Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Kwa Mara ya Tatu, Hotuba za Halaiki Zilitolewa dhidi ya Muundo wa Makubaliano katika Msikiti Mkuu Jijini Khartoum

(Imetafsiriwa)

Ndani ya wigo wa kampeni ambayo Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan inaifanya dhidi ya muundo wa makubaliano, leo Alhamisi tarehe 5/1/2023, hizb ilitoa hotuba za halaiki kwa mara ya tatu baada ya swala ya Adhuhuri katika Msikiti Mkuu jijini Khartoum, ambazo kwazo wazungumzaji walieleza hatari ya fikra ya kifederali iliyotajwa katika muundo wa makubaliano katika Ibara ya 3 Miongoni mwa kanuni za jumla ambazo Sudan Kusini ilitenganishwa, na sasa kilichobakia kwa Sudan ni kusambaratishwa na fikra hii ovu, wakieleza kwamba muundo wa makubaliano hayo kiasili ni maagizo ya Marekani na Uingereza, pamoja na katiba ambayo makubaliano haya mabaya yalijengwa. Na vilevile mazungumzaji walionyesha ufisadi wa fikra ya Hawakir; yaani ugawanyaji wa ardhi kwa misingi ya kikabila ambayo ni urithi wa mkoloni anayesisitiza kuwa ukiukwaji huu wa kisheria ubaki kuwa halali, na kwa hiyo wakausisitiza katika katiba yao katika ibara ya 8/38.

Kwa kumalizia, wazungumzaji walisema kuwa mfumo wa utawala katika Uislamu ni mfumo wa umoja na sio mfumo wa federali, wakitilia nguvu kauli zao kwa dalili za Kisharia, na kuwataka waumini washirikiane na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo hizb imetayarisha zana za katiba yenye ibara 191 zilizovuliwa kwa ijtihad sahihi kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie.

Umati wa waumini ulishiriki kwa takbira, shangwe na dua za kufaulu. Na shukrani zote ni kwa Mwenyezi Mungu kwa tawfiq yake.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Sudan

- Ripoti ya Picha juu ya Amali za Hotuba za Halaiki -

Hotuba iliyotolewa na Mhandisi Basil Mustafa

Katika Lango la Kaskazini la Msikiti Mkuu Jijini Khartoum

Hotuba iliyotolewa na Dkt Ahmad Abdul Fadheel

Katika Lango la Kusini la Msikiti Mkuu Jijini Khartoum

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu