Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wilayah Pakistan: Baada ya Amerika Kushindwa kwa Fedheha nchini Afghanistan, Simamisheni Khilafah Kummaliza Raj Mkoloni wa Kiamerika

(Imetafsiriwa)

Silaha za kisasa za majeshi waoga wa Amerika hazikulingana na Waislamu wenye silaha duni ambao hawakumuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt), huku wakitamani kuuawa mashahidi au ushindi.

Udanganyifu wa nguvu za kijeshi za Amerika umesambaratishwa machoni mwa Waislamu, huku ujasiri wa Amerika katika kukabiliana na Umma wa Kiislamu uliokakamaa umetingishwa mno.

Hali ya leo ni fursa kwa Waislamu wote ambao wanataka ukombozi kutoka kwa miongo ya mateso chini ya Raj mkoloni Amerika, ambao unaweza kutokea tu kupitia Khilafah.

Khilafah ndio itakayokataa maagizo ya kiuchumi kutoka IMF, ikiimarisha uchumi kupitia uunganishaji wa rasilimali kubwa na anuwai za Ulimwengu wa Kiislamu.

Ni Khilafah ndio itakayokata mafungamano ya uharibifu kwa "Vita dhidi ya Ugaidi" vya Amerika, ikikusanya vikosi vya jeshi la Ulimwengu wa Kiislamu kama jeshi kubwa zaidi ulimwenguni kulinda Uislamu na Waislamu.

Khilafah ndio itakayoondoa uwezo hatari wa ufuatiliaji wa ubalozi mdogo wa Amerika jijini Karachi na ubalozi mkuu wa Amerika jijini Islamabad, ambao unahujumu usalama wetu.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا)

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah an-Nisa'a 4:139]

Jumatano, 11 Dhu al-Hijjah 1442 H - 21 Julai 2021 M

#HiredFacilitators

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu