Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ardhi Iliyobarikiwa: Kalima Nzito Kutoka Msikiti wa Al-Aqsa Uliobarikiwa "Wenye Kusawazisha Mahusiano ni Wasaliti, na Palestina Itakombolewa na Majeshi ya Khilafah"

Hizb ut-Tahrir katika Ardhi iliyobarikiwa (Palestina) iliandaa amali katika Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa, ambapo ilitoa hotuba kali yenye kushutumu makubaliano ya kusawazisha mahusiano ya Imarati na Bahrain pamoja na umbile vamizi la Kiyahudi. Hayo yalijiri katika kisimamo cha kupinga baada ya swala ya Ijumaa kwa anwani "Wenye Kusawazisha Mahusiano ni Wasaliti, na Palestina Itakombolewa na Majeshi ya Khilafah"

Kalima hiyo ilijumuisha uhalifu wa makubaliano haya, ambayo yanahalalisha uwepo wa umbile vamizi la Kiyahudi na kupuuza ardhi ya Isra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na ikaonyesha kuwa makubaliano haya ya khiyana ni kiungo katika mchakato wa kutambuliwa na kusawazishwa mahusiano na yule mvamizi, na Imarati na Bahrain zimetanguliwa katika usaliti huu wote na Misri, Jordan, Uturuki na chama cha PLO.

Na kalima hii ikasisitiza kuwa watawala na serikali katika usaliti huu wote ni gora moja, wale waliosawazisha leo, na wale watakaosawazisha mbeleni na wale waliotangulia, na kwamba hawa Ruwaibidha hawatapata utukufu wa kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa, wala Al-Qudsi sio Al-Qudsi yao na wala Al-Aqsa sio Al-Aqsa yao, bali Al-Qudsi ni ya Waislamu na Al-Aqsa ni Waislamu, na majeshi ya Ummah huu ndio watakaoikomboa Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa chini ya kivuli cha Khilafah ambayo Ummah inamiliki nguzo za kusimama kwake.

Sauti za Takbir ziliongezeka na washiriki wakatamka dhidi ya serikali za khiyana na wakalingania kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ambayo itakomboa Ardhi yote Iliyobarikiwa (Palestina).

Ijumaa, 01 Safar 1442 H sawia na 18 Septemba 2020 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 23 Septemba 2020 08:45

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu