Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilaya Pakistan: Deni lenye Msingi wa Riba!

Kwa kuizamisha Pakistan ndani ya Deni Lenye Misingi ya Riba, Serikali ya PTI Inawanyima Masikini, ili Kudhamini Faida kwa Wawekeza wa Ndani na wa Kigeni kama vile ilivyo kuwa serikali za kifisadi zilizotangulia, serikali ya PTI imeizamisha Pakistan katika Deni lenye msingi wa Riba, ikiwanyang’anya masikini haki yao kutoka katika Hazina ya Dola. Kiasi cha Rupia bilioni 2,442 zimetumiwa katika malipo ya Riba hadi kufikia mwezi Machi 2020 ambayo ni kiwango kikubwa sana cha Bajeti jumla ya Rupia bilioni 7,000.

Malipo ya Riba ni kikwazo kikubwa katika miradi ya miundombinu ya Ummah na ya kibinafsi, ambapo mingi ya miradi kama hii hufadhiliwa kwa mikopo, inayo pandisha gharama ya miradi yote kama hii, mfano hai ni deni la sasa la Pakistan katika sekta ya nishati. Kimsingi, Urasilimali huzichukulia benki zenye mfumo wa riba kama aina ya biashara, ambapo riba ni kama faida halali inayotokana na biashara hiyo. Hakika, wale wote ambao hutawala kwa misingi ya Kirasilimali kamwe hawataweza kutatua tatizo la mtego wa deni, hata kama wanadai kwamba wanataka kukomesha shida za masikini. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لاَ يَقُومُونَ إِلاَّ كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنْ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. [Al-Baqara 2: 275]

Ijumaa, 21 Shawwal 1441 H - 12 Juni, 2020 M

#KataaUrasilimaliSimamishaKhilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu