Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Taarifa ya Habari 01/09/2021

Mwendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika majimbo na maeneo mbalimbali nchini ili kuunda rai jumla yenye utambuzi wa vifungu vya Uislamu na suluhisho zake zinazohusiana na nidhamu tofauti za maisha, zinazoshughulikia mada anuwai, ikiwemo hijra ya Mtume (saw) na kuasisiwa kwa dola ya Kiislamu, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, na kuwasili kwa Taliban madarakani nchini Afghanistan kati ya mada nyenginezo.

Mnamo Agosti 12, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, katika eneo la Omdurman Magharibi, walitoa hotuba ya kisiasa kwa anwani: "Kwa nini hijra ya Mtume kwenda Madina?" na Sheikh Yassin Shuqar, aliyeanza hotuba yake na swali: Kwa nini ahamie Madina na sio ash-Sham, Yemen au Iraq?

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Dukhainat pia walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Agosti 11, 2021 katika soko la Al-Kalakila, kwa anwani: "Hatari za Mvua Kubwa ... Suluhisho la Dola na Suluhisho Msingi", ambapo Bwana Abdullah Hussein alielezea hatari za mvua kubwa na hali ya serikali kupuuza jukumu lake ustawi wa mambo ya watu kwa kujenga mitaro ya maji na kutengeneza ngome za ardhini ili kulinda watu kutokana na hatari hizi.

Chini ya kichwa: "Rufaa ya Jinai ni kujisalimisha kwa Magharibi Kafiri na usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na waumini." Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba yao ya kila wiki katika mji wa Gadharef mnamo Agosti 12, 2021, wakitoa mfano wa ukimya wake juu ya uhalifu uliofanywa dhidi ya Waislamu katika maeneo anuwai ulimwenguni.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mji wa El Obeid pia walifanya kikao cha kawaida mnamo Agosti 14, 2021, kwa anwani: "Ni nani atakayejaza ombwe la kisiasa nchini?" Imam Muhammad Ibrahim aliwasilisha waraka wa kwanza wenye kichwa: "Ombwe la Kisiasa," akielezea maana ya ombwe kama kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi na utulivu, akiorodhesha aina za ombwe la kijeshi, kimkakati na kisiasa na mifano ya kila mmoja wao, huku Ustaadh Al- Nazir Muhammad Hussein akiongea katika waraka wake kuhusu "Je! Ombwe hili liliundwaje na linajazwaje? Alielezea kuwa ombwe hilo liliundwa na nchi za kikoloni baada ya mapinduzi ya viwanda huko Ulaya na hitaji lao la soko la kuuza bidhaa zao za viwandani, kwa hivyo walifikiria kuiondoa Khilafah Uthmani kupitia kueneza fikra za utaifa, uzalendo, uhuru na demokrasia.

Pia, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika jiji la El-Obeid mnamo Agosti 18, 2021, yenye kichwa: "Kesi ya Wahalifu baina ya Udhalimu wa The Hague na Uadilifu ya Uislamu" ambapo Bwana Ahmed Wadaa Abdel-Karim alizungumzia juu ya Mahakama ya The Hague na madhumuni ya kuanzishwa kwake, akielezea kuwa ni mahakama ya kisiasa tangu hapo mwanzo. Kuzinyenyekesha serikali kutekeleza ajenda za nchi za kikoloni za Ulaya.

Chini ya anwani: "Hijra ya Mtume na Mabadiliko Msingi", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba yao ya kila wiki katika jiji la Gadharef mnamo Agosti 19, 2021, ambapo Ustaadh Nasr al-Din al-Hajj alionesha kuwa hijra ni mojawapo ya matukio makubwa sana ambayo taifa la Kiislamu (Ummah) limepitia kwa sababu ya mabadiliko msingi ambayo yaliandamana nayo. Katika maisha ya Waislamu, yalibadilika kutoka udhaifu hadi kuwa na nguvu na kutoka kwa ughaibuni hadi kwenye dola.

"Mafunzo ya Hijra ya Mtume" chini ya kichwa hiki, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa huko Omdurman Magharibi mnamo Agosti 21, 2021 katika Kituo cha Al-Firdaws, kitalu cha 15, ambapo Profesa Ishaq Muhammad Hussein alizungumza

Chini ya kichwa: "Taliban na Kuanzishwa kwa Khilafah," Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika vyuo vikuu walianzisha kona ya majadiliano katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Uchumi na Mafunzo ya Kijamii, ambapo Ustaadh Al-Fateh Abdullah alizungumza, ambaye alielezea uhusiano wetu na Taliban na Khilafah, na kwamba Khilafah ni uongozi jumla kwa Waislamu ili kutekeleza sheria za Kiislamu, na kwamba Taliban inakabiliwa na fursa ya kihistoria ya kuanzisha Khilafah, na sisi, kama Waislamu, tumefungamanishwa na fungamano la itikadi ya Kiislamu pamoja nao, kwa sababu Khilafah ni dola ya kiulimwengu yenye itikadi ya kiulimwengu ichipuzayo kutoka kwake.

Chini ya anwani "Mahakama ya Jinai, Chombo cha Uadilifu au Chombo cha Kisiasa?", Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya kikao chake cha kawaida katika jiji la Gadharef katika afisi yake huko Dim Hamad Sharq mnamo Jumamosi, Agosti 21, 2021. Waraka wa kwanza uliwasilishwa na Bwana Maysara Yahya.

Mkusanyiko wa Picha

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu