Alhamisi, 07 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kongamano la Kuhitimisha Amali za Kampeni ya Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Khilafah 1444 H – 2023 M

Katika mwezi wa Rajab Tukufu mwaka huu 1444 H - 2023 M, na kwa mnasaba wa kumbukumbu chungu ya miaka 102 ya wahalifu kuivunja Dola ya Kiislamu mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu 1342 H sawia na 03/03/1924 M ambayo iliasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw) na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) ulioangaza pembe za dunia kwa kipindi cha karne 13, na kwa uelekezi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir iliangazia amali zilizoandaliwa na hizb katika maeneo inamo endesha shughuli zake, na pia ilizindua kampeni ya mtandaoni yenye kichwa:

“Je, Khilafah Inasimamishwa Vipi?

Na kileleni mwa kampeni hii ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tulifanya, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), kongamano maalum la hitimisho ambapo kundi la wasomi na wanaharakati wa da’wah walijadili mihimili muhimu inayoelezea njia ya kisheria ya kusimamisha upya dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Jumamosi, 27 Rajab Tukufu 1444 H - 18 Februari 2023 M

- Video Kamili ya Amali ya Kongamano Hitimishi -

Kongamano la kuhitimisha lilifanyika Magharibi mnamo Jumamosi tarehe 27 Rajab Tukufu 1444 H sawia na 18 Februari 2023 M, saa mbili kamili usiku kwa majira ya Madina Al-Munawwarah, saa moja usiku kwa saa za Bait ut-Maqdis (Al-Quds Al-Sharif).

Link ya Kongamano kutoka tovuti ya HTMedia
Link ya Kongamano kutoka Tovuti ya Al-Waqiyah TV  waqiyah2
Link ya Kongamano kutoka ukurasa wa Facebook wa Al-Waqiyah TV  facebook2
Link ya Kongamano kutoka Chaneli ya YouTube ya Al-Waqiyah TV youtube 

Ameer log

Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 102 ya kuvunjwa Khilafah

Jumapili, Rajab 28 Tukufu 1444 H - 19 Februari 2023 M

 

#Time4Khilafah #EstablishKhilafah
#ReturnTheKhilafah أقيموا_الخلافة#
#KhilafahBringsRealChange #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
#YenidenHilafet كيف_تقام_الخلافة#
#TurudisheniKhilafah #HakikiDeğişimHilafetle

Kufuatilia kwa lugha nyenginezo

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.