Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari: Hotuba ya Mhandisi Salah Eddine Adada katika Kongamano la Khilafah la 2022 lililofanyika nchini Uingereza

Hotuba iliyotolewa na Mhandisi Salah El-Din Adada, Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, katika kongamano "Kutoka India hadi Al-Qudsi" lililofanyika nchini Uingereza mnamo 16/07/2022 M chini ya kichwa:

"Tutasema tena na tena: Uislamu Peke Yake ndio Mgombezi Pekee wa Kuwatoa Watu Gizani na Kuwapeleka kwenye Nuru."

Jumamosi, 17 Dhul-Hijjah 1443 H - 16 Julai 2022 M

Hotuba ya Mhandisi Salah Eddine Adada, Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kutoka katika Kongamano Lililoandaliwa na Hizb ut Tahrir Uingereza, Julai 2022: “Kutoka India hadi Al-Qudsi”

(Imetafsiriwa)

Tutasema tena na tena: Uislamu Peke Yake ndio Mgombezi Pekee wa Kuwatoa Watu Gizani na Kuwapeleka kwenye nuru

Kwa miaka 100 iliyopita msukosuko wa Waislamu kote ulimwenguni umekuwa karibu sehemu kuu ya kila habari inayotangazwa.

Na mtu anaweza kuuliza, kwa nini ni hivyo?

Ni nini sababu ya mateso haya ya kuendelea?

Swali hili lingeweza kujibiwa kwa pande kadhaa, haswa kwa kuwa Uislamu ni mfumo unaoshindana kikweli na Waislamu ni Umma ulioimarishwa vyema.

Lakini upande mmoja wa jambo hili unaweza kusaidia kutoa uelewa mpana wa kile kinachoweza kuchukuliwa kuwa msukumo usioepukika kwa dhiki hii ya kuendelea.

Yaani, miaka 1400 iliyopita Uislamu ulikuja katika wakati ambapo wanadamu walikuwa wanazama katika ulimwengu wa giza wa kijahilia, ambayo ilikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya mafundisho kandamizi ya kipagani yaliyopitwa na wakati, na utawala fisadi kutokana na upotoshaji wa Biblia.

Na kwa upande wake wa kipekee wa kiroho usiofisidika, Uislamu ulikuwa na upanuzi wa haraka katika miji na maeneo ya ulimwengu uliostaarabika na ulioweza kufikika wakati huo. Na upesi akaanza kufuta giza kutoka kwa ulimwengu huo kwa kuziangaza akili na nyoyo za watu uliowagusa.

Kuenea huku kwa kijiografia kwa mfumo wa Kiislamu kuliunda muundo thabiti wa kijiografia kwa Umma wa Kiislamu. Na natija yake kizuizi kigumu sana cha kijiografia kwa yeyote aliyetaka kuufungua ulimwengu, na iliendelea kuwa hivyo kwa karne 13 zilizofuata. Yote yakisimamiwa na Khilafah.

Inakuja Uingereza, dola kuu ya kimataifa inayoibuka ya karne ya 19, ikiwa na nia kubwa ya kikoloni kushibisha njaa yake isiyokwisha ya utajiri na rasilimali.

Ikaanza kupanga njama dhidi ya Khilafah zenye ngazi nyingi, na katika mchakato huo ikaunda umbile la Kiyahudi katika Mashariki ya Kati na dola ya Kihindi katika Asia ya Kusini.

Hali mbili za kijiografia na kisiasa zenye mlipuko mkubwa ambazo ziliweka msingi wa kisingizio cha maisha yote cha uingiliaji kati kutoka kwa kigeni.

Hii ni sehemu kubwa ya jibu la kwa nini Waislamu wako katika machafuko ya kutatanisha kote ulimwenguni.

Na sasa iweje?

Kile ambacho hapo awali kiliitwa kuinuka kwa Magharibi, leo kimekuwa kile kinachoweza kuitwa laana ya Magharibi. Na hata kuanguka kwa Magharibi.

Pamoja na uvumbuzi wake wote wa kisayansi na maendeleo ya kiteknolojia, Magharibi sasa ina uwezo wa kuona ndani kabisa ya atomu na kwa mbali kwenye thureya lakini inasimama kinzani kujaribu kufafanua mwanaume ni nani mwanamke ni nani.

Ambayo ina maanisha thaqafa ya Kimagharibi imeshindwa kuleta furaha kwa wanadamu. Mbaya zaidi, thaqafa ya Kimagharibi pamoja na dosari zake za sasa katika siasa, afya, uchumi, usalama, mazingira na jamii iko ukingoni kujitumbukiza yenyewe kwenye shimo jeusi la machafuko ya kijamii na kiuchumi.

Kwa upande mwingine, Uislamu una madai ya uhakika…ambayo ni ya kimilenia, uliwafanya mamilioni ya watu kuwa na furaha. Na kama mfumo kamili wa kisiasa una ruwaza iliyo wazi kwa ulimwengu inayowafaa wanadamu; lakini hili linaweza tu kudhihirika pale Umma wa Kiislamu utakapoiregesha Khilafah na kwa mara nyingine tena kuiregesha nyumba ya wanadamu katika mpangilio.

﴿الر كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ

“Alif Lam Ra. (A.L.R.) Hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa.” [Ibrahim: 1]

Barak Allahu feekum

Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu

Media

https://htmedia.zat.one/Britain/2022/07/Salah_Conf16072022.mp4

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu