Afisi Kuu ya Habari / Kitengo cha Wanawake: “Je, Tunapaswa Kujibu Vipi Maandamano ya Iran ya Kupinga Hijab?”
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika muda wa wiki mbili zilizopita, kumekuwa na maandamano kote nchini Iran na katika sehemu nyingine za dunia kujibu kifo cha Mahsa Amini, mwanamke wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22, ambaye inasemekana alikamatwa na polisi wa maadili wa Iran kwa kutofinika nywele zake ipasavyo na Hijabu na kupigwa hadi kufa akiwa chini ya ulinzi wao.