Ijumaa, 02 Jumada al-thani 1442 | 2021/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wilaya Tunisia: Kongamano la Khilafah 2020

"Mwisho wa Demokrasia… Twaapa kwa Mwenyezi Mungu Hamuna Chengine Isipokuwa Uislamu na Khilafah

Hizb ut Tahrir / Wilaya Tunisia mnamo siku ya Jumamosi 29 Agosti 2020 M ilifanya kongamano la Khilafah la kila mwaka kwa anwani: "Mwisho wa Demokrasia… Twaapa kwa Mwenyezi Mungu Hamuna Chengine Isipokuwa Uislamu na Khilafah, katika ukumbi wa mihadhara katika makao makuu yake yaliyo katika makutano ya Ariana-Soukra katika mji mkuu. Kongamano hilo lilitanguliwa na maandamano yaliyoandaliwa na mashababu wa Hizb ut-Tahrir asubuhi hiyo hiyo, wakibeba ar-Rayah al-'Uqab huku wakitamka kaulimbiu za Khilafah, na kumalizikia kwa kuingia ndani ya makao makuu ya Hizb na kujiunga na kongamano lake la kila mwaka.

Kuliandaliwa maonyesho ya vitabu vya Hizb kwa lengo la kuutambulisha mradi wa hadhara ya Kiislamu kulingana na maono ya Hizb na ijtihadi yake ya kisheria. Pia kulikuwa na uwasilishaji video ambazo zilielezea hali ya Umma kwa kukosekana kwa Khilafah, na kichocheo cha udharura wa kuharakisha kusimamishwa kwake na kuwaokoa wanadamu kutokana na dhulma na ukatili wa demokrasia na udanganyifu wa watawala na watetezi wake.

Baada ya kusomwa Qur'an Tukufu, Ustadh Abdul Raouf, Mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Hizb ut Tahrir / Wilaya Tunisia, alitoa kalima ya ufunguzi kwa kutaja kumbukumbu ya Hijra ya Mtume (saw) na kuzaliwa kwa Dola ya kwanza katika historia ya Waislamu kupitia mkononi mwa kiongozi wa Ummah huu mtukufu. Na yenye kuthibitisha kwamba kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu ndio njia na amali ya pekee ya kuinua Neno la Mwenyezi Mungu na kuhukumu kwa sheria yake katika ardhi.   

Kalima nyenginezo zilizozungumziwa ni "Demokrasia na Mavuno Uchungu," iliyotolewa na Ustadh Khabib Karbaka, "Ummah wa Kiislamu na Maandalizi ya Kimungu ya Kusimamisha Khilafah: Hijra ni Ushahidi", iliyotolewa na Ustadh Muhammad Ali bin Salim, "Bishara ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)", iliyotolewa na Ustadh Lisaed Al-'Ajili, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilaya Tunisia.

Kongamano hili lilihitimishwa kwa kalima "Twaapa kwa Mwenyezi Mungu Hamuna Chengine Isipokuwa Uislamu na Khilafah" iliyotolewa na Ustadh Muhammad Al-Nasser Shuwaikha, ambapo alituma ujumbe wazi na mfupi kwa watoto wa Waislamu na kwa watu wenye nguvu na uthabiti, kung'oa nidhamu hizi kwa mizizi yake na kuitikia wito wa Hizb ut-Tahrir, wa kumuitikia Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) na kuliinua Neno la Mwenyezi Mungu (swt) kwani katika hilo yapo mafanikio makubwa, na kinyume chake ni uovu na hasara kubwa.

Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilaya Tunisia

- Video Kamili ya Kongamano -

Mkusanyiko wa Picha

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 21 Septemba 2020 10:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu