Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari: Kampeni ya Kitengo cha Wanawake "Waislamu wa Sri Lanka Wananyanyaswa, Walio Hai na Wafu!"

Kitengo cha wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir kimezindua kampeni pana ya kunyanyua utambuzi wa kiulimwengu juu ya dhulma kubwa na ukiukaji ambao Waislamu wanakabiliwa nao nchini Sri Lanka, na kuitaka serikali ya Sri Lanka kumaliza sera yake ya aibu ya kuchoma kwa nguvu maiti za wahasiriwa Waislamu wa COVID-19 nchini humo. Tangu Aprili mwaka huu, miili ya Waislamu wengi ambao walipimwa wakiwa na virusi vya Korona imechomwa, ikiwa ni ukiukaji mkali wa imani zao za Kiislamu.

Waislamu nchini Sri Lanka wamekabiliwa na ubaguzi, uchafuzi wa majina, na vurugu kwa miaka mingi kutokana na kuongezeka kwa msimamo mkali wa Mabudhi nchini humo. Kama inavyotarajiwa, serikali za ulimwengu, pamoja na serikali za kiimla zilizopo katika nchi za Waislamu, zimeshindwa kuwasaidia Waislamu wa Sri Lanka, kama kawaida yao ya kuwatelekezwa Waislamu wanaoteswa kote ulimwenguni. Lakini, sisi, Ummah wa Uislamu, hatutawatelekeza kaka na dada zetu Waislamu huko Sri Lanka, na sisi katika kitengo cha wanawake cha Hizb ut-Tahrir tunapaza sauti juu ulimwenguni kuwaunga mkono na dhidi ya dhulma kubwa wanayoteseka kutokana nayo.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ﴾

"Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia" [Al-Anfal: 72]

Dkt Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ijumaa, 10 Jumada Al-Awwal 1442 H sawia na 25 Disemba 2020 M

- Ili Kufuatilia Kampeni Hii kwa Lugha Nyenginezo -

Ili Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Cha zindua kampeni kwa anwani:

"Waislamu wa Sri Lanka Wananyanyaswa, Wafu na Walio Hai!"

Ijumaa, 10 Jumada Al-Awwal 1442 H sawia na 25 Disemba 2020 M

Bonyeza Hapa

Ili Kupakua Taarifa Hiyo kwa Lugha ya Waislamu wa Sri Lanka (Kitamil)

Bonyeza Hapa

Ili Kupakua Taarifa Hiyo kwa Lugha Rasmi Nchini Sri Lanka (Singhalese)

Bonyeza Hapa

- Alama Ishara za Kampeni -

#StopMuslimCremation fb instagram tw
#أوقفوا_حرق_موتى_المسلمين fb instagram tw
#MüslümanCenazeleriYakmayaSon fb instagram tw
#KomesheniUchomajiMotoMaitiZaWaislamu fb instagram tw

[ Risala za Kutilia Nguvu na Kuunga Mkono Kampeni Hii ]

- Ujumbe wa Wabebaji Ulinganizi wa Kike Nchini Uturuki -

- Ujumbe wa Wabebaji Ulinganizi wa Kike Nchini Uholanzi -

- Ujumbe wa Wabebaji Ulinganizi wa Kike katika Maeneo Yanayozungumza Kijerumani -

- Ujumbe wa Wabebaji Ulinganizi wa Kike katika Wilayah Lebanon -

- Ujumbe wa Wabebaji Ulinganizi wa Kike Nchini Indonesia -

- Video ya Ualishi wa Kampeni -

Ushuhuda wa Sameera Rinosa

Kuhusu Kuchomwa Moto Maiti za Waislamu Nchini Sri Lanka

Ujumbe kutoka kwa Kaka na Dada Zetu Nchini Sri Lanka

Zeinah As-Samit

14 Jumada al-Awwal 1442 H - 29 Disemba 2020 M

Waislamu wa Sri Lanka, Hakuna wa Kuwalilia!!

Bara’ah Manasrah

12 Jumada al-Awwal 1442 H - 27 Disemba 2020 M

Uchomaji wa Nguvu wa Maiti za Waathiriwa wa Kiislamu wa Covid-19 Nchini Sri Lanka Chini ya Utawala Ulio na Chuki na Waislamu Ambao Unalitumia Janga Hili la Maambukizi Kuzidisha Ajenda Yake Dhidi ya Uislamu

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

27 Rabii' al-Akhir 1442 H - 12 Disemba 2020 M

- Angalizi la Vyombo vya Habari -

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari:

Utumiaji wa Serikali ya Sri Lankan wa Janga la Maambukizi ya Covid19 katika Kuzichoma Moto Maiti za Waislamu!

Utumiaji wa Sri Lankan wa janga la Maambukizi ya #Covid19 katika kuzichoma maiti za Waislamu na Kutia Hofu juu ya Uislamu. Dkt. Nazreen Nawaz kutoka Uingereza anazungumza na Inayet Wadee katika

#NewsAndViews katika Salaamedia.

Jumamosi, 11 Jumadal Awwal 1442 H - 26 Disemba 2020 M

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Uchomaji kwa Nguvu wa Maiti za Waathiriwa wa Kiislamu wa COVID-19 Nchini Sri Lanka;

Vipi Tunapaswa Kujibu?!

Mnamo Aprili mwaka huu, serikali ya Sri Lanka ilitoa kanuni inayoamuru kwamba wale wote wanaokufa kutokana na Covid-19 au ambao walipatikana na virusi hivyo baada ya kifo wanapaswa kuchomwa moto, bila kujali imani zao za kidini, wakitaja wasiwasi usio na msingi wa afya ya umma kama sababu yao ya sera hii. Tangu Aprili, Waislamu kadhaa nchini Sri Lanka wamechomwa moto. Inaeleweka, kuna hofu kubwa ndani ya jamii ya Waislamu nchini Sri Lanka leo, ambao wamekabiliwa na vurugu, uchafuzi wa majina na ubaguzi ndani ya jamii kwa miaka mingi. Sasa, hawawezi hata kutekeleza ibada za mwisho za kidini za wapendwa wao kwa amani. Majadiliano haya ya paneli yanazungumzia jinsi Waislamu wanapaswa kujibu sera hii dhidi ya Waislamu na vile vile aina anuwai za dhulma ambazo Waislamu nchini Sri Lanka wamekuwa wakiteseka kwa miaka mingi.

Jumamosi, 04 Jumada al-Awwal 1442 H - 19 Disemba 2020 M

Mkusanyiko wa Picha

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 07 Januari 2021 11:41

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu