Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Barua ya Wazi kutoka Hizb ut Tahrir nchini Tunisia Kwenda kwa Majaji
Hakuna Njia ya Kupata Uadilifu wa Kimahakama Isipokuwa Kupitia Uislamu
(Imetafsiriwa)

Bonyeza Hapa Kupata Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waheshimiwa Majaji,

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia inawasilisha kwenu barua hii ya wazi, ikiweka mikononi mwenu msimamo wa kisiasa na wa vyombo vya habari katika kuhakikisha kuwepo kwa idara ya mahakama iliyo huru na ufisadi na ubaguzi, yenye kulinda haki za watu na kuwa thabiti katika kuwahisabu watawala.

Waheshimiwa Majaji,

Nchi hii imeishi chini ya dhulma kwa miongo kadhaa iliyowachosha watu na kuwacha nyoyoni mwao ugumu na ukandamizaji iliyopelekea uasi na mapinduzi yao. Kilichojitokeza wazi akilini mwa watu ni madhihirisho ya ubabe, dhulma, na upotevu wa haki katika miongo yote iliyopita. Leo, baada ya wataalamu wa siasa kuunda udikteta walioufinika kwa sura ya uwongo ya pamoja na ya maridhiano kwa kisingizio cha "maslahi ya taifa," ambao wanataka, kwa mujibu wa madai yao maovu, kutegemea ukoloni na kupoteza mali ya nchi na kuikosesha pumzi kila nafsi ya kimapinduzi inayotamani ukombozi na mabadiliko ya kweli. Watawala, baada ya Julai 25, wanafuata njia ya watangulizi wao kwa kuunda kadhia za kando; kuimakinisha sera yenyewe kwa kuibebesha nchi na wananchi mzigo wa madeni yanayoendeleza ukoloni. Wanatafuta kuendeleza udhalimu wao kwa kutumia zana za sheria za kipekee chini ya shinikizo la dhurufu na muktadha wa kutisha ili kulazimisha hali isiyokuwa na budi watu kuikubali. Hawakosi sababu na uhalalishaji, mara moja chini ya kivuli cha "kupambana na ugaidi" na mara moja chini ya jina la "maridhiano ya kiuchumi", na mara moja chini ya jina la "kupambana na virusi vya Korona", na mara moja chini ya jina 'Jamhuri ya Tatu'.

Zaidi ya hayo, wataalamu wa masuala ya kisiasa wanataka idara ya mahakama kuwa njia tu ambayo mamlaka itaitumia kwa misingi ya ubaguzi, badala ya hitaji la awali la kuzalisha udhalimu mpya, inaohakikisha kuendelea kwao kwa kuzingatia kushindwa kwa hali ya juu kwa machaguo yao ya kifikra na kisiasa kushawishi watu au kuleta mabadiliko.

Enyi Majiji Waheshimiwa,

Kundi la mabwenyenye wachache ndani ya uongozi wa kisiasa wanalinda maslahi yao na ya wakoloni wao kupitia idara ya mahakama. Demokrasia inawaruhusu kuamua kipi kiruhusiwe na kipi kipigwe marufuku, halafu dori ya idara ya mahakama inakuja kulazimisha matakwa ya mabwenyenye hao!

Wanasiasa hawa, ambao baadhi yao wanajulikana kung’ang’ania maslahi yao na wengine ni watiifu kwa ajenda za nje wanataka kuwabebesha majaji madhambi yao kwa kuhalalisha dhulma. Inafahamika vyema kuwa utekelezaji wa sheria zilizorithiwa tangu enzi za dhalimu na utabikishaji wa sheria mpya zinazodhibitiwa na ajenda za kigeni na njama za giza utakuwa na athari, utata anuwai na madhara mengi ya hatari. Endapo haya yatahalalishwa na kutabikishwa, siku moja yatatajwa kuwa ni dhulma na udhalimu, na chombo kinachohusika na hili mbele ya wananchi kitakuwa ni mfumo wa mahakama.

Kisha, baada ya maasi, ghasia, au mapinduzi mapya, wanasiasa waliovalia mavazi ya wahubiri wanakuja kuzungumza juu ya haja ya kuitakasa idara ya mahakama, ingawa wao wenyewe waliwaagiza mahakimu kuorodhesha sheria wanazotaka! Wanasiasa hawa wasio na maadili si chochote ila ni watafutaji wa maslahi na madaraka, na baadaye watapata watu watakaowafuta vumbi ili wawawasilishe tena kwenye soko la kisiasa kama wanamageuzi, watu elimu na wazoefu wenye mikono safi, na hakuna njia yoyote ya kufikia mageuzi na wokovu bila wao!

Je, ni busara kwa mahakimu kudanganywa na kuhadaiwa na njama hizi licha ya kuwa wao ndio wajuzi zaidi wa mambo yaliyo nyuma ya pazia ya watawala hawa, na jinsi walivyoteuliwa katika nyadhifa hizo na, ni ni zipi mamlaka za kikoloni zenye kuwafadhili na kuwawekea dau ili kupanua ushawishi na udhibiti juu ya nchi hii?!

Enyi Majaji Waheshimiwa:

Mnajua kuwa uhalifu ni kitendo kibaya ambacho kinakiuka mfumo na kinahitaji adhabu, yaani, ni kitendo ambacho kinakiuka desturi ya kundi, au kitendo kisicho cha kawaida, au kitendo kilichoharamisha kutoka kwa mtazamo wa sheria iliyotungwa na mwanadamu au uhalali wa kimungu, unaohitaji adhabu hapa duniani au Akhera. Kwa hiyo, kitendo kibaya kinachokiuka mfumo kwa mtazamo wa Kiislamu ni kutenda kitendo kilichoharamishwa ambacho Shariah inakataza na matokeo yake ni adhabu au ni dhambi. Hivyo basi, naapa kwa Mola wenu, ni mifumo gani inayofaa zaidi kwa mwanadamu: mfumo wa Muumba au mfumo wa viumbe?

Mfumo wa Uislamu una sheria zinazohusiana na uhalifu, hukmu za ushahidi na vigezo vya adhabu, vyote hivyo kiasili vinatoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), na Mwenyezi Mungu (swt) ndiye aliyeumba viumbe na Yeye ndiye anayejua zaidi ipi ni haki kwao na hali zao.

 [أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ]

“Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Al-Mulk: 14]

Uislamu ni mfumo unaojumuisha mkusanyiko wa hukmu za kisheria za kushughulikia mambo ya watu, na ni lazima zitekelezwe kupitia idara ya mahakama bila ya upendeleo wowote au ubaguzi kwa msingi wa ushawishi, cheo, au suala jengine lolote. Inasisitiza kuhakikisha haki za wanyonge, bila kujali rangi zao, jinsia, dhehebu au dini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akiwaonya Waislamu, alisema: «... إِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهِمْ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمْ الضَّعِيفُ أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ وَايْمُ اللَّهِ لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا» “Enyi watu, hakika yale yaliyowaangamiza watu waliokuwa kabla yenu ni kwamba walikuwa anapoiba mtukufu wao humuacha; na anapoiba dhaifu miongoni mwao humsimamishia adhabu (haddi) juu yake. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, la Fatima binti Muhammad angeiba, ningeukata mkono wake.” [Imepokewa na Bukhari].

Hakuna kinga kwa mtawala yeyote, awe mfalme au waziri. Imeelezwa katika Utangulizi wa Katiba wa Hizb ut Tahrir katika Ibara ya 87: “Jaji wa Mahakama ya Udhalimu (Madhalim) huteuliwa ili kuondoa dhulma zote ambazo zimefanyiwa mtu yeyote anayeishi chini ya mamlaka ya Dola, bila kujali kama mtu huyo ni miongoni mwa raia wa dola au la, na bila ya kujali kama dhulma hiyo ilifanywa na Khalifa au yeyote aliye chini yake miongoni mwa watawala na watumishi wa umma.”

Enyi Majaji Waheshimiwa:

Kazi yenu ni mojawapo ya kazi bora na muhimu zaidi. Hakimu sio tu mtiifu kwa bwana wake, mtiifu kwa upofu kwa bwana wake, au shahidi wa uongo ambaye hana chaguo ila kutekeleza sheria kwa nguvu ya sheria; na kwa nini isiwe hivyo, na mnajua kwamba Siku ya Kiyama hakimu atakabiliana na hisabu kwa hofu kubwa kiasi kwamba atatamani asingegawanya tende baina ya watu wawili! Na mna dori kubwa katika kuiokoa nchi hii baada ya kuchoshwa na wanasiasa, ambao kwao wananchi hawakuona chochote zaidi ya kuvunjwa moyo baada ya kuvunjwa moyo na kukosa msaada baada ya ulemavu.

Tunawatahadharisha kuwa wanasiasa hawa wanataka kuhamishia mporomoko wao kwenye uwanja wenu, na wanataka mutegemeze nusu ya kesi zenu za kimahakama kwenye maandiko ya kisheria yaliyochakaa na mengine ambayo yametungwa kwenye vyumba vya giza, na muwasilishe nusu ya kesi hizo kwa muktadha wa kuogofya unaopangwa kwa ajili ya nchi ambayo sera za vyombo tembezi vya habari huzipeperusha kwa mahitaji, na hili lenyewe ni zaidi ya dhulma; ni uongo na uonevu. Ahmad na Abu Dawud wamesimulia kutoka katika Hadith ya Abu Talha al-Ansari na Jaber bin Abdullah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwa kutoka kwa Mtume (saw) ambaye amesema: «مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً في مَوْطِنٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ. وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ    نُصْرَتَهُ».  “Hakuna mtu (Muislamu) yeyote atakayemtelekeza Muislamu katika mahali ambapo utukufu wake unakiukwa na heshima yake kuvunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika mahali ambapo angependa nusra Yake. Na hakuna mtu (Muislamu) yeyote atakayemnusuru Muislamu katika mahali ambapo heshima yake inavunjwa na utukufu wake kukiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru katika mahali ambapo angependa nusra Yake.”

Katika fiqh ya sheria ya Kiislamu na hukmu nyenginezo za kisheria, yako ya kutosha kwa Umma wetu kuwa kama anavyotaka Mwenyezi Mungu uwe:

[خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ]

“bora ya umma walio tolewa watu.” [Aal-i-Imran: 110].

Na tutakuwa na dola kama ambavyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyotoa bishara njema: «خِلَافَةً عَلَى مِنهاجِ النُّبُوَّةِ»“Khilafah kwa njia ya Utume.”

Kwa hivyo, haki zinalindwa kwa ajili ya wote, na haziathiriwi na ubaguzi, na dhulma haizikaribii hata kidogo. Bali hukmu hutekelezwa kwa uadilifu kwa mtawala na watawaliwa, mnyonge na mwenye nguvu, bila ya ubaguzi hata kidogo, hivyo watu ndani yake ni kama meno ya kichana. «لَا فَضْلَ لِعَربِيٍّ عَلَى أَعْجَمِيٍّ وَلَا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ وَلَا لِأَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ وَلَا لِأَسْوَدَ عَلَى أَحْمَرَ إِلاَّ بِالتَّقْوَى» “Hakuna ubora kwa Muarabu juu ya asiyekuwa Muarabu wala kwa asiyekuwa Muarabu juu ya Muarabu, wala kwa mwekundu juu ya mweusi wala mweusi juu ya mwekundu isipokuwa kwa uchamungu.” kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Hivyo basi kuweni waangalifu, enyi majaji, kwa sababu wapo wanasiasa wanaokujaribuni kutunga sheria za dhulma zinazopingana na sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), na wapo wanaotaka kukutumieni ili kumakinisha mamlaka yao. Ama sisi katika Hizb ut Tahrir, tunawalingania kuhukumu kwa Uislamu, ambao ndio uadilifu aliouamrisha Mwenyezi Mungu (swt).

 [إِنَّ اللهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَنْ تَحْكُمُواْ بِالْعَدْلِ إِنَّ اللهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ إِنَّ اللهَ كَانَ سَمِيعاً بَصِيراً]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” [An-Nisa: 58].

Kwa hivyo, itikieni amri ya Mola wenu, na mutapata izza hapa duniani na kesho Akhera.

Tunisia, 8 Dhul-Qa’adah 1443 H sawia na 6 Juni 2022 M.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu