Jumatano, 30 Sha'aban 1444 | 2023/03/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 13/06/2022

Katika muendelezo wa amali za hadhara zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika maeneo tofauti tofauti ya nchi, ili kuuamsha Umma wa Kiislamu kupitia kuunda rai jumla inayofahamu masuluhisho ya Uislamu, yanayoshughulikia mpango wa mfumo wa pande tatu wa mazungumzo ya kutatua mgogoro wa utawala nchini, migomo ya wafanyakazi na masuala mengine.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman walifanya mazungumzo ya kwanza yenye kichwa, "Mfadhaiko na Jinsi ya Kukabiliana nao?" mnamo Jumatano Mei 18, 2022 katika soko la Libya ambapo Bwana Muzammil Al-Siddiq (Abu Azzam) alizungumza, akielezea matumaini yake kwamba watu wataondokana na mzunguko wa mfadhaiko unaotokana na idara za kijasusi na vituo vya utafiti vya kimataifa vinavyofuatilia harakati na misukosuko ya watu na mataifa, ukiwemo Umma wa Kiislamu ambao mara tu unapokaribia kukombolewa kutoka katika utumwa wa Kafiri mkoloni, Magharibi huingilia kati kupitia zana zake kwa lengo la kuupotosha kutoka kwenye njia yake na kuunda hali ya mfadhaiko wa kisiasa, inayosifia hali ya taifa hili na kiwango cha mfadhaiko kilichofikia nchini Sudan. Kisha akawakumbusha waliohudhuria juu ya jukumu walilokabidhiwa la kuleta mabadiliko ya kweli na ya kimsingi, na  dori yao katika kuwatoa watu kwenye giza na kuwapeleka kwenye nuru, na hili linahitaji kuusoma Uislamu kupitia Seerah kama Mtume (saw) katika kuunda dola ya Uislamu na kubeba ujumbe wa nuru na uongofu kwa walimwengu.

Mnamo Mei 21, 2022, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkao wake wa kawaida katika afisi yake, chini ya mada: "Je, Mpango wa Utatu Unatatua Matatizo ya Sudan?" Ndani yake, Muhammad Al-Amin Dafa Allah alizungumza kuhusu mipango ya ndani kama vile mpango wa Chama cha Umma, mpango wa Hamdok na mengineyo, akionyesha kwamba haikujengwa juu ya msingi wa Uislamu pamoja na kuwa ni maagizo ya Magharibi. Pia alizungumzia mipango ya nje kama vile mpango wa Volcker, ambao ni miradi ya Marekani inayotumia zana zao zikiwakilishwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, IGAD na nyenginezo, akielezea kushindwa kwa mipango yote ya ndani na nje kutatua matatizo ya Sudan, hususan Umoja wa Mataifa, ambao umeshindwa nchini Yemen, Syria, Iraq, Libya na leo nchini Sudan.

Katika jiji la El-Obeid, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kaskazini, Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan ilitoa hotuba ya hadhara Mei 19, 2022 mbele ya ukumbi wa swala wa Siwar al-Dhahab, yenye kichwa: "Mambo Yanayozuia Umoja wa Waislamu", ambapo Muhammad Qoni alizungumza, akielezea kutokuwa na ufahamu kwa Waislamu na kuelewa kwao Uislamu kuwa ni mfumo kamili wa maisha na mafungamano ya watu kwa misingi ya uzalendo, n.k, jambo linalozuia umoja wa Waislamu.

Katika upande mwengine, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano katika vyuo vikuu yenye kichwa: "Mgogoro wa Kisiasa na Kamari ya Suluhisho", katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Biashara, mnamo siku ya Jumamosi, Mei 28, 2022, ambapo Mhandisi Ahmed Jaafar na Mhandisi Awab Yasser walizungumza. Ambapo Mhandisi Ahmed Jaafar alielezea uhalisia wa mgogoro wa mapinduzi ya Al-Burhan mnamo Oktoba 25, 2021 na kuyanasibisha na yale yaliyotangulia tangu kuanguka kwa utawala uliopinduliwa wa Omar Al-Bashir. Jinsi mambo yalivyozidi kuwa mabaya zaidi.

Chini ya anwani: "Mgogoro wa Kimataifa na Athari Zake kwa Sudan", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya mnamo Mei 31, 2022, huko Omdurman Magharibi, ambapo Abdul Rahim Abdullah alizungumza, akionyesha kwamba mgogoro kati ya haki na batili ni wa zamani na kwamba utaendelea kuwepo hadi kiyama kitakaposimama, akisisitiza kwamba sababu na malengo ya mzozo wa kimataifa na mvutano wa dola za kikoloni dhidi ya Sudan ni kwa ajili ya kubeba fikra zake, kueneza kanuni yake ya kikatili ya kibepari, kutandaza thaqafa yake kote duniani, kupata manufaa ya kimada na kupora utajiri mkubwa wa nchi hii ambao Magharibi inaumezea mate.

Hoja nyengine za mazungumzo zilitolewa kupitia maingiliano na umma zikielezea masuluhisho sahihi ya Kiislamu kwa masuala mbalimbali yanayoikabili Sudan hivi sasa.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu