Alhamisi, 24 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Indonesia:

Mkutano wa Wanachuoni Nchini Indonesia (Multaqo ‘Ulema) umesisitiza Kuendeleza Mvutano wa Kusimamisha Khilafah

Zaidi ya wanachuoni 600, Masheikh na wahudumu wa Kiislamu, wakiwemo Habayeb na Maprofesa, walishiriki mkutano wa wanachuoni katika eneo la Madura / Java Mashariki, uliosadifiana na kumbukumbu la tukio la Isra na Miraaj ya Mtume (saw).

Katika Mkutano huo, Wanachuoni wa Kiislamu walieleza kwamba Uislamu ni Dini Kamili na kwamba ndiyo Dini pekee ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameiridhia na kuibariki kama ilivyo elezwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الإِسْلاَمَ دِينًا

"Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” (Surah Al Maidah: 3)

Khilafah ni sehemu muhimu ya mafundisho ya Uislamu ambayo lazima yatekelezwe. Kwa hiyo, kila kitendo cha kuwazuia, kuwatishia, kuwatia hatiani na kuwaadhibu wanao shiriki mvutano wa kuiregesha kwake ni uhalifu na kwenda kinyume na Uislamu na njia yake ya maisha.

Vilevile mkutano huo ulisisitiza kwamba watetezi, makundi, mashirika na miungano ya inayo piganaji kwa ajili ya kusimamisha Dola ya Khilafah ni watu kibinafsi, kikundi, miungano na mashirika ambayo yamechukua jukumu la masuala ya kidini na kamwe hayastahili kuzuiwa, kutishwa, kutiwa hatiani wala kuteswa.

Wanachuoni wote ambao walihudhuria mkutano huo walisisitiza kujitolea kwao daima kuwa watetezi wa Ulinganizi wa Kiislamu na kuwahami, ikiwa ni pamoja na kuwahami wanaopigia debe kusimamishwa kwa Dola ya Khilafah.

Jumapili, 24 Rajab 1440 H - 31 Machi 2019 M

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Indonesia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu