Jumamosi, 10 Jumada al-awwal 1444 | 2022/12/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Kikao cha Wanahabari kwa Anwani: "Mapinduzi kutoka Tunisia... Changamoto na Matarajio"

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ilifanya kikao mnamo Jumanne, Januari 11, 2022, chenye anwani: "Mapinduzi kutoka Tunisia... Changamoto na Matarajio" katika makao yake makuu huko Ariana.

Kikao hicho kilianza kwa hotuba ya mjumbe wa afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, Ustadh Ahmed Tatar, ambaye aliitaja fahamu sahihi ya dini ya Kiislamu kuwa ni mfumo wa maisha, jamii na dola, na kwamba Uislamu haukomei tu kwenye masuala ya ibada kama unavyokuzwa na mtazamo wa Kimagharibi kuhusu dini, bali ni kwamba khumusi nne za hukmu za kisheria katika Uislamu zinahusiana na maisha ya kisiasa kama hukmu za kina maalum kwa kazi ya serikali katika uwanja wa uchungaji wa mambo ya watu, kusimamisha hudud (mfumo wa kuadhibu) za Mwenyezi Mungu, kuziba mapengo katika nchi za Kiislamu, na kubeba ulinganizi wa Kiislamu kwa watu duniani.

Ustadh Ahmed Tatar alisisitiza kuwa mapinduzi ya Januari 14, 2011, ambayo yaliwapa motisha wananchi wa eneo hili na kuwasukuma kuelekea kwenye mabadiliko, yaliwakilisha na bado yanawakilisha, katika sura yake ya kiishara, tishio la wazi kwa tawala za kikoloni za Magharibi zilizolazimishwa juu ya nchi yetu kwani wanamapinduzi walinyanyua kauli mbiu za kuziangusha tawala hizi za vibaraka, na hili ndilo lililozifanya dola za Kimagharibi kuhangaika kuyazika mapinduzi haya.

Ustadh Tatar aidha aliashiria kuwa “kupambana na ufisadi” kunaanza na kupiga vita chanzo kikuu cha ufisadi ambacho ni kuwazuia watu wa Tunisia kufurahia haki zao na kunyonya mali zao kutokana na uingiliaji wa nchi za Magharibi katika siasa za Tunisia na msimamo wake wa utawala ukizingatia kuwa wokovu wa Umma wa Kiislamu kutokana himaya ya Magharibi unaweza tu kupatikana kwa kufuata Sunnah za Muhammad (saw) pekee katika upande wa utawala na mfumo wa serikali.

Kisha Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayani Tunisia, Ustadh Khabib Karbaka, akahusisha sababu za mgogoro wa leo wa Tunisia na kituo cha kisiasa kinachohusika na sera rasmi ya dola, wawe ni watawala au wapinzani, kwani wao wako chini ya maazimio ya nchi za Magharibi na hawana utashi wa uhuru wa maamuzi.

Mkuu wa Afisi ya Habari alitoa wito kwa wataalamu wa sheria kuitazama thaqafa ya Hizb ut Tahrir, kwani ni maalumati yanayoelezea hukmu za kivitendo za Uislamu na maalumati yenye uwezo wa kuhuisha Umma wa Kiislamu, kama vile vitabu, Nidhamu ya Uislamu, Fahamu za Hizb ut Tahrir, Nidhamu ya Kijamii, Nidhamu ya Kiuchumi, Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah na sababu na dalili zake zenye mashiko.

Mwishoni mwa hotuba yake, Ustadh Karbaka alihuisha tena wito wa Hizb ut Tahrir wa kuwataka watu wanaomiliki nguvu nchini Tunisia wainue mikono yao kutoka katika kituo cha kisiasa ambacho kina mafungamano na duara mbalimbali za Magharibi na kujihusisha na mradi wa Umma wa Kiislamu kama njia ya kuondoa utegemezi wa Magharibi na sura zote za ukoloni.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

- Sehemu ya Amali za Kikao cha Wanahabari -

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu