Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 07/06/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 18 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 07 Juni 2023 M

 Njia ya Mabadiliko Yajumuisha Kutafuta Nusrah

Mabadiliko kamwe hayatakuja kupitia mapigano kati ya jeshi na watu. Kudhoofisha jeshi letu ni hatari kwa usalama wa taifa. Operesheni za kijeshi dhidi ya watu wetu kujilimbikizia madaraka ya kisiasa pia hudhoofisha serikali. Kwa mujibu wa Njia ya Utume, njia ya mabadiliko lazima ijumuishe utoaji wa Nusrah wa jeshi kwa uongozi wa kisiasa wa Kiislamu. Makamanda wa kijeshi wa Answaar walitoa Nusrah yao kwa Mtume ﷺ katika Kiapo cha Pili cha Aqabah. Matokeo yake, dola ya Kiislamu iliasisiwa Madina.

12 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 01 Juni 2023 M

Msimamo Dhaifu wa Uongozi wa Pakistan Umehujumu Uwezo Wetu Halisi wa Kijeshi

Kwa mujibu wa Global Firepower, Pakistan iko nafasi ya saba ya jeshi lenye nguvu zaidi duniani, mwaka wa 2023. Hata hivyo, msimamo dhaifu wa uongozi umetuzuia kuwa dola kuu ya dunia. Msimamo wake kwa kuzingatia kanuni za ushirikiano na dola za kikoloni. Uongozi huo dhaifu hautumii silaha hizi kwa ajili ya kuulinda Uislamu na Waislamu, iwe ni ukombozi wa Kashmir au Al-Masjid Al-Aqsa. Ni sera madhubuti ya vita ya Khilafah pekee ndiyo itakayotumia silaha hizi kwa ajili ya izza ya Uislamu.

13 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 02 Juni 2023 M

 Ni Muungano na Marekani ndio Unaosababisha Kukosekana Utulivu

Mnamo tarehe 29 Mei, mkuu wa jeshi alionya maafisa wa Chuo cha Amri na Wanajeshi Quetta kuhusu "muunganisho kati ya mambo ya ndani ya ushirikiano na vikosi vya nje ili kuleta ukosefu wa utulivu." Hakika, nguvu za nje ni hatari, kwa nini kudumisha muungano na Marekani? Marekani inazuia jeshi letu mbele ya India, ili kuruhusu uimarishaji wa kuikalia kimabavu Kashmir. Marekani inachochea mapigano na Afghanistan, ambayo yanazuia umoja kati ya Waislamu. Ni Khilafah ndiyo itakayomaliza muungano wa uharibifu na Marekani, kuwaunganisha Waislamu na kuzikomboa Ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu.

14 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 03 Juni 2023 M

Khilafah Itazuia Mfumko wa Bei Unaovunja Migongo ya Watu

Katika Ripoti yake ya Nusu ya Mwaka kwa Mwaka wa Fedha wa 2023, iliyotolewa mnamo tarehe 19 Mei 2023, Benki Kuu ya Pakistan ilionya kwamba, "mfumko wa bei ulipanda hadi kiwango cha juu cha miongo kadhaa." Mfumko wa bei ni matokeo ya moja kwa moja ya mfumo wa kibepari ambao hutekeleza ufadhili kifedha wenye riba na sarafu ya karatasi ya isiyo na thamani ya dhati (fiat). Hakuna bajeti yoyote ya kibepari inayoweza kutoa afueni kwa watu wanaoteseka. Khilafah ilihakikisha karne nyingi za bei thabiti kwa sababu ya ufadhili wa kifedha usio na riba na sarafu iliyoegemezwa juu ya dhahabu na fedha. Ilikuwa ndio kituo kikuu cha biashara ya ulimwengu.

15 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 04 Juni 2023 M

Majeshi ya Msalaba ni Maadui, Sio Washirika wa Waislamu

Mnamo tarehe 31 Mei 2023, mkuu wa jeshi la Uingereza alikutana na mkuu wa jeshi la Pakistan na "maswala ya usalama wa kikanda na mambo ya maslahi ya pande zote yalijadiliwa," kulingana na taarifa ya jeshi kwa vyombo vya habari. Jeshi la Uingereza lilikuwa sehemu ya muungano wa vita vya msalaba, ambao ulichinja Waislamu nchini Iraq na Afghanistan. Ilikuwa ndio ufunguo wa uvamizi wa kikatili wa Waingereza kwa Waislamu wa India. Khilafah haitafungua mambo yake ya usalama na maadui wa Uislamu. Itapigana nao, itawashinda na kujadili masharti yao ya kujisalimisha.

16 Dhul Qi'dah 1444 H sawia na 05 Juni 2023 M

Afisa Mmoja wa Usalama wa Misri Aweka Mfano Unaong’aa kwa Wapiganaji wa Leo

Mnamo tarehe 3 Juni 2023, afisa wa usalama wa Misri aliwapeleka wanajeshi watatu wa Kiyahudi kuzimu, kabla ya kuikumbatia shahada. Hofu ililitikisa jeshi la Mayahudi kutokana na nguvu zake za Iman. Hivyo basi je, umbile la Kiyahudi litakuwaje, wakati majeshi ya Waislamu hatimaye yatasonga mbele dhidi yake? Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Ni wakati sasa wa misimamo ya kishujaa. Uondoeni uongozi muoga unaokuzuieni. Hamasikeni kwa ajili ya ukombozi wa Ardhi za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu, mkitafuta ushindi au kifo cha kishahidi.

17 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 06 Juni 2023 M

Mfumo wa Kilimwengu wa Kimagharibi Unazuia Kuunganishwa kwa Waislamu kama Dola Moja ya Khilafah

Mnamo tarehe 4 Juni 2023, muungano wa kijasusi wa Macho Matano (FVEY) ulitangaza, "kujitolea bila kuyumbayumba kudumisha sheria kulingana na mfumo wa kimataifa." Mfumo wa dunia unaozingatia sheria za kikoloni unahakikisha Ulimwengu wa Kiislamu unadhoofishwa, kwa kuugawanywa dola za kitaifa hamsini na tano. Utaifa unawagawanya Waislamu katika mataifa kadhaa, na kusababisha uadui na uhasama kati yao. Uislamu unawaunganisha Waislamu kuwa Umma mmoja, kuwatia nguvu dhidi ya maadui zao. Khilafah kwa Njia ya Utume itaziunganisha nchi za Kiislamu zilizopo kama dola moja, kubwa na yenye nguvu.

18 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 07 Juni 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu