Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Malaysia:
Amali kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah

Sambamba na Kumbukumbu ya Kuanguka kwa Khilafah katika mwezi mzima wa Rajab mwaka huu, 1444 Hijiria, Hizb ut Tahrir/Malaysia iliandaa mfululizo wa Semina Mseto zinazosisitiza juu ya uhusiano wa kihistoria kati ya Khilafah na Ulimwengu wa Kimalay, na ufaradhi wa Waislamu kuisimamisha tena.

Semina ya Kwanza:

Tarehe: 22/01/2023

Anwani: Kuingia kwa Uislamu katika Ulimwengu wa Malay: Unachopaswa Kujua?

Wazungumzaji:

1. Ustaz Abdul Hakim Othman

2. Ustaz Ishan Ibrahim

Katika Semina hii, wazungumzaji wote wawili walijadili kuhusu historia ya jinsi Uislamu ulivyokuja katika Ulimwengu wa Malay. Wazungumzaji wote wawili waliangazia dori changamfu ya Maulamaa na wajumbe waliotumwa na Khilafah katika kueneza ujumbe wa Uislamu kwa Ulimwengu wa Malay, kinyume na maoni ya wanahistoria fulani kwamba kuenea kwa Uislamu kwenye eneo hili kulikuwa ni “matokeo ya pembeni” tu ya wafanyibiashara wa Kiislamu kutoka Mashariki ya Kati na India.

Baada ya kuthibitisha kuwa kuja kwa Uislamu katika Ulimwengu wa Kimalay hakutengani na maamrisho na faradhi ya Khilafah ya kueneza Uislamu duniani kote, wazungumzaji walisisitiza vidokezo kwamba historia ya Khilafah si ya kusomwa tu, bali pia ieleweke kuwa ni sehemu ya kanuni za Mwenyezi Mungu za Kiislamu hasa juu ya ufaradhi wa Waislamu kuungana pamoja chini ya utawala wake.

Malaysia: Semina "Uhusiano kati ya Khilafah na Ulimwengu wa Malay" kufunga Kampeni ya Rajab 1444 H

(Imetafsiriwa)

KUALA LUMPUR, 19 Februari 2023 - Baada ya mwezi mmoja wa kufanya kampeni ya ukumbusho wa kuanguka Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijri, Hizb ut Tahrir/Malaysia imefunga kampeni kwa kufanya semina ya mseto inayojadili mada hiyo.

Mtaalamu wa historia ya Nusantara (Malay Archipelagos) kutoka Indonesia, Ustadh Nicko Pandawa, alialikwa kama mgeni maalum katika semina hiyo ambaye alitoa mada yake kwa kichwa "Khilafah na Ulimwengu wa Malay: Uhusiano wa Jihad katika Kuzuia Ukoloni wa Kimagharibi".

Ustadh Nicko pia ni mwelekezi wa filamu ya "Jejak Khilafah di Nusantara" (Nyayo za Khilafah huko Nusantara), filamu ambayo inazungumziwa sana nchini Indonesia, na pia ni mwandishi wa vitabu kadhaa vya kihistoria kuhusu uhusiano kati ya Nusantara na

Khilafah.

Wanajopo wengine ni pamoja na Dkt. Tarmizi Salleh, Prof. Dkt. Muhammad Abu al-Ain na Ustadh Abdul Hakim Othman, kila mmoja aliwasilisha karatasi zenye kichwa: "Historia ya Uhusiano kati ya Ulimwengu wa Malay na Khilafah", "Kufichua Ajenda ya Magharibi ya Kuondoa

Fikra ya Kiislamu huko Nusantara" na "Nusantara na Faradhi ya Kusimamisha Tena Khilafah" mtawalia.

Semina ilianza majira ya saa nne asubuhi na kumalizika majira ya saa saba mchana na alhamdulillah ilikwenda vizuri.

Miongoni mwa risalam muhimu zilizotolewa katika semina hii ni ufahamu ambao Waislamu wa Nusantara wanapaswa kuwa nao kuhusiana na ushahidi wenye nguvu na sahihi wa kihistoria, kwamba Khilafah na ulimwengu wa Malay ina uhusiano wa karibu wa haki na watawala wa Nusantara kwa jumla wanaitambua nafasi na mamlaka ya Khalifa kuwa ndiye kiongozi mkuu wa Waislamu wote duniani.

Kilicho muhimu zaidi kwa Waislamu kuzingatia na kukumbuka, hasa kuhusiana na mwezi wa kuanguka Khilafah, ambayo imekuwa ni historia ya giza kwa Waislamu, ni juu ya ufaradhi wa kuisimamisha tena taasisi hii tukufu ya kisiasa kwa umakini.

Ni kwa njia hii pekee Waislamu wataweza kurudisha izza ya Uislamu, kuwaunganisha Waislamu, kuwashinda maadui wa Uislamu, kurudisha hadhi ya Umma huu na kuuregesha Uislamu kama dola kuu ya ulimwengu.

Huu ndio ujumbe kutoka kwa kila mwanajopo katika semina hii licha ya mada zilizojadiliwa.

Ijapokuwa mwezi wa Rajab umekwisha, juhudi na miito ya Hizb ut Tahrir ya kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume hazitakwisha hadi Mwenyezi Mungu (swt) atimize ahadi yake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Malaysia

Semina ya Pili:

Tarehe: 29/01/2023

Anwani: Mafungamano ya Kihistoria Baina ya Khilafah na Ulimwengu wa Kimalay

Wazungumzaji:

1. Ndugu Abbas Ismail

2. Dkt. Norazlan Shah

Katika Semina hii, wazungumzaji wote wawili walijadili uhusiano wa kihistoria kati ya Khilafah na Ulimwengu wa Kimalay. Ndugu Abbas aliwasilisha ushahidi wa kimajaribio kutoka kwa vitu vya kale na miswada ili kuthibitisha kuwepo kwa uhusiano hai kati ya Khilafah na watawala katika eneo hili. Ni dhahiri kwamba uhusiano kati ya Khilafah na watawala katika Ulimwengu wa Kimalay ulianzishwa mapema katika zama za Umawiyya.

Wakati huo huo, Dkt. Norazlan alitoa ushahidi mwingi kuunga mkono uhusiano mzuri kati ya Khilafah Uthmaniyyah na Wamalay katika eneo hili hasa wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia na kuvunjwa kwa Khilafah baadaye. Uhusiano huo ulikuwa wa karibu na wa dhahiri, licha ya vikwazo na vitisho vyote vilivyoletwa na wakoloni wa Magharibi kwa Wamalay.

Semina ya Tatu:

Tarehe: 05/02/2023

Anwani: Kuanguka kwa Khilafah, Uvamizi wa Magharibi na Mapigano ya Ulimwengu wa Malay

Mzungumzaji: Dkt. Muhammad Abu Al-Ain

Katika Semina hii, mzungumzaji alisisitiza juu ya juhudi za Khilafah Uthmaniyyah iliyokuwa imedhoofika katika kuimarisha tena mafungamano ya Kiislamu baina ya Khilafah na Waislamu wa dunia, zikiwemo ardhi za Malay. Kisha akaendelea na matukio yaliyosababisha kuanguka kwa Khilafah nchini Uturuki.

Kisha mzungumzaji akaendelea na juhudi za kukoloni za Magharibi kuuteka ulimwengu wa Kiislamu na juhudi za Waislamu katika Ulimwengu wa Malay kupigana dhidi ya dola za kikoloni za Magharibi. Ukweli kadhaa uliwasilishwa kuonesha kuwa Ulimwengu wa Malay ulikuwa na uhusiano wa karibu na Khilafah ambao ulidhihirika katika juhudi zake za kupambana na Wakoloni wa Magharibi, hususan Waingereza.

Semina ya Nne:

Tarehe: 12/02/2023

Anwani: Juhudi za Magharibi katika Kuzuia Kusimamishwa tena kwa Khilafah

Wazungumzaji:

1. Dkt. Norazlan Shah

2. Ndugu Wan Hisham Wan Salleh

Mzungumzaji wa kwanza alieleza kwa kina kuhusu ajenda ya Uingereza na juhudi za kuwazuia Waislamu wa Malay kurudi kwenye utawala wa Kiislamu tangu uvamizi wake katika Ardhi ya Malay. Sio tu kwamba wameikalia kimabavu ardhi hii na kutabikisha mfumo wao wa utawala, bali pia wametumia juhudi zote kuwazuia Waislamu katika eneo hili kujenga tena uhusiano wowote na Khilafah, na hatimaye kuzuia kuasisiwa tena kwa Khilafah.

Mzungumzaji wa pili aliangazia juhudi za kiulimwengu za nchi za Magharibi za kuzuia Umma wa Kiislamu kuregea katika Khilafah kwa njia ya Utume. Mzungumzaji pia alisisitiza umuhimu wa Waislamu kutambua ajenda ya Makafiri katika kutuweka tukiwa tumetengana na kuwa dhaifu kupitia dola za kitaifa na utaifa uliopandikizwa ndani ya mwili wa Ummah.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Malaysia

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Link za Ziada

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Malaysia

Facebook: Hizb ut Tahrir / Malaysia

Instagram: Hizb ut Tahrir / Malaysia

Telegram: Hizb ut Tahrir / Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu