- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari / Kitengo cha Wanawake:
“Je, Tunapaswa Kujibu Vipi Maandamano ya Iran ya Kupinga Hijab?”
Katika muda wa wiki mbili zilizopita, kumekuwa na maandamano kote nchini Iran na katika sehemu nyingine za dunia kujibu kifo cha Mahsa Amini, mwanamke wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22, ambaye inasemekana alikamatwa na polisi wa maadili wa Iran kwa kutofinika nywele zake ipasavyo na Hijabu na kupigwa hadi kufa akiwa chini ya ulinzi wao. Katika baadhi ya maandamano hayo wanawake wamekuwa wakichoma hijab zao na kukata nywele zao ili kuonyesha hasira na upinzani wao kwa utawala wa serikali ya Iran unaojionyesha kuwa ni kielelezo cha utawala wa Kiislamu.
Kwa hivyo, maandamano haya yanalenga kufikia nini? Mfumo wa kisiasa wa Iran ni wa Kiislamu kiasi gani? Na je kama Waislamu tunapaswa kujibu vipi maandamano haya ya kupinga hijab? Haya ni baadhi ya maswali tunayotarajia kuyajibu katika mjadala huu.
Jumamosi, 05 Rabi-ul Awwal 1444 H sawia na 01 Oktoba 2022 M