Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 03/01/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 21 Jumada Al-Akhir 1445 H sawia na 03 Januari 2024 M

 

Waislamu wa Pakistan Wanatamani Kusikia Takbira za Jihad kwa ajili ya Ukombozi wa Kashmir na Palestina

Mnamo tarehe 20 Disemba 2023, wakati wa ziara yake nchini Marekani, mkuu wa jeshi la Pakistan alisema kwamba Pakistan “imetoa huduma zisizo na kifani na kujitolea katika vita dhidi ya ugaidi na itaendelea kupigana hadi mwisho wa kimantiki kulingana na matarajio ya watu wa Pakistan.” “Vita dhidi ya Ugaidi" ya Marekani vilipiganwa kwa mujibu wa amri za Wamarekani, na sio matarajio ya Waislamu. Lau watawala wangejali matarajio ya Waislamu, wangelikusanya jeshi kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Hakika, Waislamu daima wanataka uhamasishaji na wako tayari kutoa kila mhanga. Mwenyezi Mungu ﷻ  amesema, 

[كُتِبَ عَلَيۡکُمُ الۡقِتَالُ وَهُوَ كُرۡهٌ لَّـكُمۡۚ ]

“Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu.” [Surah Al-Baqarah 2:216]

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 28 Disemba 2023 M

Simamisheni Khilafah na Muunganishe Eneo la Pakistan, Kusini na Asia ya Kati na kwengineko, iwe Dola Moja

Akizungumza na wanafikra nchini Marekani mnamo tarehe 20 Disemba 2023, mkuu wa jeshi la Pakistan alisema, “Pakistan inataka kujiweka kama kitovu cha mawasiliano na lango la Asia ya Kati na kwengineko.” Chini ya mfumo wa ulimwengu wa Marekani, lengo hili ni kutumikia maslahi ya Marekani, kuunda kambi ya kikanda inayotawaliwa na India. Katika mfumo wa sasa wa kilimwengu, uongozi wa kiwakala wa Pakistan unatumia nguvu za nyuklia na jeshi la sita kwa ukubwa duniani kuendeleza maslahi ya Marekani pekee. Simamisheni Khilafah kwa Njia ya Utume ili kuepuka ukoloni. Khilafah itaunganisha Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati na kwengineko, kama dola moja. Kwa haraka, Khilafah itaibuka kama dola kuu ya ulimwengu katika njia yake ya kuwa dola inayoongoza duniani.

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 29 Disemba 2023 M

Waislamu huko Gaza Wanalazimishwa Kuchagua kati ya Kifo na kifo Zaidi

Kwa mujibu wa shirika la Euro-Med Human Rights Monitor, 98% ya wananchi wa Gaza hawana chakula cha kutosha, wakati 71% wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, huku 64% wakikiri kula nyasi, matunda, chakula kisichokomaa na bidhaa zilizomalizika muda wake. Kuna wastani wa kila siku wa lita 1.5 za maji kwa kila mtu kwa ajili ya kunywa na kuoga, huku lita 16.5 zikiwa ni muhimu kwa ajili ya kuishi. Ndugu, dada, mama na watoto wetu wanauawa kishahidi kwa mabomu ya umbile la Kiyahudi, huku wale walioachwa wakiwa hai wanakabiliwa na kifo kwa njaa. Maafisa wa kijeshi wa Kiislamu wana uwezo wa kuliangamiza umbile la Kiyahudi ndani ya saa chache. Hata hivyo, pamoja na kuona usaliti wa wazi wa viongozi wao, hawataharaki. Ummah lazima uwahisabu kwa kutotenda kwao. Hakika, watahisabiwa na Mwenyezi Mungu ﷻ Siku ya Kiyama pamoja na uongozi wao wa khiyana.

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 30 Disemba 2023 M

Badala ya Kuchachawa na Uchaguzi, Mtazamo Wetu Lazima Uwe Uhamasishaji wa Haraka wa Majeshi Yetu ya Kuikomboa Palestina

Uchaguzi unapigiwa debe kwenye vyombo vya habari. Ni kana kwamba utaleta mabadiliko fulani ya kimsingi nchini Pakistan. Ulisia ni kwamba vyama vingi vimeshindwa hata kutoa manifesto zao za uchaguzi. Mabadiliko pekee ambayo chaguzi hizi zitaleta ni mabadiliko ya sura. Wasiwasi wa kweli kwa Waislamu wa Pakistan ni kukataa kwa uongozi wa kijeshi wa Pakistan kuhamasisha jeshi kuikomboa Palestina. Waislamu wa Pakistan, wenye ushawishi mkubwa na watu wenye mamlaka, wote wanapaswa kuhamasishwa kwa ajili ya kuondolewa kwa uongozi wa sasa wa Pakistan. Hapo ndipo amri, ambazo askari wetu jasiri wanangojea, zinaweza kutolewa. Inawezekana tu kwa kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 31 Disemba 2023 M

Ukatili wa Dola ya Kibaniani Utamalizika kupitia Jihad Iliyobarikiwa, Sio ShutmaTupu

Afisi ya Mambo ya Nje ya Pakistan imelaani mauaji ya “kikatili” ya watu watatu chini ya ulinzi wa Jeshi la India huko Kashmir Inayokaliwa kimabavu mnamo 24 Disemba, 2023. Je, dhalimu ashawahi kuondoa mkono wake kutokana na dhulma kwa shutma pekee? India ina ujasiri wa kuwatesa Waislamu wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu kwa sababu tu imehakikishiwa kujizuia kwa watawala wa Pakistan, kulingana na amri za Marekani. Khilafah kwa njia ya Utume itazikomboa ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu, kama vile Kashmir na Palestina, kupitia Jihad iliyopangiliwa ya vikosi vya jeshi, kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu,

[وَاَخۡرِجُوۡهُمۡ مِّنۡ حَيۡثُ اَخۡرَجُوۡكُمۡ]

“na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al Baqarah, 2:191]

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 01 Januari 2024 M

Ukaliaji Kimabavu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Umbile la Mayahudi ni Saratani, Inayohitaji Upasuaji

Mnamo tarehe 26 Disemba 2023, Mkuu wa Majeshi ya umbile la Mayahudi, Herzi Halevi, alisema, “Vita vitaendelea kwa miezi mingi.” Hivyo, Wazayuni wanatangaza mpango wao wa kuchinja hata wanawake na watoto wengi zaidi. Wakati Wanajeshi wa Msalaba waliposhambulia Palestina, walimwaga mito ya damu ya Waislamu na kuikalia kimabavu kwa miongo kadhaa. Salahuddin Al-Ayyubi aliikomboa Ardhi hiyo Iliyobarikiwa kupitia kuwaunganisha Waislamu chini ya Khilafah, na kuyakusanya majeshi ya Waislamu. Badala ya kurusha shutma kama dawa za kutuliza maumivu, saratani huondolewa kwa upasuaji kupitia vikosi vya jeshi. Leo, ugonjwa ni ule ule na matibabu pia ni yale yale. Kwa hivyo ni nani kati ya vikosi vya kijeshi vya Waislamu atakayeanzisha operesheni hii, kama Salahuddin Al-Ayyubi alivyofanya?

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 02 Januari 2024 M

Utabikishaji Kamili wa Uislamu ni Muhimu kwa ajili ya Kulinda Haki za Wasiokuwa Waislamu

Mkuu wa Jeshi la Pakistan alihudhuria hafla ya Krismasi katika kanisa moja mnamo tarehe 25 Disemba 2023. Alisisitiza haja ya kukuza maelewano kati ya dini mbalimbali katika jamii. Lengo la maelewano kati ya dini mbalimbali katika mfumo wa kisekula wa Kimagharibi ni kuachana na hukmu za Kiislamu, na kukubali mfumo wa maisha wa kisekula. Waislamu hawakubali na kamwe hawatakubali kuvunjwa kwa Dini yao. Kulinda haki za wasiokuwa Waislamu hakutapatikana kwa kushiriki sikukuu za kikafiri. Inalazimisha utekelezaji wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha. Kwa zaidi ya miaka 1300 ya Khilafah, watu wa dini nyingi waliishi maisha ya amani. Mfano mzuri ni idadi kubwa ya Mayahudi katika Andalus ya Kiislamu, ikifuatiwa na uhamiaji wa Mayahudi kutoka Andalus hadi Khilafah ya Uthmani.

21 Jumada al-Akhir 1445 H - 03 Januari 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu