Jumamosi, 19 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Tanzania:

Amali zilizo ratibiwa wakati wa Kampeni ya Kiulimwengu, “Ukombozi wa Kontantinopoli Bishara njema Ikatimia… ikifuatiwa na Bishara Njema!”

Chini ya muongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio adhimu la Ukombozi wa Konstantinopoli #Konstantinopoli (mji wa Hirakila) ambao ulizingirwa kuanzia mnamo 26 Rabii’ al-Awwal mpaka 20 Jumada al-Awwal 857 H, sawia na 5 Aprili hadi tarehe 29 Mei 1453 M na hivyo bishara njema ya Hadith tukufu ya Mtume (saw) ikapatikana:

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِير ُأَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Kwa yakini Mtaifungua Konstantinopoli, Amir bora ni Amir wake, na Jeshi bora ni jeshi hilo.”

Hizb ut Tahrir / Amerika imezindua amali zake katika kampeni hii ya kiulimwengu. .Sifa njema zote anastahiki Mwenyezi Mungu (swt).

Ijumaa, 20, Jumada al Awwal 1441 H - 15 Januari, 2020 M

Soma kwa ukamilifu Taarifa kwa vyombo vya Habari kutoka Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania:

KUKAMILIKA KWA KAMPENI YA “UKOMBOZI WA KONSTANTINOPOLI”

Hizb ut Tahrir / Tanzania imekamilisha kampeni ya Ufunguzi wa Konstantinopoli iliyo zinduliwa mwanzoni mwa mwezi huu na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kama kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio adhimu la Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli (mji wa Heraclius) ambao ulizingirwa kuanzia 26 Rabii' al-Awwal hadi 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M.

Kampeni hii ambayo iliendeshwa chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) kwa kauli mbiu “Bishara Njema Ikatimia… inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!” Kimsingi ilimakinika katika kufafanua yafuatayo:   

1. Ukombozi huo unaonyesha utukufu wa Uislamu na Waislamu pindi Uislamu unapotekelezwa kivitendo, ukafiri utatoweka.

2. Kuwahakikishia Ummah wa Waislamu juu ya kutimia kwa bishara nyinginezo tatu za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kama ilivyo patikana ya mwanzo, ambazo ni kukombolewa kwa Roma, na nyingine mbili: kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume, na kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa nguvu. 

3. Kuwakumbusha Waislamu wajibu wa kufanya kazi kusimamisha tena Khilafah Rashidah, huku wakizingatia kuwa makafiri Wamagharibi, pamoja na makhaini waliweza kuivunja Khilafah mnamo 1342 H – 1924 M na wangali wanatia juhudi kubwa ili kuzuia kurudi kwa Khilafah wakitumia kila njia na mbinu.

Kampeni hii ilifanyika katika sehemu kadha wa kadha nchini Tanzania kama vile miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar, Mtwara (Eneo la Kusini), Tanga (Eneo la Kaskazini Mashariki) nk., kwa kutumia njia na mbinu kadha wa kadha kama vile ugawanyaji hotuba ya Amiri kwa umma: darasa maalumu misikitini na nje ya misikiti, mihadhara, bayan, khutba za Ijumaa, kanda za video, mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya wanachama wa Hizb kuelezea maalumati ya kampeni hii katika vituo vya runinga na redio, kama vile Island TV, na Chuchu FM (Zanzibar).

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru tovuti za Hizb ut Tahrir / Tanzania:

Ukurasa Rasmi wa Hizb ut Tahrir/ Tanzania
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir/ Tanzania
Akaunti ya Twitter ya Hizb ut Tahrir/ Tanzania
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Tanzania
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Tanzania

Alama Ishara za Kampeni

#فتح_القسطنطينية

#القسطنطينية

#İstanbulunFethi

#istanbul

#ConquestofIstanbul

#Constantinople

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 25 Juni 2020 11:48

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu