- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
UNAMA Inashughulikiwa kwa Mapenzi huku Wabebaji Dawah Waislamu Wakijibiwa kwa Ukandamizaji?!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Julai 9, 2024, Afisi ya Misheni ya Msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) ilichapisha ripoti ambayo utendakazi wa miaka 3 wa serikali ya Afghanistan kuhusu ‘haki za binadamu’ umekaguliwa. Katika ripoti hii ya kurasa 30, UNAMA imelaani na kukashifu vikali shughuli za Wizara ya Uamrishaji Mema na Ukatazaji Maovu, ikiviita vitendo vyake kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu. Katika ripoti hiyo, imeelezwa kuwa masuala kama vile ulazimishaji “uvaaji hijabu, kupiga marufuku wanawake kuonekana kwenye sinema, kuwataka wanawake kusafiri na watu wanaotegemewa (Mahram), kuzuia kusherehekea Siku ya Wapendanao, kuamrisha Swala za jamaa na adhabu...” huchukuliwa kama ukiukaji wa haki za binadamu na uhuru.
Tunachukulia ripoti hii iliyotolewa na UNAMA kama shambulizi la wazi dhidi ya kanuni na maadili ya Kiislamu na tunalaani kwa nguvu zote iwezekanavyo. Mashambulizi kama hayo dhidi ya Uislamu na kuenea kwa Fitna katika jamii yanafanyika wakati ambapo UNAMA afisi yake rasmi imefunguliwa nchini Afghanistan na maafisa wake wanapewa itifaki za juu wakati wa mikutano na viongozi wa serikali, na hata vikosi vya usalama vya serikali tawala hulinda maisha ya wafanyikazi wake na afisi rasmi kwa hatua za juu za usalama.
Cha kusikitisha, msimamo wa serikali inayotawala dhidi ya ripoti hii unaonekana kuwa duni na wa kulaumiwa. Rasimu ya awali ya ripoti hii iliposhirikishwa na Wizara ya Uamrishaji Mema na Ukatazaji Maovu, wizara hii bila kujali ilijiwajibisha kwa UNAMA na kujibu mashambulizi na matusi ya shirika hili kwa sauti laini - hoja zao pia zimeambatanishwa na ripoti hii. Kwa kweli, UNAMA inakuza maadili ya kiliberali na hutoa maslahi ya Marekani nchini Afghanistan, na shirika hili linajaribu kushawishi kitambulisho cha Kiislamu kwa Mujahidina kwa kuchapisha ripoti kama hizo.
UNAMA bila aibu inachukulia uamrishaji mema (Amr Bil Maruf) kuwa ni ukatili na dhidi ya haki za binadamu, lakini serikali inaonyesha uvumilivu, mnyumbuko na umuhimu kwao. Hata hivyo, wakati Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya kazi kwa kuzingatia kanuni za Amr Bil Maruf, wabebaji dawah wa Hizb sio tu hawaamiliwi kwa ukatili mkali bali pia wanatupwa magerezani na kuteswa kwa kisingizio cha kueneza ‘mgawanyiko na fitna’. Kwa nini serikali inachukua msimamo dhaifu dhidi ya matusi ya wazi ya UNAMA huku ikikandamiza ulinganizi wa Kiislamu wa Hizb ut Tahrir?!
[مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ]
“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.” [Al-Fath: 29].
Kupuuza shughuli hatari za UNAMA na mashirika mengine ya kimataifa nchini Afghanistan kwa badali ya baadhi ya maslahi ya kimada ni kosa kubwa la kisiasa ambalo litakuwa na matokeo mabaya. Watawala wa Afghanistan wanapaswa kuwa na msimamo madhubuti na wa wazi kwa Umoja wa Mataifa, misheni na vyombo vyake kwa sababu mashirika hayo ni mashirika ya kijasusi na zana za kisiasa za dola za Magharibi ambazo shughuli zake ni dhidi ya Uislamu na Waislamu, hivyo zinapaswa kukomeshwa haraka iwezekanavyo.
[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللّهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ]
“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Al-Baqara: 120]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan