اللَّهُ إِلاَّ بُشْرَى وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ وَمَا النَّصْرُ إِلاَّ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

“Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe. Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.” [Surah al-Anfaal 8:10]. Ibn Kathir amesherehesha katika Tafsir yake, وإلا فهو تعالى قادر على نصركم على أعدائكم  “Hakuna yeyote isipokuwa Yeye mwenye uwezo wa kutoa ushindi kwenu dhidi ya maadui zenu.” Imam at-Tabari amesherehesha, وما تنصرون على عدوكم، أيها المؤمنون، إلا أن ينصركم الله عليهم, لا بشدة بأسكم وقواكم, بل بنصر الله لكم, لأن ذلك بيده وإليه  “Hamtakuwa na ushindi juu ya maadui zenu, enyi Waumini, isipokuwa pale Mwenyezi Mungu (swt) atakapokupeni ushindi juu ya maadui zenu, sio kwa nguvu, uwezo na utawala wenu, bali kwa kupewa kwenu ushindi na Mwenyezi Mungu (swt), kwani Ushindi uko Mikononi Mwake na Kwake Yeye.” Hakika, ingawa makafiri wanapiga vita kurudi kwa Uislamu, kwa njia ya moja kwa moja au kupitia vibaraka wao katika Ulimwengu wa Kiislamu, ni Mwenyezi Mungu (swt) Pekee ambaye atatupa ushindi juu yao.

Imani inatulazimisha kumtii Mwenyezi Mungu (swt), kujiepusha na madhambi ambayo Yeye (swt) ametukataza na kutekeleza majukumu ambayo Yeye (swt) ametuamrisha, tunapotafuta Nusra Yake,

[وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ]

“Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.” [Surah Ar-Rum 30:47] Hakika Mwenyezi Mungu (swt) ametuahidi kuwa ni juu yake (swt) kutupa Ushindi pindi tutakapoitikia maamrisho Yake (swt). Kuhusiana na Aya hii, Ibn Abi Hatim amenakili kuwa Abu Ad-Darda' Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema, “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema, «مَا مِنِ امْرِىءٍ مُسْلِمٍ يَرُدُّ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ إِلَّا كَانَ حَقًّا عَلَى اللهِ أَنْ يَرُدَّ عَنْهُ نَارَ جَهَنَّمَ يَوْمَ الْقِيَامَة»  “Hakuna Muislamu yeyote atakayeihami heshima ya nduguye isipokuwa itakuwa ni haki kwa Mwenyezi Mungu kumhami kutokana na moto wa Jahannam Siku ya Kiyama.” Kisha yeye (saw) akasoma Aya hii,

[وَكَانَ حَقّاً عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنينَ]

“Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.” Imam at-Tabari amehserehesha katika Tafsir yake kwamba hapa Mwenyezi Mungu (swt) anasema, ونجَّينا الذين آمنوا بالله وصدّقوا رسله إذ جاءهم بأسنا، وكذلك نفعل بك وبمن آمن بك من قومك وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنا نَصْرُ المُؤْمِنينَ على الكافرين، ونحن ناصروك ومن آمن بك على مَن كفر بك ومظفروك بهم  “Na tuliwaokoa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu (swt) na kuwaamini Mitume wake (as) ilipowajia nguvu zetu. Sisi tunakufanyia vivyo hivyo wewe (Ewe Muhammad (saw)  na kila anayekuamini katika watu wako,

[وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنا نَصْرُ المُؤْمِنينَ]

“Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini” juu ya makafiri. Tutakupa wewe na wale waliokuamini Ushindi juu ya wale waliokufuru na kukupa ushindi juu yao.”

Imani inatulazimisha kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), ikiwa hatutaki kupoteza nguvu zetu katika njia yetu ya kupata Ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَٰزَعُواْ فَتَفۡشَلُواْ وَتَذۡهَبَ رِيحُكُمۡ]

“Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu.” [Surah al-Anfaal 8:46]. Imam at-Tabari katika tafsir amesherehesha, kwamba Mwenyezi Mungu (swt) hapa anasema,  أطيعوا، أيها المؤمنون، ربَّكم ورسوله فيما أمركم به ونهاكم عنه, ولا تخالفوهما في شيء  “Mtiini, enyi waumini, Mola wenu na Mtume Wake (saw), katika yale waliyokuamrisheni na yale waliyokukatazeni na msende kinyume na hayo katika jambo lolote.”  Imam Qurtubi amesherehesha katika Tafsir yake ريحكم أي قوتكم ونصركم  “Uwezo wenu ndio nguvu yenu na ushindi wenu.” Kwa hivyo, ikiwa tunatafuta ushindi, tusizozane na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (swt), na kuingia katika maasiya (معصية). Hatuwezi kupata Nasr, ikiwa tutakubali kuzozana na Mwenyezi Mungu (swt), kupitia utabikishaji wa sheria za maasi katika nchi zetu, iwe ni riba, kuwatoza kodi masikini na wenye madeni, kuzigawanya Nchi za Kiislamu au kufanya miungano na maadui wa Mwenyezi Mungu (swt).

Ikiwa hatutaki kuangamia, ni lazima Mawaalaah (Utiifu) wetu uwe kwa Mwenyezi Mungu (swt). Ikiwa tunataka Mwenyezi Mungu atunusuru, ni lazima tusiwe watiifu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (swt) na tusichukue njia isiyokuwa yake (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ بِطَانَةٗ مِّن دُونِكُمۡ لَا يَأۡلُونَكُمۡ خَبَالٗا وَدُّواْ مَا عَنِتُّمۡ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni.” [Surah Aali Imran 3:118]. Imam Qurtubi amesherehesha katika Tafsir yake, نهى الله عز وجل المؤمنين بهذه الآية أن يتخذوا من الكفار واليهود وأهل الأهواء دخلاء وولجاء يفاوضونهم في الآراء ، ويسندون إليهم أمورهم  “Mwenyezi Mungu Azza wa Jal amewaharamisha waumini kwa ayah hii kutokana na kuwafanya makafiri, Mayahudi na watu wa hawaa na matamanio, kama wandani na wasaidizi, ambao wanashauriana nao juu ya rai na kuwategemea katika mambo yao.” Basi vipi tutatafuta Ushindi ikiwa sisi ni watiifu na wenye ukaribu na makafiri, tukifanya mafungamano nao, tukijadiliana nao juu ya maoni yetu badala ya kuregelea Qur'an na Sunnah, tukifanya mapatano na miungano nao pamoja na kuwashirikisha siri za kijeshi, licha ya uadui wao na ukafiri wao? Vipi?

Wakati tukijitahidi kwa ajili ya Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt), ni lazima tujitayarishe kwa ajili ya dhiki na mateso ya watu ili kupata Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَأۡتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُمۖ مَّسَّتۡهُمُ ٱلۡبَأۡسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلۡزِلُواْ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصۡرُ ٱللَّهِۗ أَلَآ إِنَّ نَصۡرَ ٱللَّهِ قَرِيب]

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” [Surah Al-Baqarah 2:214]. Hatuwezi kuingia kwenye njia ya Haki kwa kukaa kimya huku tukitunza familia na kazi zetu pekee, kutokana na kuchukia kwetu dhiki kutoka kwa watawala madhalimu. Hatuwezi kutafuta ushindi, ikiwa hatutajiandaa kukabiliana na shida, kwa kuimarisha Taqwa, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutafuta elimu ya Uislamu, kujizamisha ndani ya Quran, kumwendea Mwenyezi Mungu (swt) katika swala za usiku na saumu kwa ajili Yake miongoni mwa matendo mengi mema.

Ama kuharakisha kwetu ushindi, kwa kuuliza lini Khilafah itakuja, haraka hii sio kasoro wala Haramu kwa sababu mwanadamu ana pupa kwa maumbile yake,

[وَيَدۡعُ ٱلۡإِنسَٰنُ بِٱلشَّرِّ دُعَآءَهُۥ بِٱلۡخَيۡرِۖ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ عَجُولٗا]

“Na mwanaadamu huomba shari kama vile aombavyo kheri, kwani mwanaadamu ni mwenye pupa.” [Surah Al-Isra’a 17:11]. Hata hivyo, kinachotufanya tuingie katika dhambi, tukichochea ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) juu yetu wenyewe, ni kughafilika kwetu kwa matendo yanayotakiwa kuleta mabadiliko katika jamii. Kwa hivyo hebu haraka yetu na isitusukume katika kukata tamaa, kukosa matumaini na kufadhaika. Kwa hiyo ni lazima tuwe tunausoma Uislamu katika Halaqah, kama Maswahaba (ra) walivyofanya katika Dar al-Arqam. Ni lazima tuwe tunafanya kazi pamoja katika kutlah (muundo) kama Maswahaba (ra) walivyofanya, sio kama watu binafsi binafsi. Ni lazima tuwe tunakutana na watu mmoja mmoja na kwa pamoja kama Maswahaba (ra) walivyofanya. Ni lazima tuwe tunatangaza Haki kwa uwazi katika medani ya maisha, kama Maswahaba (ra) walivyofanya. Na kwa sisi ambao ni miongoni mwa watu wenye nguvu, silaha na vita, ni lazima tuwe kama walivyokuwa wakuu wa Answaar (ra), tunyoshe Nusrah yetu ili hukmu ya Uislamu iregee tena. Basi hata mmoja wetu asichoke au kulegea katika kufuata Njia iliyobarikiwa ya Mtume (saw) ya kuleta mabadiliko katika jamii, kurudi nyuma katika kujitenga na kukata tamaa. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atutie nguvu katika matendo yetu mema na kujitolea kwa Dini yake, tusije tukapotea gizani!

Hapo ndipo Ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt) utakuja, baada ya kupatikana mabadiliko ya mwanadamu, ambayo yanafuatiwa na mabadiliko ya kiwahyi na kupatikana ushindi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِهِمۡ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Surah Ar-Ra’ad 13:11]. Kwa hiyo pindi watu wanapobadilika kutoka katika Iman kwenda katika ukafiri, kutoka kwenye utiifu na kwenda katika uasi, au kutoka katika kushukuru neema za Mwenyezi Mungu (swt) hadi kufuru, basi Mwenyezi Mungu (swt) huwanyima kila kheri juu yao. Vile vile ikiwa waja watabadilisha kila kilichomo ndani ya nafsi zao ili wageuke na kumtii Mwenyezi Mungu (swt), Mwenyezi Mungu (swt) atayabadilisha yote yaliyo juu yao, kutoka kwenye taabu hadi kwenye wema, furaha, neema na rehema. Basi tujitahidi katika mambo ya kheri, enyi Waislamu, tujitahidi.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّههُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُببَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَااسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An-Noor 24:55]. Ibn Kathir amesherehesha katika Tafsir yake, هذا وعد من الله لرسوله صلى الله عليه وسلم . بأنه سيجعل أمته خلفاء الأرض ، أي : أئمة الناس والولاة عليهم ، وبهم تصلح البلاد ، وتخضع لهم العباد ، وليبدلن بعد خوفهم من الناس أمنا وحكما فيهم  “hii ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Mtume wake (saw) ya kwamba ataufanya Ummah wake kuwa makhalifa duniani, yaani, watakuwa viongozi na watawala wa wanadamu, ambao kupitia kwao atautengeneza ulimwengu na ambao kwao watu watasalimu amri, ili wawe na badali ya amani na usalama baada ya khofu yao.” Basi tujitahidi enyi Waislamu katika matendo mema, ili Mwenyezi Mungu (swt) aurudishe Umma wa Muhammad (saw) mahali pake, wawe watawala juu ya wanadamu.

Kwa hiyo, hebu na tutembee kuueneza Uislamu kote duniani kuanze tena, kutoka pale ambapo Khilafah iliiachua miaka mia moja ya Hijria ya Kiislamu iliyopita, hadi kufikia hatua ya Uislamu kuenea kote duniani. Thauban amepokea kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema, «إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَاا زُوِيَ لِي مِنْهَا وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الأَحْمَرَ وَالأَبْيَضَ وَإِنِّي سَأَلْتُ رَببِّي لأُمَّتِي أَنْ لاَ يُهْلِكَهَا بِسَنَةٍ بِععَامَّةٍ وَأَنْ لاَ يُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُوًّا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ وَإِنَّ رَبِّي قَالَ يَا مُحَمَّدُ إإِنِّي إِذَا قَضَيْتُ قَضَاءً فَإِنَّهُ لاَ يُرَدُّ وَإِنِّي أَعْطَيْتُكَ لأُمَّتِكَ أَنْ لاَ أُهْلِكَهُمْ بِسَنَةٍ بِعَامَّةٍ وَأَنْ لاَ أُسَسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُوًّا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ يَسْتَبِيحُ بَيْضَتَهُمْ وَلَوِ اجْتَمَعَ عَلَيْهِمْ مَنْ بِأَقْطَارِهَا»  “Mwenyezi Mungu alinikunjulia ardhi kwa ajili yangu. Basi nikaziona ncha zake za mashariki na magharibi. Na ufalme wa Ummah wangu ungefika ncha zile ambazo zimesogezwa karibu yangu na nimepewa hazina nyekundu na nyeupe na nikamwomba Mola wangu Mlezi kwa Ummah wangu kwamba usiangamizwe kwa sababu ya njaa, wala usisalitiwe juu yake adui asiye miongoni mwao na kuwaangamiza, na Mola wangu Mlezi akasema: Ewe Muhammad, pindi ninapofanya uamuzi, hakuna wa kuubadilisha. Nimekupa kwa ajili ya Ummah wako kwamba kamwe sitauangamiza kwa njaa na sitausaliti na adui ambaye hatakuwa miongoni mwao awaangamize, hata kama watu wote kutoka sehemu mbali mbali za dunia watakusanyika (kwa kusudi hili)” [Muslim]. Tunaomba Umma wa Kiislamu uyaone yale ambayo Bwana Muhammad (saw) ametupa kwayo bishara njema!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu