- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Mkutano na Waandishi wa Habari katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) Kuzindua Kampeni ya Kupambana na Mihadarati!
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa mkutano wa waandishi wa habari mnamo siku ya Jumapili 29 Jumada al-Aakhir 1444 H sawia na 22/1/2023 M katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) kuzindua kampeni kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 102 ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu (Khilafah) ili kupambana na mihadarati chini ya kichwa: “Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan yazindua kampeni ya kupambana na mihadarati”.
- Video Kamili ya Amali za Mkutano wa Waandishi wa Habari -
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Mkutano na Waandishi wa Habari katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) Kuzindua Kampeni ya Kupambana na Mihadarati
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumapili, 29 Jumada II 1444 H sawia na 22/1/2023 M, katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) kuzindua kampeni ya kupambana na mihadarati chini ya kichwa: “Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan yazindua kampeni ya kupambana na mihadarati”.
Waliozungumza ndani yake ni: Ustadh Ibrahim Othman Abu Khalil - msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, na Dkt. Muhammad Abdul Rahman - mwanachama wa Hizb ut Tahrir.
Dkt. Mohamed Abdel-Rahman alizungumzia hatari ya mihadarati, na jinsi inavyotengenezwa, kukuzwa na kutishia makundi na watu binafsi, na jinsi ilivyobadilika kutoka kuwa biashara ya asili hadi kuwa tasnia ya kemikali za sumu. Pia alizungumzia maendeleo ya kuingia kwake Sudan kutoka kwa kiasi kidogo kilicho languliwa kabla ya mwaka 2013 M hadi tani nyingi zilizobebwa na makontena kupitia viwanja rasmi vya ndege na bandari nchini kwa utambuzi wa serikali. Kilichochangiwa na hali hiyo ni kudorora kwa hali kutokana na ombwe la kisiasa, kiusalama na kiuchumi na ulegevu wa serikali tangu utawala uliopita kwa suala la madawa ya kulevya, ambayo iliwezesha kuenea kwake na kuifanya kuwa bidhaa maarufu.
Ama kuhusu Ustadh Abu Khalil, msemaji rasmi wa hizb katika Wilayah ya Sudan, yeye alisisitiza umuhimu wa akili, jinsi Mwenyezi Mungu alivyomtukuza mwanadamu kwayo, na jinsi Uislamu ulivyoifanya akili kuwa moja ya malengo ya juu zaidi ya jamii ambayo lazima yachungwe na kuhifadhiwa.
Ustadh Abu Khalil alionya kwamba kuzama Sudan katika mihadarati inachukuliwa kuwa moja ya silaha madhubuti katika vita vya kisasa vya kisiasa. Ambayo imeainishwa ndani ya vita vya kizazi cha nne, au kizazi cha tano, na kwa hakika ni vita vilivyokusudiwa kumwangusha adui aliyelengwa ndani, kuinyenyekesha dola yake, na kuinyang'anya mapenzi yake, na akaashiria kuwa ni vita hatari vinalenga jamii yote, sio tu ya kijeshi, na Ustadh Abu Khalil alionyesha kwamba fikra za Kimagharibi zenye sumu pia ni silaha za uharibifu mithili ya madawa ya kulevya, zenye kulenga fikra na thaqafa ya watu wa nchi hii, kwa kulenga Uislamu mtukufu; ambayo ni dini na kutokana nao ni dola, kama vile uteuzi wa Volker kama gavana mkuu wa Sudan, balozi za Magharibi na muitiko wa mashirika ya kimataifa kwa nchi hii, shughuli za mashirika ya kiraia yaliyoundwa na mkoloni, na upandaji fikra za kisekula na za kiraia, fikra za demokrasia, kuelekea kutengwa kwa wanawake, na ufisadi wa vijana, ambayo yote husababisha kuanguka kwa ukuta Mlinzi wa jamii hivyo kukiukwa na kuporomoka.
Kupitia mkutano huu, Ustadh Abu Khalil alizindua kampeni hii kubwa iliyoongozwa na hizb ya kutokomeza mihadarati chini ya kichwa: (Mihadarati ni vita na kupitia Khilafah tutashinda).
Na kampeni hii itaendelea, Mwenyezi Mungu akipenda, katika mwezi wa Rajab al-Fard. Na akasema: Tunalenga vijana katika sehemu zao za mikusanyiko, pamoja na semina, khutba za Ijumaa, mihadhara, na hotuba katika vitongoji na furqan, na mikusanyiko ya watu katika maeneo ya umma, vipande, mabango, na mengineyo. Abu Khalil amesisitiza kuwa, ushindi wa kweli katika vita hivi dhidi ya Umma wa Uislamu, kwa mihadarati au mengineyo, utapatikana tu kwa kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, kwani peke yake ndio mlinzi na mtetezi akitumia kama dalili kauli ya Mtume (saw): «الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye.”; yaani ni kinga. Alihitimisha kuwa kampeni hiyo iko chini ya kauli mbiu (#المخدرات_حرب_بالخلافة_ننتصر).
Katika kipindi cha maingiliano, idadi kubwa ya wanahabari na wale wanaopenda masuala ya umma walitoa michangio mizuri na ya ukarimu, ambapo waliipongeza hizb kwa majibu yake ya kawaida na ya mara kwa mara kwa kadhia nyeti za watu na hamu yake katika mambo yao ambapo wanahabari walitoa maoni: Wanasiasa na viongozi wa nchi wako wapi kutabanni suala muhimu kama hili?
Pia waliitaka hizb kutabanni suala hili hadi ilifikishe kwenye nafasi za maamuzi nchini.
Kwa kumalizia, mwendesha jukwaa aliishukuru hadhira kwa ushiriki wao na usikilizaji mzuri.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Katika Wilayah ya Sudan
- Mahojiano kando ya mkutano na waandishi wa habari katika Shirika la Habari la Sudan -
- Mahojiano na Ustadh Muhammad Jami (Abu Ayman) -
- Mahojiano na Dkt. Mohamed Abdel-Rahman -
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
“Usomaji wa Vifungu vya Muundo wa Makubaliano Vinavyohusiana na Wanawake”
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kilifanya muhadhara kwa kichwa “Usomaji wa Vifungu vya Muundo wa Makubaliano Vinavyohusiana na Wanawake” ambapo wafuatao walihadhiri: Ustadha Ghada Abdel-Jabbar (Um Awwab) na Ustadha Hanan Ibrahim (Umm Ali Saeed).
Jumatano, 03 Rajab Tukufu 1444 H - 25 Januari 2023 M
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/2995.html#sigProIddc552948b7
kwa Anwani: Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Yazindua Kampeni ya Kupambana na Mihadarati
Mwaliko wa Kuhudhuria na Kushiriki katika Mkutano na Waandishi wa Habari
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan
Alama Ishara za Kampeni
#Time4Khilafah |
#EstablishKhilafah |
#ReturnTheKhilafah |
#TurudisheniKhilafah |
#KhilafahBringsRealChange |
#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي |
أقيموا_الخلافة# |
كيف_تقام_الخلافة# |
#YenidenHilafet |
#HakikiDeğişimHilafetle |