Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vidokezo kutoka katika Kumbukumbu za Gerezani na Sharafu ya Uswahiba wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Sheikh Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

Jarida la Al-Waie lilipokea baadhi ya kumbukumbu za ndugu muheshimiwa, Salim al-Amr.  Tunapeperusha baadhi yake kwa kuwa ndani yake muna mafunzo na manufaa, insha'Allah kwa wale ambao watazingatia. Tunatambua na kutoa shukrani kwa Kaka Salim kwa kumbukumbu hizi zilizojaa majonzi na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie kuyafikia hayo na kwamba Yeye amlinde kutokana na maovu yote.

Kumbukumbu za Gerezani na Sharafu ya Uswahiba (6)

Nilikuwa nikimuuliza Abu Yasin (Sheikh ‘Ata) kuhusu sababu ya kutetemeka kwake ambako kulikuwa kumeathiri sehemu ya mwili wake wakati alipokuwa anatuongoza katika swala. Nikagundua kwamba ilitokana na kuteswa alikopitia ndani ya jela za vitengo vya kijasusi ndani ya Jordan, Libya na Iraq – kuchomwa kwa umeme na aina nyingine za mateso. Nakumbuka akiniambia kwamba Shabab waliteswa katika jela hizo kiasi kwamba walifungwa katika mitungi ya gesi ili waweze kuzunguka baina yao wakati wa nyakati za baridi kali ndani ya vyumba vya mateso huku viboko vikiwachapa kutoka kila upande. Hapa nitatosheka kwa kutaja baadhi ya ushahuda kuhusu Shabab wa Hizb ut Tahrir ambao niliwasikia kutoka ndugu (wasiokuwa Hizb) ambao tuliowajua tangu tulipokuwa ndani na nje ya jela.

1. Mwalimu wa Azhar, Sheikh Ahmad al-Farkh (Abu al-Amin), mkaazi wa al-Karak, Jordan. Alifariki mnamo 2006 baada ya kuishi na kufikia zaidi ya miaka 80. Nilimuuliza kuhusu fikra za Hizb. Alisema, "Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha mimi kupitia Hizb ut Tahrir kuona kipimo cha wazi baina ya ukweli na urongo, Ewe Salim. Naapa kwamba Hizb ut Tahrir iko katika Haqq." Akanisimulia hadithi kuhusu mkomunisti mmoja ndani ya Anabta (Tulkarm, Palestina) ambaye alikuwa akijadiliana mara kwa mara na Shabab. Alikuwa na binti aliyeheshimiwa ambaye wengi miongoni mwa rafiki zake ndani ya chama cha Kikomunisti walimtaka kumuoa lakini alikataa. Lakini mmoja katika Shabab wa Hizb ut Tahrir ambaye walikuwa na mzozo wa kimfumo alipomtaka amuoe, alikubali papo hapo. Na wenzake walipomuuliza, "Kwa nini ulikubali kumuozesha binti yako mtu wa Tahriri ambaye mtakuwa mnazozana mara kwa mara na hakubaliani nasi, badala yetu sisi ambao tunatoka chama kimoja nawe (chama cha kikomunisti)?! Jibu lake lilikuwa, "Wao watamtunza na kumuheshimu, nyinyi hamtofanya hivyo." 

Aliniambia siku moja kwamba mmoja kati ya ndugu wanaotoka Anabta waliokuwa wanaichukia Hizb aliamua siku moja kwamba watakutana na Sheikh Taqiuddin an-Nabahani kwa njia yoyote ile ili kujadiliana naye kuhusu fikra zake. Alifika Lebanon kwa njia ya Shabab na alibakia huko kwa muda chini ya uwenyeji wa Sheikh Taqi. Aliporudi kutoka Lebanon aliulizwa kuhusu Sheikh naye akasema, "Nitafupisha yale niliyo yashuhudia kuhusu mwanamume huyu kwa kifupi kwa kusema kwamba lau Qur'an haikuteremshwa kwa Muhammad (saw), ningelisema kwamba imeteremshwa kwake yeye."

Sheikh Ahmad al-Farkh (RahimahuAllah), mwanachuoni mkubwa. Wote waliomjua miongoni mwa watu wa al-Karak wanathibitisha tabia na elimu yake. Shabab walidumu kuwa na mahusiano naye mpaka pale alipoamua kujiunga na Hizb siku tatu tu kabla kufariki kwake. 

2. Mhandisi na mshairi maarufu, Dkt Ayman al-‘Atum, swahibu wangu gerezani. Yafuatayo ni yale aliyoyaandika kuhusu Shabab wa Hizb katika kitabu chake, Enyi Maswahaba mlioko Gerezani [YaSahibay al-Sijn] katika ukurasa wa 192-197:

"Katika chumba na.12 na kisha kulikuwepo vyumba viwili vinavyoangalia walikaa Shabab wa Hizb ut Tahrir. Walikuwa takribani wafungwa kumi. Niliwaendea kama mgeni kutokana na kufanana kwa kesi zetu ambazo tulikuwa tunatuhumiwa kwa 'kurefusha ulimi' (maanake ni kupaza sauti dhidi ya utawala). Nilipowafikia, kiongozi wa chumba, Walid alinikaribisha. Walid alikuwa mwanamume katika miaka yake ya mwisho ya thelathini. Alikuwa na ndevu ndefu na sauti ya nguvu na kali. Tabasamu lake daima lilikuwa haliondoki usoni mwake. Upande wa juu kushotoni mwa kifua chake ulielekea kidogo kulia anapokuwa anatembea kama ambaye anaonekana alikuwa anaringa au anacheza densi aina fulani.

Sheikh ‘Ata, kiongozi wa Hizb ut Tahrir ndani ya Jordan, alikuwa mmoja wa wafungwa kumi. Alikuwa mwanamume anaye heshimiwa na kupewa hadhi akiwa katika miaka ya hamsini, mwenye kichwa cha kijivu, maneno machache, mcheshi, macho ya samawati, kidevu cheupe chenye urefu wa wastani kinachozunguka uso wake. Alikuwa anauungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wafungwa wa chama chake, ambao walikuwa tayari kumtumikia, kutekeleza maagizo yake na kumsikiza kwa makini kwa kila mnong'ono unaotoka kwake. Na kwani nini isiwe hivyo, ilhali yeye alikuwa ndiye kiongozi wa Hizb ut Tahrir sio tu kwa hawa kumi bali kwa kila mwanachama wa Hizb ndani ya Jordan yote na hata Palestina, na huenda –siku moja akawa kiongozi wake katika ngazi ya kiulimwengu.

Walid aliniandalia kitanda chenye hadhi. Hizb ut Tahrir ilikuwa inawathamini wafungwa mfano wa kesi yangu (kuzungumza haqq) na walisikia kuhusu msimamo wangu na mashairi yangu. Hivyo basi, Walid kama kiongozi wa chumba aliniandalia kitanda cha hadhi kwa kuniwekea tandiko jipya na ziada ya mashiti. Na pia kuengwa katika cheo kwa kuwa karibu na kitanda cha Sheikh Ata.

Sheikh Ata alikuwa mwanamume ambaye aliweza kutekeleza kivitendo na kudhihirisha kikweli fikra za Hizb ut Tahrir. Lengo kuu na msingi ambalo linafanyiwa kazi na Hizb ni Khilafah. Wanafungamanisha kila wanalolifanya, kuliendea mbio na kutaabika kwa njia ya kufaulisha lengo hilo nalo ni kusimamisha Khilafah ya Kiislamu juu ya Ardhi. Ama kuhusu vipi, wapi, lini, kwa njia gani, kwa kipindi gani…kila mwanachama wa Hizb alikuwa na majibu ya maswali haya.

Aghalabu huwa ni kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hurudiwa katika ndimi zao katika mijadala yao

((وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آَمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ))

"Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada  ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu." [An-Nur: 55]

Walitosheka na ahadi hiyo ya Mwenyezi Mungu ndani ya ayah hii na hutaja ayah hiyo pamoja na ayah nyingine,

((فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا يُوقِنُون))

"Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala wasikupaparishe hao wasio kuwa na yakini." [Ar-Rum: 60]

Sheikh Ata alikuwa akitoa kila wiki masomo matatu ya tafsiri ya Qur'an na matatu ya lugha ya Kiarabu. Hivyo basi, wiki ya wafungwa wa Hizb ut Tahrir ilikuwa imegawanywa katika siku mbili: siku moja ya tafsir iliyofuatiwa na siku ya lugha. Ata kwa kujua kuwa mimi ni mshairi alikuwa akinishajiisha zaidi kuliko wengine kuhudhuria masomo haya, kuchangia na kuchanganyika nao na nilifanya hivyo. Na sijasahau mpaka wa leo maelezo yake kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu,

 ((هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آَيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ الْابْتِغَاءَ فِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آَمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ))

"Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili." [Aal-e-Imran: 7]

Sheikh alitumia muda mwingi katika kiunganishi 'waw' (na) ndani ya "waw al-rasikhuna fi al-'ilm" (na wale wenye ilimu) kuhusiana na ima ilikuwa ni 'waw' ya kujumuisha ('atf) au ni 'waw' kianzishi (isti'naf). Suala hili limejadiliwa kwa urefu katika ufafanuzi na utaalamu wa lugha. Sheikh kwanza aliwasilisha kwa urefu maoni tofauti tofauti kuhusiana na suala hili na kisha akaelezea msimamo wake ambao ulikwenda kupinga jumla ya misimamo mingi. Msimamo wa wafafanuzi wengi ni kwamba 'waw' iliyotumika ni 'waw' ya kianzishi lakini yeye alikuwa na msimamo kwamba ni 'waw' ya kujumuisha. 

Wanafunzi wa masomo kutoka Hizb ut Tahrir walikuwa wakibeba nakala za Qur'an na sehemu za kuandika na walikuwa wakiandika kile ambacho Sheikh amefunguliwa na Mwenyezi Mungu katika ilimu. Nilijiona mwenyewe nikiwa katika uandishi wa Sheikh, sehemu tatu za kuandika zilikuwa zimejaa tafsir ya surat al-Baqarah. Sehemu hizi za kuandika zilikuwa zinasambaa baina ya wanafunzi wa Shabab kama ambaye zilikuwa ni hazina yenye thamani. Walitaka kuzilinda zisije zikaharibika au kupotea. Mmoja wao alikuwa akizihifadhi karibu na kifua chake wakati anazisoma. Katika kufikisha amana, lazima nitaje kwamba nilimuona Sheikh katika masomo hayo akiwa makini na jasiri katika kufasiri aya na yale yaliyokuwemo katika hukmu za kisheria na sehemu zilizokuwa na tafsir yake zilikuwa na mng'aro usiokuwa kawaida. Wanafunzi walikuwa wakihamishiana miongoni mwao sawa na sonara anavyohamisha vito na lulu.

Sheikh alianza kuandika tafsir ya Qur'an akiwa gerezani mpaka pale ilipopelekea kujumuishwa kwa sehemu hizo tatu za kuandika. Wakati huo aliendelea katika mpangilio wake. Sijui ikiwa leo ima amemaliza tafsir ya Qur'an au ima kazi zake za kuiongoza Hizb ut Tahrir zimemzuia yeye kutofanya hivyo.

Ama kuhusu masomo ya lugha ya Kiarabu, nakumbuka masomo niliyohudhuria ambamo Sheikh alielezea 'majaz' na mahusiano yake tofauti tofauti (maanake halisi). Nakumbuka yeye kutaja aya ya Mwenyezi Mungu (swt)

As for the lessons in the Arabic language, I still recall the lessons I attended in which the

((أَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌ بِقَدَرِهَا فَاحْتَمَلَ السَّيْلُ زَبَدًا رَابِيًا))

"Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake." [Ar-Rad: 17]; na kuielezea kwamba, "Kihalisia hatusemi 'bonde lilitiririka,' tunasema 'maji ndani ya bonde yalitiririka.' Haya ni matumizi ya majaz. Ama kuhusu kuhusiana kwake, ni mahusiano kati ya mabonde na maji, huku mabonde yakiwa ndiyo sehemu ambapo maji yanatiririkia; kwa hiyo iliyoko ni mfano wa majaz isiyokuwa ya moja kwa moja [majazmursal] ambayo kuhusiana kwake ni kwa sehemu."

Sheikh alikuwa akimpa kila mmoja aliyehudhuria somo kazi ya kukamilisha kwa somo lijalo. Kwa mfano, alikuwa akiwaambia, "Tafuteni tofauti ya mahusiano ya majaz kutoka katika surat Aal-e-Imran," au "Vueni aina tofauti tofauti (kilugha) za kufuta kutoka katika surat al-Furqan na hakikisheni misingi na aina zake." Masomo yake yalikuwa yakiitikiwa pakubwa na maingiliano ya watu binafsi kutoka chama chake, miongoni mwao walikuwa wakubwa kwa wadogo, wasomi na wasiokuwa wasomi, daktari na mwalimu.

Ushirikiano, twaa kwa kiongozi na mfano wake zilikuwa sifa zinazojitokeza za kundi la wafungwa hao ambazo nimeshuhudia kwa kuishi miongoni mwao. Na walikuwa majasiri katika kufikisha mitazamo yao. Nakumbuka mmoja wao kuwa mkali katika mijadala na maafisa wa kijeshi, kwa kutodhibiti ulimi wake dhidi ya utawala uliokuwa uongozini nchini humo. Afisaa huyo kwa haraka alipeleka malalamishi rasmi dhidi yake na kupelekea kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi na kuhukumiwa miezi sita gerezani ikiwa ni nyongeza kwa miaka miwili ambayo tayari walikuwa wamehukumiwa. Hivyo basi kuhukumiwa gerezani ilhali tayari alikuwa yumo gerezani!

Kutokana na hilo, alihesabiwa na wafungwa wenziwe kwa kufanyiwa mzaza kwa yale yaliyomtokea kwa kumwambia, "Wewe kubakia hapa ni bora. Kwani huwezi kudhibiti ulimi wako hata kwa sekunde kwa ajili yako na chama chako. Daima unazungumza." Naye akawajibu kwa jibu zito zaidi kwa kuwalaumu kwa kuwa waoga na madhaifu, akiwaambia kwamba wanaogopa hata vivuli vyao wenyewe na wamefikia hali mpaka hawawezi kupaza sauti za ukweli na badala yake wanataabika. Mara kwa mara akiwarudia, "Ukweli unawataka wanaume na sio watu wote ni wanaume." 

Hizb ut Tahrir iliamini – na inaendelea kuamini hivyo –kwamba mabadiliko ya polepole ni kupoteza juhudi na kwamba mtu anatakiwa kuanza juu kabisa ya piramidi na sio katika msingi wake, na kwamba mtu lazima akate kichwa cha nyoka ili kusitisha madhara yake mwanzo na mwisho. Ama kuhusu njia ya kutekeleza hilo ilikuwa inawezekana kutafuta nusrah kutoka kwa wale ambao wanaweza kuaminiwa miongoni mwa maafisa wanajeshi ili kutekeleza kwa mfano mapinduzi ya kijeshi. Ilhali hawakuamini katika kutumia nguvu kupindua tawala, walijitetea kwamba wanatafuta msaada kutoka kwa wengine ili kuleta mabadiliko haya ambayo kimsingi yanahitaji nguvu. 

Ikrimah mara kwa mara alikuwa akipenda kujadiliana nao, na lau asingepata yeyote wa kumsikiza angelikuja kwangu kuniumisha kichwa kama ilivyokuwa tabia yake ya kujadili fikra zao na mimi. Alikuwa akisema, "Tatizo la Hizb ut Tahrir ni kwamba imeganda. Wanataka kutekeleza sera iliyotumika zamani katika zama zetu. Ni watu wa tayari tayari." Huku akiwa ameshikilia kikombe mkononi husema, "Wanataka kukilazimisha kikombe kupita katika shingo ya chupa…hawataki kufahamu kwamba miaka 13 ndani ya Makkah wakati wa Mtume (saw) sio miaka 13 ndani ya Jerusalem, Amman au Beirut, wala hata miaka 100…"

Sheikh Ata alikuwa mtu wa kawaida asiyejidhilalisha, mtulivu asiyejiangamiza. Alikuwa amezoea labda kutokana na sababu za kiafya kuweka baadhi ya matango chini ya kitanda chake. Mara kwa mara nilimuona akiunyoosha mkono wake na kuchukua vipande viwili au vitatu na kuvisafisha kwa mkono wake na kisha kuninyooshea kimoja upande wangu na kunikaribisha katika karamu ya matango.  

3. Ushuhuda uliotumwa kwangu na Kaka Muhammad Ali Abd al-Hamid (Abu Bakr) kutoka kwa Shahab wa Hizb, Amman.

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

"Ushuhuda kutoka kwa Mwanamume wa Haki"

Siku chache baada ya Ata Abu al-Rashtah kuchukua uongozi wa Hizb ut Tahrir na baada ya sisi kutoka Masjid Zamili ndani ya Amman baada ya kutekeleza swala ya pamoja, mhandisi Salih Abdullah al-Jaytawi (kutoka Muslim Brotherhood) alinijia na akaushika mkono wangu kwa furaha na kusema, "Pongezi, Mwenyezi Mungu aibariki." "Kwa nini" nikauliza. Akajibu, "Kwa kaka yetu, mhandisi, Ata Abu al-Rashtah kuchukua uongozi wa Hizb ut Tahrir na kwa hilo sasa nina uhakika kwamba Hizb ut Tahrir ni chama chenye ikhlass, kwa sababu kimemruhusu Ata Abu al-Rashtah kufika katika ngazi za uongozi. Namjua huyu mwanamume vizuri. Alikuwa mwenzangu na rafiki kipenzi."

"Namjua tokea siku za shule ya upili. Nilifuatana naye kwenda Beirut katika mitihani yetu ya kuingia katika Chuo cha Amerika ndani ya Beirut. Lakini, Mwenyezi Mungu hakutaka tuingie chuoni humo. Hivyo basi, tukasafiri kwenda kusomea uhandisi Cairo na kuishi pamoja huko na kukamilisha masomo ya uhandisi pamoja. Naapa kwamba muda niliomjua alikuwa mwanamume bora katika taqwa, maadili na tabia. Na baadaye tukawa tunatembeleana kila mmoja ndani ya Amman. Ukikutana naye mfikishie salamu za dhati kutoka kwangu."

Aliyekamilika ni Mwenyezi Mungu, Bwana mwenye cheo, aliye juu ya sifa wanazomuelekeza na amani iwe kwa manabii wake na sifa zote ni za Mwenyezi Mungu.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:48

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu