Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Je, India Yainuka?

(Imetafsiriwa)

India inasonga mbele lakini hii haitokani na rasilimali au nguvu zake yenyewe. Ni kwa sababu ya msaada wa Marekani. Marekani huunga mkono dola ambazo zinajitahidi kuimarisha mfumo wa kimataifa unaoungwa mkono na Marekani na kulinda maslahi ya Marekani.

Sera hii ya Marekani si kwa India pekee. Marekani imefuata sera mithili ya hiyo kwa dola zengine vilevile. Kwa mfano, Japan. Marekani iliimarisha Japan kiuchumi baada ya Vita vya pili vya Dunia, lakini iliiweka kuwa dhaifu kijeshi. Mfano mwingine ni Korea Kusini. China pia iliimarishwa na Marekani katika siku za nyuma ili kuzuia muungano wake na Umoja wa Kisovieti. Kando na hayo, Ujerumani pia iliimarishwa na Marekani baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ili Marekani iweze kutawala mambo ya Ulaya.

Hadi kufikia katikati ya miaka ya tisiini, India ilikuwa nje ya mzunguko wa ushawishi wa Marekani. Katikati mwa miaka ya tisiini, India haikuwa na nguvu kwa msingi wa nguvu zake yenyewe. Hata hivyo, mkakati wa Marekani kwa India ulibadilika. Marekani ilitabanni sera ya kuimarisha India dhidi ya China.

Marekani hutumia zana tano kuimarisha, au kudhoofisha, dola chini ya mfumo wake wa kilimwengu, hizi ni:

1-Uwekezaji wa Kigeni: Marekani huelekeza makampuni yake kuwekeza katika nchi zinazofungamana na sera za Marekani, ikiwemo India. Ilianza mchakato huu nchini India, wakati wa Manmohan Singh na inaendelea hadi leo.

2-Uhamisho wa teknolojia: Marekani inaruhusu makampuni yake ya teknolojia kuwekeza katika nchi washirika. Inawapa teknolojia ya hali ya juu. Kama mfano Amazon, Google na Apple wanawekeza nchini India leo.

3-Ufikiaji masoko ya kimataifa: Marekani kupitia mashirika ya kimataifa inatoa njia ya ufikiaji masoko ya kimataifa kwa nchi washirika wake. Hii ni ili waweze kuuza bidhaa na huduma zao katika masoko haya. India na China ziliboresha uchumi wao kwa kuongeza mauzo ya nje. Hii ilitokana na ufikiaji masoko ya kimataifa ambao uliwezeshwa na Marekani.

4-Usaidizi wa Kijeshi: Kupitia mikataba ya uhamisho wa teknolojia ya kijeshi, Marekani huimarisha ulinzi wa nchi zilizo chini ya ushawishi wake. Inafanya hivyo leo na India na umbile la Kiyahudi. Zaidi ya hayo, Marekani inauza silaha zake, manuari, makombora, droni na nyambizi, kwa nchi kama hizo.

5-Uhamiaji na kuingiza thaqafa ya Kimagharibi: Marekani inawepesisha uhamiaji kwa watu wa nchi zilizo chini ya ushawishi wake. Inarahisisha sera za visa kwao. Kwa hivyo, vijana na wafanyibiashara wa nchi hizi wanapata njia ya ufikiaji wa taasisi kuu za kielimu na utafiti za Marekani. Marekani inawafunza vijana hawa na wajasiriamali kulingana na maadili yake na mfumo wa kimagharibi.

Sasa swali linazuka kwamba ikiwa watawala wote wa India na Pakistan wanataka kutekeleza ajenda ya Marekani katika eneo hilo, basi kwa nini India inaendelea kwa msaada wa Marekani, wakati Marekani haisaidii Pakistan kujiendeleza?

Kwanza, huu ni mpango wa Marekani. Itaimarisha baadhi ya nchi na kudhoofisha nyingine kulingana na mtazamo wake wa maslahi yake. Ni somo kwetu kuwa na ruwaza yetu ya maendeleo yetu. Hatupaswi kuandaa ramani ya utendakazi kwa maendeleo yetu kulingana na mipango ya dola zengine. Ruwaza yetu ya maendeleo isiwe tu kwa Pakistan pekee bali kwa Umma mzima wa Kiislamu.

Pili, Marekani kukataa kutusaidia ni kutokana na mgongano wa hadhara kati ya Uislamu na Magharibi. Demokrasia ya kiliberali ya kibepari inakinzana na aqeeda ya Uislamu na maagizo ya wazi ya Shariah. Wazo la uhuru unaoleta vitendo kama ushoga na kutukana matukufu ya Uislamu kwa hakika ni kinyume na aqeeda ya Uislamu. Je, tunawezaje kutarajia Marekani itusaidie, au kutuimarisha, wakati mfumo wake wa kimataifa umejengwa juu ya maadili ambayo ni kinyume na aqeeda yetu?

Kwa hivyo, badala ya kutumia juhudi zetu zote kuiridhisha Marekani na kuwa chombo cha kulinda maslahi ya Marekani, ambayo watawala wetu wamekuwa wakifanya kwa miaka 75 iliyopita, inatubidi kuukataa mfumo wa kilimwengu wa Marekani.

Inatubidi tujitengenezee njia huru yetu wenyewe. Inatubidi tuanzishe mfumo wetu wa kilimwengu uliojengwa juu ya umoja wa ulimwengu wa Kiislamu kupitia kusimamishwa Khilafah. Ardhi za Waislamu ni tajiri wa rasilimali, zina majeshi makubwa na idadi ya vijana ambayo itaifanya Khilafah kuwa dola kuu ya dunia. Zaidi ya yote, mfumo wa ulimwengu unaoegemezwa juu ya umoja wa Waislamu utaegemezwa juu ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu ﷻ na Mtume Wake ﷺ na utakuwa kwa mujibu wa maagizo ya Dini yetu na maadili yetu. Kwa hiyo hebu na tuukataeni mfumo wa dunia wa Marekani na tuzidishe mapambano yetu ya kusimamisha Dola ya Khilafah.

#Time4Khilafah

Jumapili, 21 Dhul-Hujjah 1444 H - 09 Julai 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu