Jumatano, 09 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kilio kwa Wabebaji Dawah
“Mulikuwa wapi Muda wote huu?!”
(Imetafsiriwa)

Katika ghururi ya maisha na kutojali kwa jamii, neno moja pekee linabaki kuwa na uwezo wa kutikisa milima, kuchochea dhamiri, na kuamsha ari ya uwajibikaji katika nyoyo za Umma wa Uislamu. Ni neno lililotoka katika vinywa vya wale ambao miili yao ilichakaa kwa mateso na ambao fremu zao zilisagwa kwa dhulma ndani ya magereza ya madhalimu: “Mulikuwa wapi muda wote huu?!” Ilisemwa na mmoja wa wale walioachiliwa huru kutoka magereza ya mtoro Bashar al-Assad, wale walioonja majanga na ambao miaka yao ilizimwa gerezani; alipokutana na baadhi ya watu waliokuwa wameachiliwa huru, hakuuliza kuhusu idadi ya miaka gerezani, badala yake alipiga kelele usoni mwake: “Mulikuwa wapi, mulikuwa wapi muda wote huu? Kwa nini hamkutuachilia huru wakati tulipokuwa tunazikwa tukiwa hai?”

Maneno haya yalinisuta sana nilipohisi mapungufu yangu kwa wote waliodhulumiwa duniani. Uislamu ulikuja kama rehma kwa watu kuwatoa katika ibada ya waja na kuwapeleka katika ibada ya Mola wa waja. Hapa hakuna kutoroka kutoka kwa hisabu, hakuna nafasi ya kuomba msamaha, hakuna njia ya kutoka kwa lawama. Kwa hivyo shida iko wapi?

Na hapa narudia neno lile lile mbele ya wabebaji ulinganizi ambao wanabeba suluhisho msingi la matatizo ya Ummah, hasa pale nilipojua maelezo ya kina ya mradi wa mwamko wanaoubeba. Nilimwambia mmoja wa wabebaji ulinganisi: “Umekuwa wapi muda huu wote?”

Na sasa nimeapa kubeba hamu ya kuregea kwa Uislamu kwenye uhalisia wa maisha na kufanya kazi pamoja na wale wanaofanyia kazi jukumu hili kubwa. Nauliza: Je, tumefikisha Ujumbe kama tulivyopaswa? Je, tumewafikia waliodhulumiwa? Je, tumetia bidii katika kubeba Da‘wah kama alivyotuamrisha Mwenyezi Mungu?

Hatubebi ulinganizi wa starehe, wala mradi finyo wa mageuzi. Tunabeba kadhia ya uhai au kifo. Tunabeba ujumbe kamili wa Uislamu. Tumebeba tiba kwa wanadamu. Tunabeba ahadi ya Mwenyezi Mungu ya Khilafah, na tunabeba ukombozi wa watu kutoka kwenye moto wa dhulma, ujinga na utumwa.

Basi mwenye kuzembea katika kufikisha amepuuza amana, na anayechagua mtu wa kumlingania na kuwaacha wanyonge basi ameufanyia khiyana utakatifu wa Ujumbe.

Hebu fikiria waliofungwa kwa miaka mingi, wafungwa wa ujinga, wafungwa wa vyombo vya habari vya upotoshaji, wafungwa wa thaqafa ya Kimagharibi, wafungwa wa tawala dhalimu, wafungwa wa mahitaji ya kila siku ambayo yamewachosha hata wasizingatie tena dini yao, wafungwa wa ubabaishaji na kufuata michezo, watu mashuhuri na matamanio...

Pindi Da‘wah itakapowafikia hawatauliza isipokuwa: “Mbona ulinganisi wenu haukutufikia?!” Ndio, watu wengi leo wamefungwa bila ya kuwa gerezani, na wote wanangojea mtu wa kubisha hodi kwenye milango yao na kuwaamsha, ili kuwaletea Uislamu kama alivyouteremsha Mwenyezi Mungu – sio Uislamu uliodogoshwa kwa ibada pekee, lakini Uislamu unaookoa ambao humkomboa mwanadamu kutoka kwa aina zote za utumwa, kusimamisha uadilifu, kueneza kheri, na kuangaza njia.

“Mulikuwa wapi muda wote huu?!” si neno tu, bali ni kofi kwa kila mlegevu, na tahadhari kwa kila mbebaji ulinganizi ambaye azma yake imedhoofika katikati ya uhalisia huu mbaya wa kutusukuma kusonga, kutoa ukweli, kubomoa kuta kati yetu na watu, kuipeleka nuru kwenye magereza yenye kina kirefu zaidi duniani, ili tuunganishe usiku na mchana; kwani aliyenyamaza kuhusu Da‘wah, aliyezembea katika kufikisha, ni mshirika katika kuendeleza kufingo cha watu.

Na mwenye kujua kuwa Uislamu una ukombozi, kisha asiufikishe, anabeba mzigo kwa kila aliyebaki kwenye giza lake.

Enyi wabebaji da’wah, inukeni, jifungeni azma yenu; musisubiri wakati mutapoulizwa “Mulikuwa wapi?” kuweni jibu kabla ya kuulizwa. Kuweni pale dhulma ilipo, pale ujinga ulipo, pale mateso yalipo; kwani kuna waja wa Mwenyezi Mungu wanaongoja sauti ya haki. Je, tutawaangusha? Wenye bidii miongoni mwenu huongeza bidii maradufu, na wanaokwenda polepole wataupata msafara. Ewe Mwenyezi Mungu, usitufanye kuwa miongoni mwa waliozembea.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Hussam al-Idrisi – Wilayah Yemen

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Sudan: Mfano Mwengine wa Utaifa Uliofeli

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu