Jumanne, 01 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Wanaozuru Kurasa zake kwa Mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wa Mwaka 1444 H Sawia na 2023 M
(Imetafsiriwa)

Kwa Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu... Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu ameutukuza kwa utiifu Wake...

Kwa wabebaji Da’wah ambao biashara wala uuzaji haviwashughulishi na kumkumbuka Mwenyezi Mungu...

Kwa waheshimiwa wanaozuru ukurasa wanaokuja kwa ajili ya kheri unayo beba ...

Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na wanaomfuata.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَنْ كَانَ مَرِيضاً أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ)

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.” [Al-Baqara 2:185]. Na Mtume (saw) amesema, kwa mujibu wa yale aliyopokewa na Al-Bukhari kutoka kwa Abu Salamah kutoka kwa Abu Huraira:

«مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَاناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»

Mwenye kufunga mwezi wa Ramadhan kwa imani ya kweli, na kutaraji kupata thawabu za Mwenyezi Mungu, basi husamehewa madhambi yake yote yaliyopita.” Ni mwezi wa ́ibaadah na maghfirah, na hoja za uongofu na upambanuzi (Furqan).

Kadhalika ni mwezi wa jihad na ufunguzi wa wazi ambayo ndani yake kuna Badr kubwa, na ndani yake ni kufunguliwa kwa Makka, ufunguzi mkubwa kabisa ambao ulikuwa ndio nukta kianzio kwa majeshi ya Waislamu walipobeba liwa (bendera) ya kheri hadi pembe zote za dunia... Na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba mwezi huu mtukufu uwe mwanzo wa kheri na baraka juu ya Waislamu, ili Khilafah Rashida irudi kwa mara nyengine, nayo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt).

(وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا)  

Mwenyezi Mungu amewaahidi walio muamini” [Al-Ma’iadah 5:9] na bishara njema ya Mtume wake (saw), hapo Uislamu na Waislamu watapata izza na ukafiri na makafiri watadhalilishwa.

(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ)  

Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Ar-Rum 30:4-5].

Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

1 Ramadhan 1444 H sawia na 23/03/2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu