Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Salamu kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wanaozuru Mitandao yake katika Siku Kuu Hii Iliyo Barikiwa ya Idd ul-Fitr 1441 H sawia na 2020 M

 (Imetafsiriwa)

Kwa Ummah wa Kiislamu kwa Jumla… Mwenyezi Mungu (swt) auruzuku ushindi juu ya maadui zake, na auruzuku kushikamana na neno la ucha Mungu (Kalimat ul Taqwa), unastahiki hili na watu wake… Kwa Wabebaji Dawah haswa… Mwenyezi Mungu aulete ushindi mikononi mwao, na awaruzuku nusra yake (swt) ili wasimamishe Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume… Kwa waheshimiwa wanaozuru kurasa kwa ajili ya kheri zinazo beba… ambapo wanatoa juhudi zao kutafuta haki na kuwaunga mkono watu wake… Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh, nawapa tahania kwa kuwasili kwa Idd ul-Fitr, na namuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba iwe ndio mwanzo wa kheri na baraka kwa Waislamu wote… ili Ummah wao urudi kuwa Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu, kupitia kusimamisha Dola yao, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; ili Mwenyezi Mungu awaondolee mateso yao na awaregeshee izza yao.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّـهِ ۚيَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖوَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

Na pia namuomba Mwenyezi Mungu (swt) ayaondoe mateso ya masaibu ya janga la maambukizi kutoka kwa Waislamu wote, na kwamba huu utakuwa ndio mwanzo wa ushindi wazi na ufunguzi, hakika hili ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kulitimiza.

Hatimaye, pokeeni salamu zangu na dua za kheri kwenu, na namuomba Al-Qawi Al-Aziz (Mwenye nguvu na uwezo), aujaaliye mwezi huu mtukufu uwe ndio mwezi wa mwisho ulio na baraka kuwafikia Waislamu huku kukiwa hakuna Dola inayo leta izza kwa Uislamu na Waislamu, na Mwenyezi Mungu ni Al-Aziz (Muweza) na Al-Hakim (Mwingi wa hekima).

Wa Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Siku ya Idd ul-Fitr, 1 Shawwal 1441 H

Ndugu yenu

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah           23/5/2020 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 24 Mei 2020 02:32

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu