Alhamisi, 19 Dhu al-Hijjah 1442 | 2021/07/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 20/06/2021

Mwendelezo wa amali za umma zinazofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mikoa na wilaya mbalimbali za nchi ili kujenga rai jumla kuhusu vipengee vya Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na hali mbaya na hali ngumu ya maisha ambayo watu wanateseka kwayo kutokana na kufuata sera za wakoloni makafiri na kutiishwa kwa masuluhisho ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa.

Mnamo Jumanne, Mei 25, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan - eneo la Umbada walitoa hotuba ya kisiasa kwa anwani: "Janga la Kiuchumi Nchini: Sababu na Masuluhisho Yake" iliyotolewa na Ustadh Muzmil Sadeeq (Abu Azam).

Chini ya anwani "Kongamano la Paris ni mfano wa kupoteza utajiri wa Waislamu chini ya jina la uwekezaji", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya Sudan walitoa hotuba yao ya kila wiki katika mji wa Gadharef, Alhamisi, Mei 27, 2021, karibu na eneo la Mfalme Maidan Rowena, na Mhandisi Al-Bashir Ahmed Al-Bashir aliwahutubia wahudhuriaji, akifichua ukweli wa makongamano ambayo husemwa ni juu ya kusaidia nchi masikini ambazo zina madeni makubwa. Chini ya kichwa hiki: "Demokrasia ni urithi wa makafiri na Khilafah ni urithi wa utume," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Kosti mnamo Ijumaa, Mei 28, 2021 katika Soko la Rabak, makutano ya reli na Barabara ya 50, ambayo Ustadh Musa Abkar alizungumza, akielezea mgongano wa demokrasia na ghariza ya kibinadamu kama matokeo ya kutenganisha dini na serikali na maisha.

Katika muendelezo wa kaulimbiu ya Kongamano la Paris, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya Sudan – eneo la Madani walitoa hutuba ya umma katika kituo cha basi katika Souk Al Kabeer mnamo Jumanne, 1 Juni 2021, chini ya anwani: "Kongamano la Paris ni Kumpa Uwezo Mkoloni Kafiri Kupora Utajiri wa Ummah", ambapo Ndugu Ali Sowar alizungumza, akielezea serikali imeweka matumaini yake yote kwenye kongamano hili ili kutatua tatizo lake la kiuchumi.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Khartoum pia walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Jumatatu, Juni 7, 2021 katika uwanja wa Jackson, chini ya anwani: "Ukweli wa Mazungumzo ya Amani huko Juba." Mhandisi Ahmed Jaafar alihutubia hadhira juu ya ukweli wa mazungumzo ya sasa kati ya ujumbe, serikali na vuguvugu maarufu katika sekta ya kaskazini, na akaweka wazi kuwa lengo kuu la mazungumzo haya ni kuondoa Uislamu kutoka katika maisha ya watu kupitia fikra ya usekula.

Mnamo Jumanne, Juni 8, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya Sudan - eneo la Madani walitoa hotuba ya umma katika kituo cha basi katika Souk al-Kabeer chini ya anwani: "Dola ya Khilafah huchukua sarafu za dhahabu na fedha, na dolari haina thamani." Kutakuwepo na dhahabu na fedha, kutakuwepo na ustawi katika bei za bidhaa, huduma na ubadilishanaji wa biashara, na hakutakuwa na nafasi ya wizi wa juhudi na udanganyifu.

Chini ya anwani: "Makubaliano ya Amani, Ni Kujisalimisha Zaidi na Dhidi ya Uislamu," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - Jiji la Gadharef walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Alhamisi, Juni 10, 2021, Maysara Yahya Muhammad Nour alihutubia wasikilizaji, akielezea kuwa serikali inasonga mbele kutekeleza mipango ya Wamagharibi makafiri kwa kujibu harakati za kisilaha kwa kujumuisha haki ya kujitawala wenyewe, ambapo ni mwendelezo wa kuipasua nchi vipande vipande kwa kufuata nyayo za Serikali ya Wokovu iliyopita.

Hotuba ya kisiasa kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Kosti ilipewa kichwa: "Khilafah ni dola ya uangalizi, sio dola ya utozaji ushuru," mnamo Ijumaa, Juni 11, 2021 katika Soko la Ribik, makutano ya reli na Barabara ya 50, ambapo Ustadh Abd al-Majid Othman Ibrahim alizungumza, ambaye alielezea jinsi ya ushughulikiaji wa maswala ya watu wa Dola ya Khilafah tangu wakati wa Mtume (saw) hadi Makhalifa Waongofu.

Katika muktadha wa kuongezeka kwa bei ya mafuta hivi karibuni, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Madani walitoa hotuba ya hadhara katika kituo cha mabasi katika Soko Kuu mnamo Jumanne, Juni 15, 2021 kichwa: "Serikali ya Mpito inaongezeka maradufu bei za mafuta na inakwenda mbali zaidi katika kufukarisha watu wake kupitia maagizo ya mabwana zake,” ambapo Abdulaziz alielezea kuwa serikali ya mpito inatekeleza maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na haijali kuhudu ugumu wa maisha unaotokana na kuongezeka kwa bei za mafuta.

Mnamo siku ya Jumatano, Juni 16, 2021, Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi eneo la Libya, ikihutubia sera inayoitwa: "Usekula ni kutengwa kwa Uislamu na kuvunjwa vunjwa kwa kile kilichobaki cha Sudan", ambapo Ustadh Ahmed Abkar alizungumza, ambaye alianza hotuba yake kwa utangulizi wa kihistoria juu ya utekelezwaji wa Uislamu katika nchi ya Kiislamu hadi ulipoanza utekelezwaji wa usekula.

Katika muktadha huo huo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Dukhainat, kusini mwa Khartoum, mnamo Alhamisi, Juni 17, 2021, ambayo ilikuwa na anwani: "Kuongezeka kwa bei za mafuta ... Sababu na suluhisho msingi”, Ambapo Al-Fateh Abdullah, ambaye aliorodhesha sababu za kuongezeka kwa bei ya mafuta, ikiwemo kuelea kwa pauni na kuondolewa kwa ruzuku juu ya bidhaa kwa kujibu na kulinga na masharti ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa.

Katika mwelekeo mwingine, uthabiti juu ya maadili na ikhlasi katika mwendo na kuhisi jukumu kubwa, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkao wake wa kila mwezi jijini Gadharef mnamo Ijumaa, Juni 19, 2021 katika afisi ya chama huko Gedaref, ambao ulipewa anwani: "Mapambano ya majenerali wa Amerika na raia wa Ulaya na hasara ya watu wa Sudan." Waraka wa kwanza uliwasilishwa na Maysara Yahya Muhammad Nour, ambapo alielezea ukweli wa mzozo wa Ulaya na Amerika juu ya nchi hii unaojumuishwa katika pande za serikali, kila moja kulingana na matumizi yake.

Katika waraka wa pili, Bwana Billa Mahmoud alifafanua kwa kina hukmu ya kisheria kwa yale wanayoyafanya watawala wa Sudan, wa kiraia pamoja na wa kijeshi, na akafafanua kutoweka uaminifu kwa makafiri na kuwawezesha kutokana na utajiri wa Waislamu, na aliwahakikishia wahudhuriaji kwamba yule anayehifadhi utajiri wao na kuwalinda kutokana na utawala wa nchi za kirasilimali ni dola Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu