Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan: Silsila, “Kauli za Wanazuoni kuhusu Khilafah”

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi wake na wageni wa kurasa za Afisi Kuu ya Habari silsila ya video yenye kichwa, “Kauli za Wanazuoni kuhusu Khilafah” iliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Pakistan.

Tafadhali Tegea...

#Ulema4Khilafah

[Kipindi 1]

Imam Ahmad, aliyefariki mwaka 241 H, katika “Musnad,” yake amesema kwamba, “Mtume (saw) amesema, 

«إِذَا خَرَجَ ثَلاَثَةٌ فِي سَفَرٍ فَلْيُؤَمِّرُوا أَحَدَهُمْ»

‘Wanapotoka watu watatu katika safari, basi wachague mmoja wao kuwa Amir.’” Ibn Tamiyyah alieleza, “Hivyo basi, Mtume (saw) alitoa amri ya kuwekwa amiri juu ya kundi linalofanya safari, ambalo ni la lazima kwa aina zote za makundi. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kuamrisha mema na kukataza yale ambayo ni munkar. Hili linaweza tu kufanywa kwa nguvu na utawala... Kuhusiana na hili ilisimuliwa, ‘Mtawala ni kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) katika ardhi.’”

Jumapili, 27 Safar 1446 H - 01 Septemba 2024 M

[Kipindi 2]

Katika “Sunan” yake, ad-Darimi, ambaye alifariki mwaka 255 H, alisimulia kutoka kwa Umar (ra) ambaye alisema, “Hakuna Uislamu, bila ya jamaa. Hakuna jamaa, bila ya Imarah. Hakuna Imarah, bila ya utiifu. Yeyote anayefanywa kuwa mtawala na watu wake, kwa mujibu wa Fiqh (ufahamu wa kisheria wa Dini), kuna uhai kwa ajili yake na kwao. Yeyote anayetawalishwa na watu wake, kwa mujibu wa isiyokuwa Fiqh, ni maangamivu kwake na kwao.”

Jumatatu, 28 Safar 1446 H - 02 Septemba 2024 M

[Kipindi 3]

Imam Mawardi, aliyefariki mwaka 450 H, alisema katika kitabu chake “al-Ahkam as- Sultaniyyah,” kwamba, “Imamah inaasisiwa ili kuchukua urithi baada ya Utume, katika kulinda Dini na siasa za dunia.

Hufungwa juu ya yule mwenye kutekeleza wajibu ndani ya Ummah. Ni faradhi kwa Makubaliano ya pamoja (Ijma’a).”

Jumanne, 29 Safar 1446 H - 03 Septemba 2024 M

[Kipindi 4]

Imam Al-Khateeb al-Baghdadi, aliyefariki mwaka 463 H, alisema, katika “Tarikh Baghdad,” kwamba, “Muhajirina na Answari walikubaliana kwa kauli moja juu ya Khilafah ya Abu Bakr (ra).

Wakamwambia, ‘Ewe Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).’ Hakukuwa na mtu wa ziada aliyetajwa pamoja naye. Inasemekana kwamba yeye (ra) alimrithi Mtume (saw) kwa mamlaka ya Waislamu thelathini elfu. Kila mmoja wao akamwambia Abu Bakr, ‘Ewe Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).’ Walitosheka naye na wale waliokuwa baada yake, Mwenyezi Mungu (swt) awe radhi nao.”

Jumatano, 01 Rabi Al-Awwal 1446 H - 04 Septemba 2024 M

[Kipindi 5]

Mwanachuoni wa fiqh Abu Al-Fath ash-Shahrastaani, aliyefariki mwaka wa 548 H, amesema katika kitabu chake “Nihayat al-Aqdaam,” kwamba, “Na haikutokea kwa Abu Bakr (ra), wala kwa mtu mwengine yeyote, kwamba inajuzu kusiwepo na Imamu (Khalifa) ardhini.

Kwa hiyo yote haya ni ushahidi kwamba Maswahaba (ra), ambao ndio waliotangulia, wote walikuwa wanakubaliana kwamba lazima kuwe na Imam. Hivyo, hiyo ni Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja). Ni ushahidi wa kukatikiwa wa faradhi ya Imamah (Khilafah).”

Alhamisi, 02 Rabi Al-Awwal 1446 H - 05 Septemba 2024 M

[Kipindi 6]

Imam an-Nawawi, aliyefariki mwaka 676 H, alisema katika kitabu chake “Al-Manhaj Sharh Sahih Muslim,” kwamba, “Ilithibitishwa kwa Makubaliano ya Pamoja (Ijma’a) kwamba Waislamu lazima wamchague Khalifa. Ufaradhi wake unatokana na Shariah, na sio fikra za kibinadamu.”

Ijumaa, 03 Rabi Al-Awwal 1446 H - 06 Septemba 2024 M

[Kipindi 7]

Ibn Taymiyyah (rh), ambaye alifariki mwaka 728 H, alisema katika kitabu chake, “Majmuu’ al-Fatawa,” kwamba, “Ni faradhi kujua kwamba usimamizi wa watu ni miongoni mwa faradhi kuu za Dini.

Zaidi ya hayo, hakuna Dini wala maisha ya dunia bila hayo. Wana wa Adam (as) hawawezi kufikia maslahi yao, isipokuwa kwa kukusanyika. Hii ni kutokana na mahitaji ya pamoja baina yao. Ni jambo lisiloepukika kwamba wanahitaji mamlaka, wanapokusanywa kwa pamoja.”

Jumamosi, 04 Rabi Al-Awwal 1446 H - 07 Septemba 2024 M

[Kipindi 8]

Ibn Khaldun, ambaye alifariki mwaka 808 H, alisema katika “Al Muqaddimah,” kwamba, “Kumteua Imam (Khalifa) ni faradhi.

Ni faradhi katika Shariah, inajulikana kwa Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja) ya Maswahaba (ra) na Taba’iyn. Maswahaba (ra) wa kipenzi chetu Mtume (saw), waliharakisha kumpa Bay’ah Abu Bakr (ra), baada ya kifo chake (saw). Walimkabidhi jukumu la Khilafah kusimamia mambo yao. Ndivyo ilivyokuwa, katika kila zama. Watu hawakuachwa katika machafuko, katika zama zozote. Ilitatuliwa kwa makubaliano ya pamoja, kutokana na dalili ya ufaradhi wa kumteua Imam (Khalifa).”

Jumapili, 05 Rabi Al-Awwal 1446 H - 08 Septemba 2024 M

[Kipindi 9]

Allama Zain al-Din al-Ansari, aliyefariki mwaka wa 926 H, alisema katika kitabu chake, “Ghayat ul-Wasul,” kwamba, “Ni wajibu kwa watu kumteua Imam (Khalifa) ambaye anatimiza maslahi yao, kama vile kulinda mipaka, kuandaa majeshi na kuwatiisha maadui na wezi. Ni Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja) ya Maswahaba (ra), baada ya kifo cha Mtume (saw), kumteua Imam (Khalifa). Waliliona hili kuwa faradhi muhimu zaidi. Walilitanguliza juu ya mazishi ya Mtume (saw). Watu katika kila zama walitenda ipasavyo.”

Jumatatu, 06 Rabi Al-Awwal 1446 H - 09 Septemba 2024 M

[Kipindi 10]

Ibn Hajar al-Haytami, aliyefariki mwaka wa 974 H, alisema katika kitabu chake, “Al-Sawa’iq Al-Muhriqah,” kwamba, “Jueni pia kwamba Maswahaba (ra) walikuwa na Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja) kwamba kumteua

Imam (Khalifa), baada ya mwisho wa zama za Utume, ni faradhi. Zaidi ya hayo, waliifanya kuwa faradhi muhimu zaidi ya zote. Walijishughulisha na faradhi hii juu ya kumzika Mtume (saw).

Jumanne, 07 Rabi Al-Awwal 1446 H - 10 Septemba 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu